Ushauri: Abdul Nondo tekeleza hili jambo haraka sana

Ushauri: Abdul Nondo tekeleza hili jambo haraka sana

Gambamala

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2014
Posts
1,045
Reaction score
766
Bahati mbaya sina namba ya Abdul Nondo ningempigia na kumpa huu ujumbe.

Wenye mawasiliano nae tafadhali mfikishie ujumbe huu. Mwenye mawasiliano nae tafadhali mfikishie wazo hili.

Ukweli ni kwamba sioni usalama wako pia na uendelevu mzuri katika masomo yako, wewe kama kiongozi wa mtandao wa wanafunzi ilikuwa ni haki yako kutoa tamko kulingana na nafasi yako na tukio la mauaji ya mwanafunzi mwenzenu.

Wasiwasi wangu ni kwamba kuna watu wana chuki kubwa juu yako, hivyo nahisi unaweza kuuawa au kutekwa na ukapotea moja kwa moja, na kwa namna hali ilivyo, wakisha kuteka zitabaki siasa kuwa tulitahadharisha kuwa watekaji wanaweza kumteka tena, zinapigwa story matokeo yake utaanza kusahaulika kama Ben Saanane.

Kumbuka kwa sasa wauaji na watekekaji wana enjoy freedom kuliko wakati wowote ule tangu tupate uhuru.

Nakushauri kwa haraka sana fanya ifuatavyo;

Kwa kuwa wewe ni mwanafunzi na hauna kipato, kimbilia ubalozi wowote wa nchi za Magharibi ulioko hapa Tanzania (hasa Marekani). Waeleze juu ya wasiwasi wa maisha yako, waeleze namna iliivyokuwa wajibu wako kutoa tamko kama kiongozi wa wanafunzi, waeleze mateso uliyopitia ukiwa lock up, kisha omba wakuondoe nchini kwa ajili ya usalama wako, omba wakupe scholarship usomee hukohuko na utapata elimu nzuri sana utafurahi.

Mimi nina uhakika Jogoo wa dunia Marekani watakubali ombi lako. Mimi naamini kwa matukio ya mauwaji na utekeji lazima ombi lako litakubaliwa.

Tofauti na hapo sioni future yako honestly ndiyo maana umeona hata kule chuoni kwako tayari wameanza kubana, naona giza.
 
Utafanya mwenzio awe mkimbizi for the rest of his life na asije ishi maisha ya AMANI huko unapomshauri akimbilie (Huku kunaitwa kusaliti nchi)...huu ushauri haupo sawa kabsa.....
Kama kweli unamtakia mema jambo zuri hapa ni kumshauri kama kweli NAFSI YAKE INA MSUTA alifanya makosa kwa kutokujua au kwa kushauriwa vibaya na baadhi ya watu....ATOKE ADHARANI AKILI alifanya makosa na aombe msamaha kwa SERIKALI,this will help...
Nondo bado bwana mdogo sana he still have a long way to GO.....Me naamini kabsa hata kwa sasa anajuta kwa nini alifanya hivyo...Ndio maana tunasema hivi SIASA mchezo mchafu sana ukiingia kichwa kichwa LAZIMA ILE KWAKO.....hata hao kina WANAOWANYOOSHEA wenzao mikono ikatokea MWENYEZI MUNGU akatufunulia yaliyonyuma TUNAWEZA MUOMBA MAGUFULI MSAMAHA
 
Utafanya mwenzio awe mkimbizi for the rest of his life(Huku kunaitwa kusaliti nchi)...huu ushauri haupo sawa kabsa.....
Kama kweli unamtakia mema jambo zuri hapa ni kumshauri kama kweli NAFSI YAKE INA MSUTA alifanya makosa kwa kutokujua au kwa kushauriwa vibaya na baadhi ya watu....ATOKE ADHARANI AKILI alifanya makosa na aombe msamaha kwa SERIKALI,this will help...
Nondo bado bwana mdogo sana he still have a long way to GO.....
Na kama ni kweli alitekwa itakuwaje??.Anyways ni kwamba Dogo bado yuko at risk kwa sababu serikali imeshawaaminisha wananchi kuwa NONDO Alijiteka, sasa kitakachofuatia hapa ni kwa Nondo kutekwa moja kwa moja , Na sirikali itakuja na majibu mepesi kuwa NONDO KAJITEKA TENA kwa sababu huwa anakawaida ya kujiteka, Na mjadala kufungwa kabisa.
 
Na kama ni kweli alitekwa itakuwaje??.Anyways ni kwamba Dogo bado yuko at risk kwa sababu serikali imeshawaaminisha wananchi kuwa NONDO Alijiteka, sasa kitakachofuatia hapa ni kwa Nondo kutekwa moja kwa moja , Na sirikali itakuja na majibu mepesi kuwa NONDO KAJITEKA TENA, Na mjadala kufungwa kabisa.
Ndio maana tunashaur dogo ajishushe tu aombe msamaha hata kama NI KWELI SERIKALI NDIO INAHUSIKA KATIKA UTEKWAJI WAKE...He is young and still have a long way to GO......Mwenye nguvu mpishe TU
 
Utafanya mwenzio awe mkimbizi for the rest of his life na asije ishi maisha ya AMANI huko unapomshauri akimbilie (Huku kunaitwa kusaliti nchi)...huu ushauri haupo sawa kabsa.....
Kama kweli unamtakia mema jambo zuri hapa ni kumshauri kama kweli NAFSI YAKE INA MSUTA alifanya makosa kwa kutokujua au kwa kushauriwa vibaya na baadhi ya watu....ATOKE ADHARANI AKILI alifanya makosa na aombe msamaha kwa SERIKALI,this will help...
Nondo bado bwana mdogo sana he still have a long way to GO.....Me naamini kabsa hata kwa sasa anajuta kwa nini alifanya hivyo...
Sioni kosa LA Kijana Nondo kwa nafasi take ila naona uonevu kutoka kwa mwigulu siro na bashite kuambiwa wajiuzulu ndio wakaamua wamteke.nani asiyemjua tabia mwigulu?au bashite?
 
Angalia masharti ya dhamana aliyopewa. Yaliwekwa mahsusi kabisa wakijua hilo unalomshauri linaweza kutokea. Akikimbia, wasiojulikana watawageuzia kibao hao wadhamini. Ila wazo lako linawezekana na ni wazo zuri.

Mimi nadhani wabaya wake wamemalizana naye, wameshamnyamazisha na kumuadhibu, unless roho ya TL imuingie ila wazazi wake watamkatalia. Hii kesi ni ya kuwatunishia kifua tu ila sioni kama serikali ina mpango wa kumfunga zaidi. Nondo ndiyo anastahili kuwafungulia kesi hao polisi na mabosi wao ila mwanasheria wake hatoshi kwa kesi nzito kama hiyo. Inahitaji mtu bold na ambitious.

Abdul Nondo hatatolewa kabla ya 4/4, afungue kesi ya kutekwa
 
Back
Top Bottom