Ushauri: Abaki na mwanaume yupi kati ya hawa?

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
651
Reaction score
589
Wanajamvi,
Heri ya mwaka mpya!
Kitambo sana sijaingia huku kutokana na pilika za hapa na pale. Twende kwenye hoja.

Nitajaribu kufupisha maelezo kama nitaweza ili nisiwachoshe.
Kuna binti mmi ni rafiki yangu hapa nilipopanga, huyu binti amehamia hapa mwishoni mwa December.

Alihamia hapa peke yake na alikuja na rafiki zake wawili. Kumbe wale rafiki zake wana maisha yao na pale walifanya kumhamishia tu.

Mimi kazi zangu nafanyia karibu na mazingira ya nyumbani,nhivyo ilikuwa rahisi sana kuzoeana nae ukizingatia alikuwa mgeni eneo lile. Baada ya kuzoeana jana katika story na katika kumdodosa maisha yake(maana ni mrembo hasa) ndo akaanza kunieleza;

Kwanza akaniambia pale amepangishiwa na mkaka mmoja mume wa mtu. kwa maelezo yake huyo kaka aliwahi kuishi kwake kama mfanyakazi katika moja ya biashara zake. Baadae akaacha kazi pale na kuanza kufanyabiashara zake.

Kwa vile hakugombana na huyo mwajiri wake wa awali, walikuwa na mawasiliano ya kawaida. Mawasiliano hayo ndo yalipelekea kutongozana.

Wakati anamtongoza yeye tayari alikuwa na uhusiano na kijana mwingine ambae alimuahidi kumuoa. Hivyo akamwambia huyo boss wake hataweza kujigawa kuwa na wapenzi wawili.

Jamaa hakuridhika akaendelea kubembeleza. Mungu alivyo wa ajabu, jamaa akiwa anamfuatilia yeye akaingia kwenye maumivu ya mapenzi baada ya kumfumania mpenzi wake katika chumba kilekile ambacho yeye pia hupelekwa! Baada ya kufumania alizimia na kuzinduka akiwa hospitali.

Baada ya tukio lile, mfariji mkubwa akawa boss wake wa zamani,na kwa vile alikuwa anamjua akajikuta wanaingia kwenye uhusiano. Baada tu ya kuanza uhusiano, jamaa akamhamisha kutoka katika chumba alichokuwa anakaa na kumpeleka nje ya mazingira ya nyumbani kwa jamaa.

Alikuwa kwenye nyumba ya giza akapelekwa nyumba ya umeme na maji ndani.

Jamaa akamnunulia kila kitu cha ndani.
Tatizo linalomkabili, pamoja na kwamba anapata kila kitu kwa huyu jamaa, lakini anahisi hampendi! Kabla hajaingia kwenye uhusiano na huyo aliyemfumania, aliwahi kuishi na kijana mwingine ambae moyo wake hasa ndo upo kwake.

Huyo kijana hana kipato kikubwa lakini ana wivu hatari na haoni shida kukupiga akihisi unachepuka. Sababu kubwa iliyomuondoa mara ya kwanza ni kipigo kutoka kwa huyo jamaa. Lakini anahisi huyo ndo mtu anampenda sana na anashindwa kuendelea kubaki kwenye mali lkn hana furaha.

My take:
Mimi nilimshauri abaki hapa na mshikaji mwenye uwezo wa kumhudumia. Haya mambo ya kujifanya unampenda mtu unaweza kwenda kujitesa bure! bora abaki na anayempenda na anampa kila kitu.
 
Neno NINGEJUA huja baada ya bahati kupotea,
Mwache ajichanganye sentensi iliyopo hapo juu ITAMHUSU soon.
 
Kwanza mume wa mtu ni sumu. Kuibiwa mume inauma bana.

Huyo binti kakuomba ushauri huku tayari akiwa na jibu lake moyoni hapo hata umshauri vipi mwisho wa siku atakushangaza pale atakapo rudi kwa bondia wake
 
Ngungwangungwa hii story me imenijeruhi ni km naijua...!! Hili tukio lipo wapi..!!?? Samahan lkn..
 
Mkuu magode,hapa ni jijini dar. Mwanzo binti alikuwa anaishi tabata bima na jamaa ndo anaishi hapo. Huku alikoletwa ni kinyerezi na me naishi hapa kinyerezi. Km unataka maelezo zaidi njoo pm.
 
