Ushauri: Kufanya kazi ambayo siyo uliyosomea

Ushauri: Kufanya kazi ambayo siyo uliyosomea

evamajo

Member
Joined
Apr 12, 2014
Posts
11
Reaction score
1
Habari zenu wana JF!

Imepita miaka miwili sasa tangu kijana huyu mtanzania amalize Advanced Diploma ya Computer Science hana kazi!
Wiki iliyopita anakutana na kazi eneo ambalo hakutegemea... kazi ya kuwa mwalimu wa sekondari.
katika kazi hii ~mshahara ni 300000 kwa mwezi.
~Ni kwa masaa tisa kwa siku.
~mazingira ya kazi ni kijijini,
Anaomba ushauri kuwa ni sahihi kwake kufanya kazi hii au ndio atakuwa anapoteza future yake?
wenye uzoefu tafadhali
 
kwa ushauri wangu nenda kapige mzigo, masharti ya kazi hupati kazi kama huna kazi, hapo ndio chanzo chakupata kazi nyingine.
 
Nenda tu kapige mzigo,tangu nimalize chuo mpk sasa nimefanya kazi sehem tatu tofauti..na zote hakuna niliyosomea lkn maisha yanasonga.pia mwaka jana nilipata kazi inayoendana na nilivyosoma lkn sikwenda kureport nikawaachia wengine..
So angalia maslahi sio ulivyosoma..
 
Akafanye hyo kazi ni bora, kuliko kukaa bure, pia hyo hela itamsaidia katika kuhangaikia kaz nyingine
 
Nenda tu kapige mzigo,tangu nimalize chuo mpk sasa nimefanya kazi sehem tatu tofauti..na zote hakuna niliyosomea lkn maisha yanasonga.pia mwaka jana nilipata kazi inayoendana na nilivyosoma lkn sikwenda kureport nikawaachia wengine..
So angalia maslahi sio ulivyosoma..

nafurahi kwa kunifumbua macho.
 
Mchagua jembe sio mkulima.....kazi ya ualimu ni ngumu lakini haimaanishi kwamba si kila mtu anaweza kuifanya.......cha msingi azingatie maadili yanayoendana na hiyo kazi....hilo ndilo kubwa zaidi..commitment na uwajibikaji wenye tija vitampelekea kufungua milango ya mafanikio na.kupiga hatua zaidi
 
Kapige kaz,mm pia nlimalza degre ya uhasib 2011 toka hapo had leo nmekuwa nafundsha bt mshahar 500000,juz kuna mtu ambaye ni rafk yak na kak amesema ataniita anfundshe kaz 2months then niwe employed kama mhasib so komaa kwan hujui utatokea wapi!
 
kuna changamoto zipi ambazo umekumbana nazo huko
 
Mchagua jembe sio mkulima.....kazi ya ualimu ni ngumu lakini haimaanishi kwamba si kila mtu anaweza kuifanya.......cha msingi azingatie maadili yanayoendana na hiyo kazi....hilo ndilo kubwa zaidi..commitment na uwajibikaji wenye tija vitampelekea kufungua milango ya mafanikio na.kupiga hatua zaidi

naomba kufahamu kwa ufupi juu ya maadili ya kazi hii na ugumu wa kazi pia.
 
Tena asifikirie aende akafundishe watu tumekomaa kutafuta kazi za course tuliyosoma tukapoteza mda na sasa tunafanya kazi ambazo sio fani zetu

Kazi ni kazi kikubwa maslah
 
Tena asifikirie aende akafundishe watu tumekomaa kutafuta kazi za course tuliyosoma tukapoteza mda na sasa tunafanya kazi ambazo sio fani zetu

Kazi ni kazi kikubwa maslah

Noted!
 
mie napenda nitafautiane na woote waliokushauri. huko kijijini unaenda kujizika, opportunity nyingi achia mbali kupata uwezo wa kuzigombania bali hata kuzisikia. utaishia huko hadi ukija kushtuka kufunga banda , farasi atakuwa tayari ametoka....
kuwa makini kwani watu wengi imewapata hiyo
fanya kazi usiyosomea ili ikusaidie kimaisha huku ukiangalia maslahi na uwezekano wa kupata carrier yako
 
Back
Top Bottom