Inashangaza michango ya wengi hapa. Ni kukatisha tamaa zaidi.
Ina maana hizo gari zinaletwa Tanzania kwa makusudi gani ?
Wakati mwingine, inabidi uyapokee maoni ya watu kwa hadhari sana, maana kila jambo utakalotaka kufanya watakuambia haiwezekani.
Lakini kila siku, tunaona gari barabarani zimebeba mizigo.
Ushauri ni kwamba, kama unafikiria kuanzisha biashara hiyo , uwe na mpango kazi ( business plan)
Fungua kampuni ya usafirishaji.
Tafuta makampuni ambayo unaweza kuwapa huduma ya usafiri wa kutumia gari yako.
Mfano, kuna makampuni ambayo ni distributor .... Hawawezi kufika kila eneo katika mji huu wa DSM hapo ndipo unaweza ukaingia.
Hebu angalia mtaani kwako, bidhaa gani zinaletwa kwa magari , unaweza ukapata idea, ongea na madereva kutaka kujua undani kidogo wa mambo. Bidhaa ni nyingi, kuna mikate, maji, bidhaa mbalimbali za duka nk.
Fanya biashara na makampuni , watakuwa wanahitaji huduma ya usafirishaji .
Ni bora ukajiingiza kwenye kutafuta soko kwa ajili ya gari, kuliko kumuachia dereva jukumu hilo.
Unapomuachia dereva jukumu hilo, basi matokeo yake dereva anafanya chochote, ambayo italeta madhara kwa mwenye gari.
Dereva aajiliwe tu kwa ajili ya huduma na alipwe mshahara .