Sawa mkuu nimekusoma..
 
Mwambie aache kuharibu ndoa ya mwenzie (hata kama mwanaume hajielewi kajisahau ana ndoa)
 
Mtu humpendi unapokeaje vitu kutoka kwake?

Ndo hapo tamaa huwa zinatuponza wadada mwisho wake tunaliwa vibaya tunabaki kulia lia.
 
Nyambizi akikuingia ndo utajua unacho kitafuta acha kutufanya watoto wadogo we ndo unamtaka huyo binti
 
Mtu humpendi unapokeaje vitu kutoka kwake?

Ndo hapo tamaa huwa zinatuponza wadada mwisho wake tunaliwa vibaya tunabaki kulia lia.
Muache atanuliwe hizo raba zake za huko chini....zikilegea sana akili itamrudi
 
Wanajamvi,
Heri ya mwaka mpya!
Kitambo sana sijaingia huku kutokana na pilika za hapa na pale. Twende kwenye hoja.

Nitajaribu kufupisha maelezo kama nitaweza ili nisiwachoshe.
Kuna binti mmi ni rafiki yangu hapa nilipopanga, huyu binti amehamia hapa mwishoni mwa December.

Alihamia hapa peke yake na alikuja na rafiki zake wawili. Kumbe wale rafiki zake wana maisha yao na pale walifanya kumhamishia tu.

Mimi kazi zangu nafanyia karibu na mazingira ya nyumbani,nhivyo ilikuwa rahisi sana kuzoeana nae ukizingatia alikuwa mgeni eneo lile. Baada ya kuzoeana jana katika story na katika kumdodosa maisha yake(maana ni mrembo hasa) ndo akaanza kunieleza;

Kwanza akaniambia pale amepangishiwa na mkaka mmoja mume wa mtu. kwa maelezo yake huyo kaka aliwahi kuishi kwake kama mfanyakazi katika moja ya biashara zake. Baadae akaacha kazi pale na kuanza kufanyabiashara zake.

Kwa vile hakugombana na huyo mwajiri wake wa awali, walikuwa na mawasiliano ya kawaida. Mawasiliano hayo ndo yalipelekea kutongozana.

Wakati anamtongoza yeye tayari alikuwa na uhusiano na kijana mwingine ambae alimuahidi kumuoa. Hivyo akamwambia huyo boss wake hataweza kujigawa kuwa na wapenzi wawili.

Jamaa hakuridhika akaendelea kubembeleza. Mungu alivyo wa ajabu, jamaa akiwa anamfuatilia yeye akaingia kwenye maumivu ya mapenzi baada ya kumfumania mpenzi wake katika chumba kilekile ambacho yeye pia hupelekwa! Baada ya kufumania alizimia na kuzinduka akiwa hospitali.

Baada ya tukio lile, mfariji mkubwa akawa boss wake wa zamani,na kwa vile alikuwa anamjua akajikuta wanaingia kwenye uhusiano. Baada tu ya kuanza uhusiano, jamaa akamhamisha kutoka katika chumba alichokuwa anakaa na kumpeleka nje ya mazingira ya nyumbani kwa jamaa.

Alikuwa kwenye nyumba ya giza akapelekwa nyumba ya umeme na maji ndani.

Jamaa akamnunulia kila kitu cha ndani.
Tatizo linalomkabili, pamoja na kwamba anapata kila kitu kwa huyu jamaa, lakini anahisi hampendi! Kabla hajaingia kwenye uhusiano na huyo aliyemfumania, aliwahi kuishi na kijana mwingine ambae moyo wake hasa ndo upo kwake.

Huyo kijana hana kipato kikubwa lakini ana wivu hatari na haoni shida kukupiga akihisi unachepuka. Sababu kubwa iliyomuondoa mara ya kwanza ni kipigo kutoka kwa huyo jamaa. Lakini anahisi huyo ndo mtu anampenda sana na anashindwa kuendelea kubaki kwenye mali lkn hana furaha.

My take:
Mimi nilimshauri abaki hapa na mshikaji mwenye uwezo wa kumhudumia. Haya mambo ya kujifanya unampenda mtu unaweza kwenda kujitesa bure! bora abaki na anayempenda na anampa kila kitu.
Anayempa kila kitu ni mume wa mtu au nimesoma vibaya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom