Dar mkuu.
Kila biashara huku inalipa. Kikubwa umakini na juhudi.
Ingawa kama una mwenyeji ingekua poa zaidi maana unahitaji mwezi mmoja wa kujua eneo zuri la biashara yako, na mahala utakapokua unatoa mzigo na mahali utakapo kaa (kodi chumba).
Kama mwenyeji poa zaidi. Atleast unaweza jua jinsi utakapoanzia.
Maeneo kama Sinza unaweza pata hadi chumba kwa 50-70 kwa mwezi ingawa kuna michango kama Maji, umeme na usafi inaweza fika 20 kwa mwezi, hafu biashara zako ukawa unafanya Mawailiano, hadi Mwenge. Hapo ata dala dala haupandi unatembea tu.
Kama bishara zako haziitaji fremu unaibuka Kariakoo ingawa uko itabidi ukakae nje ya mji kidogo kule nyumba hazigusiki.
Karibu sana mzee baba waambie wakazi wa Ipogoro Kihesa Ilula Kidamali Kalenga hadi TRM wakuombee.