Ushauri juu ya kuoa!

Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
81
1: Usioe kwa sababu umechoka kula kwa mama lishe>>Mke sio mpishi kama umechoka kula kwa
mama lishe jifunze kupika.

2: Usioe kwa sababu umechoka kufua na kupika >>Mke sio housemaid, kama umechoka kufua ajiri mtu akufulie.

3: Usioe kwa sababu rafiki zako wote wameoa >>Mke sio mashindano maana hataishi na marafiki zako wala sio zawadi kwa wazazi wako bali wewe ndiwe utakayeishi naye.

4: Usioe kwa sababu unataka kufungua kanisa sasa unatafuta ama mchungaji

5: Usioe kwa sababu wazazi wanakulazimisha maana dada zako wote wameshaolewa.

6: Usioe kwa sababu mpenzi au mchumba amepata mimba yako.

7: Usioe kwa sababu unataka kumuonyesha msichana aliyekuacha kuwa bado upo juu.

8: Usioe kwa sababu unamhurumia msichana uliyenaye ukimuacha atachanganyikiwa.

9: Usioe kwa sababu wazazi wako wanampenda na kumkubali msichana huyo.

10: Kuliko kumuoa msichana kwa kumhurumia na si kumpenda itapelekea kuteseka moyoni maisha yenu yote ni afadhali umwambie
ukweli kungali mapema.

11: Kuoa ili kujionyesha kuwa ume- move on baada ya kuachwa ni kujikomoa mwenyewe.
Oa ukiwa na uhakika kuwa huyo ndiye chaguo lako pekee na upo tayari kuishi naye katika hali zote, ndio mpango wa Mungu katika maisha yako na ndiye unayempenda kwa moyo wako wote.
 
Hizo ni tabia za kuelekea ushoga mkuu,wewe dume zima na gorola zako 2 tena hai utapikaje?? Aah pika mwenyewe! Mimi sipiki ng'o!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom