Kafariki tu mogonjwa ya kawaida ya kibinadamuAmefariki na ugonjwa gani huyo mke wa huyo jamaa, asije kuwa anataka tu kurudi kwa huyo manzi ili afugwe....si unajuwa wanaume wa Dar walivyo? Watalia mpaka na kutokwa na makamasi ili aonewe tu huruma na kupokelewa atunzwe.
Atakuwa amemuuwa ili apate kuolewa na huyo mwanaume , kwanini hakuolewa na mwanaume mwingine miaka yoteHabari
Kuna mdada kaja kuomba ushauri nami nikaona sio mbaya nikawashirikisha na nyie.iko hivi huyu manzi alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na jamaa mmoja hivi sasa baadae huyo jamaa akamtosa yaani huyu manzi akapigwa chini na huyo mshikaji akachukua manzi mwingine na wakafunga na ndoa kabisa wameishi kama miaka mitatu ya ndoa na walifanikiwa kupata mtoto mmoja sasa kwa bahati mbaya miezi kama mitatu nyuma mke wake huyo jamaa amefariki.
Sasa huyo jamaa amerudi tena kwa huyu manzi na kumwambia warudie penzi lao kama zamani. Anaomba ushauri je akubali au, je hataumizwa tena?
Miaka yote mitatu huyo binti hakua na mambo mengine kiasi kwamba jamaa arudi kwake tena? Atumie akili yake binafsi maana hakuna atakaepita kwenye hio njia kumsaidia ni yeye binafsi ajitambue ni kipi anahitaji kwa sasa maana kama ni mapenzi alishayawekeza na yakamuangusha ni kipi kipya anachoenda kukigundua kwa huyo jamaa?