Ushauri jamani

PLATO MAGELE

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
203
Reaction score
54
Kuna mwanamke nilimpenda sana na tukapeana ahadi ya kuoana, baada ya makubaliano hayo alikuwa na mtoto nikaamua kumsomesha kwenye shule ya English medium karo zaidi ya milioni moja na mtoto huyo sasa mwaka huu atakuwa darasa la sita. Mgogoro katika mahusiano umeanza baada ya yeye kuanza kumiliki hela nyingi za kwake. Kipindi nampata alikuwa mnyenyekevu sana, mwenye upendo na utii usio wa kawaida kwangu. Kwa sasa siko karibu naye nikipiga simu hata hapokei kabisa. Jamani mimi nifanyeje?
 
Ulijitwika mzigo usio wako...hizo kazi za kusomesha huwa wanafanya waliooa...
Lakini pia kama uliifanya kwa moyo wa upendo huna haja ya kutumia kama kigezo cha kuonewa huruma...
Hapo nikisema ulikua buzi sijui utakasirika, nashukuru hata ukinitemea mate yataishia kwenye skrini ya simu au dadavuzi yako.
 

Hana thamani ya penzi lako, huoni kwamba 'it could have been worse'? Fikiria umeshafunga naye ndoa ya kanisani sijui ambayo ni mpaka kifo kiwatenganishe halafu akaja akaonesha her true colors.

Mungu kakuepushia kichomi, na in God's time utapata mke ambaye utakuja toa ushuhuda na kumshukuru Mungu kwa kukuepushia hicho kichomi.
 
Kisicho riziki hakiliki, achana naye, Mola atakulipa siku moja jasho lako.
 
MMmmhh...kuna watu wanapenda majukumu jamani.....Sijui mm mapenzi sina....yaani mtu nimkute ana mtoto...halaf nianze kumsomeshea...khaa..kwani breweries wamefunga kile kiwanda???Pole sana mkuu..siku nyingine usiwe na akili za mbayuwayu!!!changanya na zako kidogo...Naamini huyo mtu alikaa nawe kwa ajili ya pesa tu....punguza..:majani7:
 

skiza mkuu ulichoanya hapo ni sawa nakutoa sadaka kanisani au kusaidia wasiojiweza nenda kwenye nyumba za ibada kamuombe mungu akuzidishie kwa kile ulichafanya..

#Mapenzi +Pesa
 

dats tru buddy..
 
Inaonyesha hakukupenda kwa dhati ama alikukubali sababu ya msaada wako kwake..
Usipoteze mda ongea nae ujue kimoja
 

Asante kwa ushauri
 

Pole sana mkuu kwa hiyo changamoto ...
Nashindwa kuchangia sana maana umesema kuwa mgogoro ulianza baada ya yeye kuanza kumiliki pesa nyingi. Ktk hali ya kawaida ni vigumu mtu kubadilika kwa kupata pesa pekee yake, lazima kutakuwa na chanzo halisi cha tatizo maana inaweza kuwa hata umiliki wake wa pesa nyingi kwa upande wako umekuwa tatizo na kukufanya ujijengee hali ya kujidharau au pengine kuona unadharauliwa.

Hebu kaa chini na jaribu kuchunguza chanzo cha tatizo bila kufikiria suala la yeye kumiliki pesa nyingi ...
Kwa sehemu nafahamu mabadiliko ya kisaikolojia yanayoweza kumpata mwanaume aliyekuwa na uwezo mkubwa kuliko mpenziwe mambo yanapogeuka na yeye kuwa na kipato cha chini kuliko mpenziwe ...!
 
Nimekua mara nyingi sana nikisema hapa mafanikio kwa baadhi ya binadamu ni mtihani mkubwa sana.
"
Ndugu yangu PLATO pole sana
"
Ulimuonesha upendo wa kweli lakini kama ilivyn kawaida yetu wanadamu(mara nyingi wanawake) unapooneshwa upendo na mtu unamuona mjinga
"
Najua namna unavyoumia(i've been there for several times)Napenda kukuambia usijali
"
Kitu kikubwa cha kufahamu ni kwamba,huwezi kuumia milele,maumivu hayo yataisha tu
"
Sijui ni muda gani ameanza vituko hivyo ila weka time frame kama hajaeleweka move on
"
Atakupotezea muda,haijalishi amekutia hasara kiasi gani,hilo huwezi kulifuta,pia huna la kufanya kama hataki kuwa na wewe
"
Usiangalie ulichopoteza angalia mbele,fanya juhudi kujaribu kuokoa uhusiano wenu ikishindikana achana nae
"
Utaweza tu!
 

Haya ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…