Ushamba wa PhDs na hatma ya Tanzania

Ushamba wa PhDs na hatma ya Tanzania

Elimu ni jambo njema sana. Linamfanya mtu kufungua ubongo wake kwa mapana.
Hata hivyo elimu tu haitoshi linapokuja suala la uongozi. Katika qualities za uongozi bora elimu ya madegree na maPhDs sio sifa namba moja.
Ni kama magadi tu lakini sio chumvi kwenye mboga tunayoita hapa kwa jina la 'uongozi'.
Uongozi unataka mtu mwenye busara, uvumilivu, subira, maono, hekima, msimamo thabiti na heshima kwa wale anaowaongoza. Vitu hivi si lazima uvipate darasani.
Daktari lazima asomee udaktari ili afanye kazi ya udaktari. Vivyo hivyo kwa mwalimu, mhasibu, lawyer, mhandisi nk.
Vilevile katibu mkuu wa wizara lazima awe graduate. Sawa. Hata hivyo kusoma pekee na kujaza mavyeti hakumfanyi mtu kuwa waziri mzuri. Si lazima sana waziri kuwa na elimu ya juu sana kuwa waziri mzuri kwani yeye ni mwanasiasa tu na hategemewi kuingia 'jikoni'
Elimu pia haimfanyi mtu kuwa mbunge mzuri. Mara nyingine hekima na busara tu zinatosha katika uongozi wa siasa.
Hivi sasa umeingia 'ushamba' wa kudhani kuwa viongozi wenye PhD ndio hamira ya maendeleo nchini.
Historia ya karibuni inatuonesha kuwa kuna viongozi walifanya vizuri katika nafasi zao bila degree. Akiwa wizara ya mambo ya ndani, Mrema alifanya kazi nzuri na hakuna aliyevunja rekodi yake mpaka sasa. Hakuwa na shahada wala kishada. Mzee Mwinyi aliongoza nchi kwa busara na hekima kubwa bila kuwa na 'degree wala nini.
Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.
Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters?!
Tujiulize wabunge au mawaziri wenye degrees wamefanya nini cha maana. Wame add value gani? Au wamezikimbia tu taaluma zao kifuata maslahi bungeni?
Mamlaka ziwe makini zinapompima mtu based on elimu pekee. Waende beyond vyeti. Kwa mfano haikuwa busara kuwatoa madereva wazoefu kazini eti kwa vile tu hawakuwa na chetu cha form 4.
Sioni mantiki ya kumwamini zaidi dereva mpya kwa vile tu amemaliza kipato cha nne ukamwacha mzoefu wa miaka 20!
Hii homa homa ya shahada na PhDs inahitaji vidonge. Shahada haikufanyi kuwa nesi mzuri zaidi kama huna wito na kazi hiyo.
Wala uprofesa haukufanyi kuwa waziri bora zaidi kuliko akina Mzee Kawawa kama sio mzalendo. Vyeti havifanyi kazi. Get out of the bottle!!!
Makubaliano na wewe na kumekuwabna jitihada nyingi kwa wanasiasa wengi kutafuta PhD kwa nguvu hata kwa najua za pants ilautendaji wao unawaumbua, Mfano mtu anaitea dr kinyeaji lakini kiutendaji ni chini ya std vii, anaogopa hata majukwaa ya kimataifa
 
Kuna msomi nguli wa sheria anaitwa Prof Paramagamba Kabudi, alichokifanya kwenye ishu ya makinikia wote tuliona na kusikia, kuna Dr Mwakyembe tunamsikia kwenye medani za siasa, kuna Dr Bashir Ali ndo amaeanza kushika kasi kwa sasa katika medani za siasa!

mleta mada ushanielewa kama napinga au nakubali hoja yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Prof Paramagamba Kabudi. Mhhh!
🙄🙄🙄🙄😀
 
Hoja ni kwamba shahada pekee sio mwarobaini wa kuleta maendeleo. Tumeona watu wengi wenye hizo degrees uwezo wao ni mdogo sana. Wanajua wenyewe walivyopata hivyo vyeti kwani haviakisi performance yao on ground. Kuna haja kubwa ya ku overhaul the whole education system kuondoa wasomi feki. Ndiyo kuna vilaza wengi wenye vyeti halali achilia mbali walioghushi!!
 
