Ushauri kuhusu duka la reja reja

Ushauri kuhusu duka la reja reja

Sicario poison

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2021
Posts
2,327
Reaction score
4,575
Wakuu habari za leo..
Nadhani wote mu wazima wa afya na mnaendelea na mitikasi ya maisha
Mimi ni kijana wa miaka 20 ambaye Nina ndoto za kufika mbali..mwaka Jana baada ya shule nilijiweka mtaan na kujifunza njia mbali mbali za kujipatia kipato na mwaka huu nimefanikiwa kupata laki tisa kutokana na shughuli za kilimo ingawa ilikuwa niwe na zaidi ya hiyo pesa sema nilitapeliwa pia kiasi cha laki tano[emoji22] na sikuwa na uwezo wa kumfanya chochote yule bosi wangu
Kwa kufupisha wakuu ningeomba ushauri wenu maana nataka nifungue duka la rejareja na sehemu niliopo ni kijijini na vipi hiyo pesa itatosha kweli pia na Mambo mengine muhimu..ushauri wenu unaweza kuwa msaada mkubwa sana kwangu
Ahsante sana
 
Back
Top Bottom