Ushauri juu ya kuanzisha consultancy firm

Drat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
966
1,069
Habari ndugu zangu JF?
Kutokana na ugumu wa upatikanaji wa ajira, nimekuwa na wazo la kujiajiri kwa kuzingatia taaluma yangu na ujuzi kiasi katika masuala ya sheria ya kodi na usimamizi, na pia uchumi.
Lengo langu hasa ni kujikita katika masuala ya wa kodi.Ninachooma kusaidiwa ni yafuatayo:
1. Je huduma hii bado ina kipato kizuri kwa small firms?
2. Kwa kawaida malipo ni kiasi gani kwa maandalizi ya hesabu(Yearly Financial Statements,VAT returns e.t.c)?, naomba kupewa wastani, natambua workload zinatofautiana kulingana na kazi inayopatikana.
Thanks in advance,Natanguliza shukrani zangu kwenu
 
Mkuu utatoa vipi ushauri kuhusu kodi wakati hata VAT return hujui kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu utatoa vipi ushauri kuhusu kodi wakati hata VAT return hujui kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani haujaelewa ninachouliza, nimemaanisha kwa mfano mi nina biashara nikitaka wewe kama business consultant uniandalie hesabu za VAT utataka malipo kiasi gani, kwa hiyo nilitaka kujua wastani wa bei.
 
Unataka tukupangie bei?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu anapotaka kujua wastani wa bei ya bidhaa au huduma fulani we unaona ni sawa kuhitaji apangiwe bei ya bidhaa au huduma anayotaka kuitoa?
Unataka tukupangie bei?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka tukupangie bei?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimehitaji kujua wastani wa bei, sio kupangiwa bei, au kwa uelewa wako kwa mfano kama kampuni inaandaa mradi halafu katika study yao wakataka kujua prevailing salary scale, je wanakuwa wanataka uwapangie mshahara?
Sikujui lakini inaonekana we ni mtu wa kejeli,kebehi na ngebe kutokana na matokeo fulani mazuri ya kimaisha ambayo unayo. Mungu akulinde sana cuz mambo yakibadilika hata watu wako wa karibu watakukataa.
 
Niwie radhi mkuu rudisha laana ulizonipa. Nitajaribu kuwa mwelewa zaidi mbeleni hata pale ninapichukizwa na uvivu wa wazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza Kabisa ili uwe Tax consultancy na umiliki firm yako ni lazima upate kibali kutoka TRA na ili upate hicho kibali ni lazima uwe na uzoefu wa kuanzia miaka mitatu na kuendelea katika maswala ya kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu malipo utakayopata kutoka kwa wateja, malipo yake ni mazuri sana kama utakua na nidhamu ya kazi na utapata wateja wengi sana kwani wateja hua wana tabia ya kuambiana endapo utakua unatoa huduma nzuri. Ukiwa na wateja 10 wa uhakika huna haja ya kuajiriwa na mtu yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu utachagua ww wapi ubase... kama kuhusu financial statements itategemea na ukubwa wa kazi let say kampuni iko na subsidiaries kibao and wanafunga mahesabu kwa pamoja yaan consolidation accounts hapo utatoza pesa nyingi kiasi kutokana na ugumu wa kazi yenyewe.. pia kama kampuni unataka kudeal na tax consultants only hapo utahitaji kutoza kutokana na ishu zenyewe.. maana wengine wanataka upige dili nzito za ukwepaji kodi na ishu kama hizo.. Bei zake huwa haziko constant.. Muhimu kutoza kulingana na FAINI husika wakati wa kufanya manuva yako ili hesabu ikae sawa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom