Ushauri: Hataki afanye kazi yoyote ile.

Ushauri: Hataki afanye kazi yoyote ile.

Mundana

Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
84
Reaction score
114
Habari za jumapili na poleni na majukumu ya kila siku.
Bila kupoteza muda nina rafiki yangu wa kike tulipotezana muda mrefu sana. Sasa hivi karibuni tumekutana tena yeye tayari ameshaolewa na ana watoto wawili na ndoa inaelekea mwaka wa 5.

Sasa kikubwa mwanaume aliyekuwa nae ana wivu uliopitiliza hataki mwanamke afanye kazi yoyote ile, yeye ni wa kukaa nyumbani tu kulea watoto, akitoka sehemu yoyote anamfuatilia hataki awe na marafiki wa aina yoyote ile yeye ni nyumbani tu na yeye na kama akitoka sana basi ameenda kwa wazazi wake kuwatembelea na hapo lazima apige simu kuhakikisha kama kweli yupo na huwa anampeleka na kumrudisha. Na hataki ajiunge na mitandao ya kijamii yani yeye ni mama wa nyumbani tu.

Mwanamke hapendi hii hali na amewaambia wazazi wake(yeye mwanamke) lakini wamemwambia kuwa aendelee tu kuvumilia kwa kuwa hata wazazi wake wanafahamu tabia ya huyo mwanaume na mpaka tumeachana haielewi afanye nini amekuwa kama mtumwa sasa.

Naombeni ushauri wenu wanajamvi, naamini hapa kuna watu wenye hekima na busara zao.

Tumsaidie huyu mwanamke.

NB; Hii ndio thread yangu ya kwanza hivyo Naombeni ushirikiano wenu
Jumapili Njema.
 
Dah!!! Na awe pole kama anampenda mumewe na avumilie tuuu
 
awe mpole, miaka yote hiyo aendelee tu, huku atahatarisha bure ndoa yake
 
Habari za jumapili na poleni na majukumu ya kila siku.
Bila kupoteza muda nina rafiki yangu wa kike tulipotezana muda mrefu sana. Sasa hivi karibuni tumekutana tena yeye tayari ameshaolewa na ana watoto wawili na ndoa inaelekea mwaka wa 5. Sasa kikubwa mwanaume aliyekuwa nae ana wivu uliopitiliza hataki mwanamke afanye kazi yoyote ile, yeye ni wa kukaa nyumbani tu kulea watoto, akitoka sehemu yoyote anamfuatilia hataki awe na marafiki wa aina yoyote ile yeye ni nyumbani tu na yeye na kama akitoka sana basi ameenda kwa wazazi wake kuwatembelea na hapo lazima apige simu kuhakikisha kama kweli yupo na huwa anampeleka na kumrudisha. Na hataki ajiunge na mitandao ya kijamii yani yeye ni mama wa nyumbani tu.
Mwanamke hapendi hii hali na amewaambia wazazi wake(yeye mwanamke) lakini wamemwambia kuwa aendelee tu kuvumilia kwa kuwa hata wazazi wake wanafahamu tabia ya huyo mwanaume na mpaka tumeachana haielewi afanye nini amekuwa kama mtumwa sasa.
Naombeni ushauri wenu wanajamvi, naamini hapa kuna watu wenye hekima na busara zao.
Tumsaidie huyu mwanamke
NB; Hii ndio thread yangu ya kwanza hivyo Naombeni ushirikiano wenu
Jumapili Njema.

Namuunga mkono jamaa kwani wanawake wanadanganya sana na kupinduana mno. Mwanamke amvumilie tu jamaa ipo siku tutakutana nitamuonya ajirekebishe na kumpa uhuru mkewe.
 
Acha kuingilia ndoa ya mwenzako, acha waishi wapendavyo, Mwambie avumilie
Mkuu mimi sijaingilia ndoa ya watu mbona.
Amekuja mwenyewe kuomba ushauri afanyaje
 
Namuunga mkono jamaa kwani wanawake wanadanganya sana na kupinduana mno. Mwanamke amvumilie tu jamaa ipo siku tutakutana nitamuonya ajirekebishe na kumpa uhuru mkewe.
Mkuu hata mimi naunga mkono hoja lakini mwanamke atavumilia mpaka lini? Maisha ya sasa hivi ni kusaidiana hasa usawa huu ulivyokaza. Cha msingi ampe hata uhuru wa kufanya biashara wasaidiane katika majukumu mengine ya kifamilia.
 
Hiyo ni sifa mojawapo ya mwanaume mwenye michepuko.
Hilo nalo neno maana siku zote mawazo ya mtu anaechepuka anamuwazia mwenzake kuwa anachepuka kama anavyofanya yeye, Hivyo ndo maana anambana sana mkewe akijua atachepuka kama anavyochepuka yeye.
 
Namuunga mkono huyo mume wa huyo dada.
 
Namuunga mkono huyo mume wa huyo dada.
Afu ishu sio kumbana mtu kihivyo. Kuchepuka ni hulka tu ya mtu unaweza ukambana mwisho wa siku ukawa unamlea mtoto wa mwanaume mwenzako. Cha msingi ni kumpa mtu uhuru wake mambo hayo ya kumbana mtu yamepitwa na wakati mkuu.
 
Asilimia nyingi ya uchepukaji huletwa na uhuru.
 
Amevumilia miaka mitano astahmili tu kwan tayar ameshaweza kuzoea hali, angejaribu kuongea na mumewe kwa upole na saut yenye kumaaniaha ndan yake kama mume anashikilia msimamo wake bas yeye awe naakili ya kudunduliza vipesa mana kuna leo na kesho na maisha n kusaidiana
 
Back
Top Bottom