myhny
Senior Member
- May 27, 2014
- 123
- 23
Kuna dada mmoja alikuwa na mwanae alomzaa bila kuolewa kaishi nae mpaka kafika mtoto darasa la 5 .kunasiku yule dada alipotelewa na pesa yake elfu kumi haijulikani kama yule mtoto aliiba pesa ya mama ake au ilipotea tu .kamuhoji mwanae akakataa na kusema hakuchukua hiyo pesa ilikua asubuhi akamwambia nikurudi niikute hiyo pesa karudi jioni jibu lilikuwa nihilo hilo kwamba yule mtoto hakuchukua pesa .yule dada akachukua mafuta ya taa na kumwagia mwanae na kumuwasha na kiberiti akatoka .mda majirani wakasikia kerere mpaka wanafika hapo nyumbani mtoto kaisha zimia .ndo na yule dada kurudi akajifanya hajui kitu na kumpeleka mtoto hospital baada ya siku tatu mtoto kuhojiwa akasema mama kanichoma ikabidi yule dada afungwe .ushauri unakuja hapa bibi wa huyo mtoto anasema eti zilikuwa hasira na shetani wakija kumhoji tena polic aseme ni hasira ni kweli huyu mama anastahiri kufungwa ama ni hasira tu
