Ushauri Juu Ya Tatizo la Nyongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri Juu Ya Tatizo la Nyongo

Discussion in 'JF Doctor' started by Wit, Apr 11, 2011.

 1. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele Wakuu, nina dada yangu ameugua muda mrefu kdg na hosp wamekuwa wakimwambia ni tatizo la nyongo imezidi mwilini na kuzagaa kny damu! Kwa hakika ametumia dawa nyingi na tumeshawaona specialist wengi lkn bado hali yake inazidi kuwa mbaya! Naombeni wataalamu hapa wanisaidie kujua nyongo ikisambaa kny damu dalili zake ni zipi na inasababishwa na nini?! Nawiwa kujua hilo kwa kuwa imetupa utata sana hivyo natamani nipate maoni ya wakuu hapa,vile vile naomba kujua kama hili tatizo huwa linahitaji operation.Asanteni
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Kuna tofauti kidogo kati ya 'nyongo' na 'manjano', japo magonjwa mengi (kama siyo yote) ya nyongo dalili yake ni manjano. Tofauti ni kuwa manjano ya nyongo huwa yanaambatana na kuwashwa mwili. Kama una uhakika tatizo ni nyongo, basi kuna ulazima wa huyo mgonjwa kuonwa na daktari bingwa wa upasuaji, kwa sababu mara nyingi manjano ya nyongo huwa yanasababishwa na kuziba kwa mfuko wa nyongo (gall bladder), na mara nyingi tena kuziba kwa mfuko wa nyongo kunahitaji upasuaji kama tiba.

  Kama si nyongo, bado dada atahitaji vipimo mbali mbali hasa vya damu kugundua manjano yake yanasababishwa na nini. Kuna matatizo kadhaa ya damu ambayo husababisha manjano. Manjano pia yanaweza sababishwa na matatizo ya maini, hivyo atahitaji pia kufanya vipimo vya kuonyesha kama ini lake linafanya kazi vyema.

  Mpeleke dada kwenye hospitali yenye wataalam na uwezo wa kufanya vipimo hivyo ili tatizo lijulikana na apate tiba inayostahili.
   
 3. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Riwa asante sana kwa maelezo makini,binafsi niko mbali na dada yangu umenipa kitu kipya khs manjano,ukweli ni kuwa anawashwa sana,ngozi yake imekuwa nyeusi sana na kukakamaa,pia macho yamekuwa njano,naambiwa pia anachoka sana,kutapika,na kuharisha kidogo.Mkuu amepima vipimo vingi kikiwemo cha ini ameambiwa liko na vipimo vya mara ya mwisho amefanyia kcmc ambapo ataenda tena kesho kwa vipimo vingine nadhani ni hiyo bleda unayosema imeziba, Swali lingine ni kuwa eti kuna operation ya kutumia mionzi bila kupasuliwa? Na manjano inasababishwa pia na nyongo? Je baada ya operation hiyo haitamsumbua tena? Asante sana nasubiri majibu mkuu
   
Loading...