Ushauri kuhusu Fursa za kazi za muda(Vibarua) zilizopo Sweden

mkuu shida ya Sweden Scholarship lazima ulipe application fee for addmision
Kiongozi mmoja mkubwa mstaafu hapa Nchini aliwahi kusema " Ukitaka kula sharti ukubali kuliwa".

Kwahiyo kutoa admission fee ya takribani Tsh 230,000 ili upate Scholarship ya mamilioni siyo hasara kubwa Mkuu.!
 
Kiongozi mmoja mkubwa mstaafu hapa Nchini aliwahi kusema " Ukitaka kula sharti ukubali kuliwa".

Kwahiyo kutoa admission fee ya takribani Tsh 230,000 ili upate Scholarship ya mamilioni siyo hasara kubwa Mkuu.!
Sasa hapo siinakuwa probability ya schorship maana unaweza kutoa hiyo hella na huna uhakika wakupa scholarship
 
Sasa hapo siinakuwa probability ya schorship maana unaweza kutoa hiyo hella na huna uhakika wakupa scholarship
Mkuu, katika maisha usiogope ku-take risk. Tafiti zinaonesha kuwa watu wengi waliofanikiwa katika maisha haya wengi wao walifanya maamuzi magumu(ku-take risk).
 
Wakuu, nashukuru sana kwa wanaoendelea kutoa ushauri kuhusu mada yangu, ila kwa uchunguzi mdogo nilioufanya, inaonesha wadau huko Sweden wapo wengi na wanajuwa connections za hapa na pale kulingana na uhitaji wangu. Ila wana hofu kubwa ya kumkaribisha mtu na akawa mzigo kwake. Wanaona wakishatoa msaada basi itakuwa juu yao kuwa responsible kwa wanaye msaidia. Wengine wana hofu na kudhani huenda suala la shule ni geresha tu na nataka kuzamia kama wazamiaji wengine.

Kwa muktadha huo, naomba kuthibitisha kuwa mie siyo mzamiaji bali naenda kimasomo. Na sitohitaji kukaa/kuishi kwa mtu, na ikiwezekana sitolazimika kuonana na atakayenipa connection. Muhimu tu ni kupata connection na kujuwa kazi zipi zitapatikana na nitazipataje. Ikumbukwe sitohitaji Professional works kutokana na usumbufu wa kuzipata. Nahitaji non-skilled jobs. Karibuni kwa ushauri Wakuu.
 
Mkuu, wewe unaenda kama Mwanafunzi hauna Haja ya ku panic Wala Nini. Kila kitu ukifika kule kitaa kaa sawa. Kama vipi unaweza kuwasiliana na International office ya Chuo chako. Hakika watakusaidia.

Pia Kama mwanafunzi utahitaji kufanya Kazi masaa 20 tu kwa wiki, na kipindi Cha summer so wewe ukiingia kule utapata vibali kila kitu halafu utachagua Kazi ipi ufanye. Wewe jua Ukiingia Sweden utakuwa na uhakika wa Kazi.

Cha msingi jipange na Safari tuu. Mambo mengine utayakuta huko huko.
 
Nashukuru sana Mkuu. Naendelea kufumbuka zaidi..
 
Vizuri, ila international office itakupa taarifa zote kuhusu suala la kupata Kazi. Wasiliana nao. Wao watakupa mwongozo Mzuri.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…