Ushauri kuhusu Fursa za kazi za muda(Vibarua) zilizopo Sweden

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,046
Wakuu habari za Majukumu!

Kuanzia mwezi August natarajia kuwa Sweden. Nimepata Scholarship ya kusoma masters. Hivyo, kwakuzingatia hali yetu kiuchumi sisi Wabongo, tunapopata fursa moja basi hujaribu kuangazia hapa na pale kuhusu fursa nyingine zaidi.

Muda ambao nitakuwa free, haswa wakati wa research na wakati mwingine ambapo masomo yanakuwa hayajachanganya, nataka niwe nafanya kazi ya muda (Part time job). Kwakuwa JF ni wajuvi wa kila jambo chini ya jua hili, naomba mwenye kujua ABCD kuwa nitakapofika nipate vipi channel ya kufanya kazi yoyote.

Nipo tayari kufanya kazi yoyote hata kama ni kukatia ng'ombe nyasi za kuwalisha, kusambaza magazeti, kuosha magari au kufanya usafi. Muhimu iwe ni kazi halali na iniingizie kipato. Angalau kwa mwezi niweze kutengeneza SEK 10,000.

Nitakuwa kwenye mji unaoitwa "Umea". Chuo nachoenda ni "Umea University ".

Sihitaji professional works hivyo naomba nisiulizwe mimi ni mtaalamu wa mambo yapi.

Mwenye ushauri wa kwamba, niachane na masuala ya kuulizia kazi na nikazingatie tu masomo naomba ushauri huo auache kwanza kwa sasa, awape nafasi wadau wenye connection ya kazi kwanza.

................ . UPDATES................

Wakuu, nashukuru sana kwa wanaoendelea kutoa ushauri kuhusu mada yangu, ila kwa uchunguzi mdogo nilioufanya, inaonesha wadau huko Sweden wapo wengi na wanajuwa connections za hapa na pale kulingana na uhitaji wangu. Ila wana hofu kubwa ya kumkaribisha mtu na akawa mzigo kwake. Wanaona wakishatoa msaada basi itakuwa juu yao kuwa responsible kwa wanaye msaidia. Wengine wana hofu na kudhani huenda suala la shule ni geresha tu na nataka kuzamia kama wazamiaji wengine.

Kwa muktadha huo, naomba kuthibitisha kuwa mie siyo mzamiaji bali naenda kimasomo. Na sitohitaji kukaa/kuishi kwa mtu, na ikiwezekana sitolazimika kuonana na atakayenipa connection. Muhimu tu ni kupata connection na kujuwa kazi zipi zitapatikana na nitazipataje. Ikumbukwe sitohitaji Professional works kutokana na usumbufu wa kuzipata. Nahitaji non-skilled jobs. Karibuni kwa ushauri Mkuu.
 
Mi mwenyewe natamani sana kwenda uko sijui tu pa kuanzia maana bongo kwa sasa hapakaliki.
Mkuu, weka tu nia na muhimu uwe na sifa za kufika. Mfano ni kwa ajili ya masomo. Kingine muombe Mungu afanikishe matarajio yako kwa kuzingatia mapenzi ya Mungu.
 
Mtafute Dr. Slaa, yupo huko anaweza akakurushia dodo, huwezi jua.
hata Jon Stephano anaweza akakupa maushauri na michongo pia.
Mkuu, Dr. Salaa yeye ni Balozi na tayari alishatoboa maisha haya. Sasa Balozi na " Unskilled jobs" wapi na wapi. Natafuta connection ya wavuja jasho wenzangu. Lengo nitengeneze SEK 10,000 kwa mwezi kupitia " Unskilled labour "
 
Hongera Mkuu, umea Ni mji Mzuri sema winter Kuna full barafu tofauti na Stockholm. Kazi zipo kibao ukifika unaweza kufanya Restaurant au kwa wafugaji kozi wanafuga. Nilishawahi fika hicho chuo Ni mmoja ya Chuo kizuri sana. All the best. Nipo bongo now. Nilienda kutembelea marafiki miaka kadhaa iliyopita.
 
Mji unao kwenda kwaajili ya kusoma ni mji mdogo sana hasa katika harakati za kupata kazi tofauti na miji mikubwa
 
Hongera Mkuu, umea Ni mji Mzuri sema winter Kuna full barafu tofauti na Stockholm. Kazi zipo kibao ukifika unaweza kufanya Restaurant au kwa wafugaji kozi wanafuga. Nilishawahi fika hicho chuo Ni mmoja ya Chuo kizuri sana. All the best. Nipo bongo now. Nilienda kutembelea marafiki miaka kadhaa iliyopita.
Nashukuru kwa ushauri huu muhimu Mkuu. Naona pia ili upate kazi ambazo siyo professional inatakiwa uwe unafahamu lugha yao. Hapa najaribu kupambana kujifunza online mpaka kieleweke.

Suala la baridi nitapambana tu Mkuu. Hakuna namna. Muhimu nipo huko majuu..
 
Mji unao kwenda kwaajili ya kusoma ni mji mdogo sana hasa katika harakati za kupata kazi tofauti na miji mikubwa
Sawa Mkuu. Ila hakuna kukata tamaa. Ngoja nijaribu bahati yangu pia kwa chochote kitakachowezekana.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom