Nimekuwa na uhusiano na msichana mmoja kwa muda wa mwezi mmoja na tuliahidiana mambo yakikaa sama tutaoana kwani tayari wazazi wanajua kuhusu swala hili.
Lakini kinachoniumiza ni kuwa nina rafiki yangu wa karibu ambaye anadai kuwa anasumbuliwa na huyu dada jambo ambalo kwa mara ya kwanza sikuliamini, lakini nilikuja kuamini baada ya kuona ujumbe wake simu ya rafiki yangu na pia siku hizi hana furaha yoyote anapokuwa na mimi na ninapomuuliza anakuwa mkali kidogo kwenye kunijibu. Jambo lingine linaloniumiza ni kuwa amekuwa akiwatangazia watu kuwa mimi ninamsumbua kimapenzi kitu ambacho sikufanya ila uhusiano wetu ulikuwa wa makubaliano kati yangu mimi na yeye.
Yani kwa sasa sijui nifanye kwa sababu wazazi wote wanajua wazi kwamba muda si mrefu tutafunga ndoa na mambo anayofanya ndo kama hivi, nifanyeje? Nikisema nimuache nitachora picha mbaya kwa wazazi wangu na wake kwa sababu wazazi wangu wanampenda sana dada huyu, na wazazi huwa wanamsifia mtoto wao kuwa ni mwenye tabia njema nifanyeje?