Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 6,289
- 10,999
Wadau Nina mdogo wangu ana umri wa miaka 30, anaishi chumba cha kupanga na amejiajiri, mwaka juzi alitaka kuoa lakn kwa bahati mbaya aliachana na mchumba wake baada ya kumfumania!. Mwanzoni mwa mwaka Jana alianza mahusiano na binti mmoja ambaye alionyesha dhahiri kumpenda kijana, binti huyu anaishi kwa kakake na pia anajishughurisha na biashara ndogondogo, Kwa ujumla binti anaonekana mvumilivu na mwenye mapenzi ya dhati pia hana sifa mbaya mtaani!
Tatizo ni kijana anadai pamoja na kupendana kwote ila nyota zao haziendani! Anadai yeye nyota yake ni moto, na nyota ya binti huyo ni maji! Hivyo eti wakioana hawatofanikiwa kimaisha! Sio siri kijana anampenda sana binti huyo binti pia anampenda na kumjali tatizo ni hiyo imani ya kinyota imetawala kichwa cha kijana Hutu! Mimi binafsi sina utaalamu wa elimu ya nyota hivyo kwa mwenye uelewa juu ya hili naomba anisaidie kujibu maswali haya. Je ni kweli kuna uhusiano kati ya nyota na mafanikio? Je kwa jinsi hawa watu wanavyopendana wakioana nini kitatokea? Je wote waliofanikiwa katika ndoa walioana kwa kufuata imani za kinyota?
Natanguliza shukrani!