Ushauri: Binti wa kiarabu ananipenda lakini mama yake hanitaki

Babumawe

JF-Expert Member
Sep 12, 2014
2,556
2,559
Habari,

Katika harakati na pilika za mjini hapa nilikutana na binti mmoja mwenye asili ya kiarabu inakaribia mwaka mpaka sasa tangu tufahamiane.

Kwakweli tulikuwa na urafiki wa karibu sana kwa kipindi cha muda mfupi tuliweza kuzoeana sana na kila mtu aliufurahia urafiki wetu. Ikafika kipindi nikawa naenda hadi kwao, yeye anaishi maeneo ya upanga ndiko wazazi wake wanapoishi, mara ya kwanza haikuwa rahisi aliponambia niende kwao kwani nilikuwa na hofu ya hali ya juu na ukizingatia asili yao kidogo ngumu kuchanganyika na watu wengine lakini nilivyofikiri haikuwa ivyo walinipokea vizuri na alinitambulisha kama rafiki tu kama marafiki wake wengine.

Baada kama ya miezi mitatu ya urafiki wetu basi zikaja hisia zingine kabisa kwani tuliweza kuwa wapenzi japo sikuwahi kwenda tena kwao kwani yeye ndio alikuwa anakuja kwangu sasa kwa muda huo wote.

Hakika niseme tu huyu mtu alinipenda sana hadi watu wangu wa karibu wakawa wanashangaa sana.

Katika hali ya mshangao kuanzia wiki ilopita mama yake amenishupalia nisiwe karibu na mtoto wake kwani yeye hataki kuona tena ukaribu wetu na ikafika kipindi hadi na vitisho juu.

Nilipojaribu kumueleza huyu binti kwakweli alilia sana na kuahidi hakuna atakayezuia penzi letu na hatotokea kamwe, naombeni ushauri wenu maana nipo njia panda hapa wazazi wake wamekomalia hawataki kunisikia japokuwa mie nawaambia ni rafiki yake tu lakini ndo hivyo hawataki, na ukizingatia huyu binti mie nishaanza kufanya nae vitu vya msingi kama kushare biashara na vitu vingine..

Hii hapa ni moja ya chats anazonitumia mama yake.

IMG_20201209_104521.jpeg
 
Back
Top Bottom