wabunge wasiwe na elimu wakajadili nn mule ndani sasa. au ndo yes kwenye kila kitu...yaaaana mie naona wabunge wote wawe kuanzia na diploma kwenda mbelee...aya mambo ya kujua kusoma na kuandikaa naona ni ujinga mtupuuu
Elimu ni jambo njema sana. Linamfanya mtu kufungua ubongo wake kwa mapana.
Hata hivyo elimu tu haitoshi linapokuja suala la uongozi. Katika qualities za uongozi bora elimu ya madegree na maPhDs sio sifa namba moja.
Ni kama magadi tu lakini sio chumvi kwenye mboga tunayoita hapa kwa jina la 'uongozi'.
Uongozi unataka mtu mwenye busara, uvumilivu, subira, maono, hekima, msimamo thabiti na heshima kwa wale anaowaongoza. Vitu hivi si lazima uvipate darasani.
Daktari lazima asomee udaktari ili afanye kazi ya udaktari. Vivyo hivyo kwa mwalimu, mhasibu, lawyer, mhandisi nk.
Vilevile katibu mkuu wa wizara lazima awe graduate. Sawa. Hata hivyo kusoma pekee na kujaza mavyeti hakumfanyi mtu kuwa waziri mzuri. Si lazima sana waziri kuwa na elimu ya juu sana kuwa waziri mzuri kwani yeye ni mwanasiasa tu na hategemewi kuingia 'jikoni'
Elimu pia haimfanyi mtu kuwa mbunge mzuri. Mara nyingine hekima na busara tu zinatosha katika uongozi wa siasa.
Hivi sasa umeingia 'ushamba' wa kudhani kuwa viongozi wenye PhD ndio hamira ya maendeleo nchini.
Historia ya karibuni inatuonesha kuwa kuna viongozi walifanya vizuri katika nafasi zao bila degree. Akiwa wizara ya mambo ya ndani, Mrema alifanya kazi nzuri na hakuna aliyevunja rekodi yake mpaka sasa. Hakuwa na shahada wala kishada. Mzee Mwinyi aliongoza nchi kwa busara na hekima kubwa bila kuwa na 'degree wala nini.
Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.
Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters?!
Tujiulize wabunge au mawaziri wenye degrees wamefanya nini cha maana. Wame add value gani? Au wamezikimbia tu taaluma zao kifuata maslahi bungeni?
Mamlaka ziwe makini zinapompima mtu based on elimu pekee. Waende beyond vyeti. Kwa mfano haikuwa busara kuwatoa madereva wazoefu kazini eti kwa vile tu hawakuwa na chetu cha form 4.
Sioni mantiki ya kumwamini zaidi dereva mpya kwa vile tu amemaliza kipato cha nne ukamwacha mzoefu wa miaka 20!
Hii homa homa ya shahada na PhDs inahitaji vidonge. Shahada haikufanyi kuwa nesi mzuri zaidi kama huna wito na kazi hiyo.
Wala uprofesa haukufanyi kuwa waziri bora zaidi kuliko akina Mzee Kawawa kama sio mzalendo. Vyeti havifanyi kazi. Get out of the bottle!!!
Mkuu, hili nalo ni jambo la kutizama sana. Kuna Phd zinazotokana na direct entry qualification nikiwa na maana Form six- Bachelor- Msc- Phd bila experience ya kutosha katikati. Hizi ni nyingi. Utazigundua, ukifika ofisini kwake ukiwa na shida ndogo tu ya kuhitaji maelezo tuu, utaona laptop zaidi ya mbili zinawashwa. Hapo mko kimya mnasubiri ziwake. Zikiwaka, utasikia,nipe maelezo yako tena. At the end of the day,unakuwa confused kuliko ulipokuja.
La pili, wengi wa aina hiyo wakipata madaraka, asst wake akawa ni Msc na experienced, atapata tabu sanaa. Wengine hutafuta certificate level awe msaidizi wake.
 
Back
Top Bottom