Ushauri kuhusu kusoma masters

Jamani asanteni kwa ushauri, me naamini Kila mtu katoa ushauri wenye kujenga, Mungu awabariki
 
Nani anakulipia ? Ni hela ya uhakika au ya kubangaiza ? we mwenyewe una nini mkononi.. biashara yoyote ?
 
Kwa GPA yake ni sawa tu akisoma Masters then ataomba nafasi za assistant lecturer huwa zinatangazwa mara kwa mara kwenye vyuo vikuu, ila Masters anapaswa apate GPA isiyopungua 4
 
Kwa GPA yake ni sawa tu akisoma Masters then ataomba nafasi za assistant lecturer huwa zinatangazwa mara kwa mara kwenye vyuo vikuu, ila Masters anapaswa apate GPA isiyopungua 4
Of course braza ukizingatia kuwa hakuna ajira serikalini kwa walimu wa arts.
 
Ndugu zangu wanajamvi mimi ni muhitimu wa chuo kimoja cha serikali, nimemaliza masomo yangu ya degree ya kwanza mwaka huu 2019.Nilikuwa nasoma ualimu (BED) na kufanikiwa kupata GPA ya 4.2 (Teaching subjects Ni geography and history)
Kama una ada na hela ya kujikimu kwa miaka 2 nenda kasome Geography ubobee. Kusoma kunapanua mawazo na hata kama utapata kazi hata kama ni ya kuajiriwa kusoma kunakuongezea uhuru. Mshahara hata kama sio mkubwa lakini hubanwi kama yule ambae hana hiyo masters. Pia masters inaweza kufungua milango ambayo degree ya kwanza inaweza isifungue.
Kama uko ki-academic basi na GPA yako unaweza kuanza safari ya kuwa mtafiti au mhadhiri vitu ambavyo vinahitaji Masters. Unaweza pia ukapata scholarship ukikomaa ili ukasome. Ukisoma au ku-specialise sehemu nzuri ya geography (ongea na watalaam) hata kujiajiri unaweza kwa mfano kuwa consultant (miradi, gis etc). La msingi usome ukiwa na malengo.
 
Nashukuru mzee ushauri nzuri Sana huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…