Ushamba wa PhDs na hatma ya Tanzania

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,091
1,202
Elimu ni jambo njema sana. Linamfanya mtu kufungua ubongo wake kwa mapana.
Hata hivyo elimu tu haitoshi linapokuja suala la uongozi. Katika qualities za uongozi bora elimu ya madegree na maPhDs sio sifa namba moja.
Ni kama magadi tu lakini sio chumvi kwenye mboga tunayoita hapa kwa jina la 'uongozi'.
Uongozi unataka mtu mwenye busara, uvumilivu, subira, maono, hekima, msimamo thabiti na heshima kwa wale anaowaongoza. Vitu hivi si lazima uvipate darasani.
Daktari lazima asomee udaktari ili afanye kazi ya udaktari. Vivyo hivyo kwa mwalimu, mhasibu, lawyer, mhandisi nk.
Vilevile katibu mkuu wa wizara lazima awe graduate. Sawa. Hata hivyo kusoma pekee na kujaza mavyeti hakumfanyi mtu kuwa waziri mzuri. Si lazima sana waziri kuwa na elimu ya juu sana kuwa waziri mzuri kwani yeye ni mwanasiasa tu na hategemewi kuingia 'jikoni'
Elimu pia haimfanyi mtu kuwa mbunge mzuri. Mara nyingine hekima na busara tu zinatosha katika uongozi wa siasa.
Hivi sasa umeingia 'ushamba' wa kudhani kuwa viongozi wenye PhD ndio hamira ya maendeleo nchini.
Historia ya karibuni inatuonesha kuwa kuna viongozi walifanya vizuri katika nafasi zao bila degree. Akiwa wizara ya mambo ya ndani, Mrema alifanya kazi nzuri na hakuna aliyevunja rekodi yake mpaka sasa. Hakuwa na shahada wala kishada. Mzee Mwinyi aliongoza nchi kwa busara na hekima kubwa bila kuwa na 'degree wala nini.
Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.
Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters?!
Tujiulize wabunge au mawaziri wenye degrees wamefanya nini cha maana. Wame add value gani? Au wamezikimbia tu taaluma zao kifuata maslahi bungeni?
Mamlaka ziwe makini zinapompima mtu based on elimu pekee. Waende beyond vyeti. Kwa mfano haikuwa busara kuwatoa madereva wazoefu kazini eti kwa vile tu hawakuwa na chetu cha form 4.
Sioni mantiki ya kumwamini zaidi dereva mpya kwa vile tu amemaliza kipato cha nne ukamwacha mzoefu wa miaka 20!
Hii homa homa ya shahada na PhDs inahitaji vidonge. Shahada haikufanyi kuwa nesi mzuri zaidi kama huna wito na kazi hiyo.
Wala uprofesa haukufanyi kuwa waziri bora zaidi kuliko akina Mzee Kawawa kama sio mzalendo. Vyeti havifanyi kazi. Get out of the bottle!!!
 
Kuna msomi nguli wa sheria anaitwa Prof Paramagamba Kabudi, alichokifanya kwenye ishu ya makinikia wote tuliona na kusikia, kuna Dr Mwakyembe tunamsikia kwenye medani za siasa, kuna Dr Bashir Ali ndo amaeanza kushika kasi kwa sasa katika medani za siasa!

mleta mada ushanielewa kama napinga au nakubali hoja yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta gamba mkuu upate kitengo..acha ubishi...watu wanabadirika kulingana na falsafa ya mtawala.....wenye Phds ndo awamu yao hii...acha wafaidi....labda atakuja mwingine mwenye maono kama yako..hapo sasa hao unaowaongelea watapata vitengo pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingekuwa vizuri kama ungedadavua zaidi kwa kuonesha watu wenye taaluma za uongoz (yaan Wenye PSPA, HR na Utawala nk) ktk level ya degree, masters na pHDs jinsi wanavyoshindwa kuongoza na ukiwalinganisha na watu ambao hawana taaluma zozote. Ikumbukwe si kila Degree, masters, pHDs na Prof inahusiana uongozi mana inaweza ikawa ya madini,misitu, majengo, biashara nk. Ingekuwa vzur kam unge focus ktk specific Profession abt uongoz kuliko kuwa too general

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi mtoa mada hana elimu ya juu, kiasi fulani ana "Inferiority complex" japo anachokisema kwa kiasi kidogo sana 6% hutokea kwenye jamii lakini sio rule of thumb, kinachofanyika kwa sasa ni BORA SANA kwa dunia ya leo kimaendeleo, kipi bora kuchuja hao wasomi(cream) ili kupata wanaofaa au kuchuja mchanganyiko ili kupata wanaofaa ? ? Tambua kusoma sio lele mama hata kidogo hizo sifa ulizozitaja sehemu kubwa ya wasomi 85%++ wanazo.
 
Elimu ni jambo njema sana. Linamfanya mtu kufungua ubongo wake kwa mapana.
Hata hivyo elimu tu haitoshi linapokuja suala la uongozi. Katika qualities za uongozi bora elimu ya madegree na maPhDs sio sifa namba moja.
Ni kama magadi tu lakini sio chumvi kwenye mboga tunayoita hapa kwa jina la 'uongozi'.
Uongozi unataka mtu mwenye busara, uvumilivu, subira, maono, hekima, msimamo thabiti na heshima kwa wale anaowaongoza. Vitu hivi si lazima uvipate darasani.
Daktari lazima asomee udaktari ili afanye kazi ya udaktari. Vivyo hivyo kwa mwalimu, mhasibu, lawyer, mhandisi nk.
Vilevile katibu mkuu wa wizara lazima awe graduate. Sawa. Hata hivyo kusoma pekee na kujaza mavyeti hakumfanyi mtu kuwa waziri mzuri. Si lazima sana waziri kuwa na elimu ya juu sana kuwa waziri mzuri kwani yeye ni mwanasiasa tu na hategemewi kuingia 'jikoni'
Elimu pia haimfanyi mtu kuwa mbunge mzuri. Mara nyingine hekima na busara tu zinatosha katika uongozi wa siasa.
Hivi sasa umeingia 'ushamba' wa kudhani kuwa viongozi wenye PhD ndio hamira ya maendeleo nchini.
Historia ya karibuni inatuonesha kuwa kuna viongozi walifanya vizuri katika nafasi zao bila degree. Akiwa wizara ya mambo ya ndani, Mrema alifanya kazi nzuri na hakuna aliyevunja rekodi yake mpaka sasa. Hakuwa na shahada wala kishada. Mzee Mwinyi aliongoza nchi kwa busara na hekima kubwa bila kuwa na 'degree wala nini.
Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.
Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters?!
Tujiulize wabunge au mawaziri wenye degrees wamefanya nini cha maana. Wame add value gani? Au wamezikimbia tu taaluma zao kifuata maslahi bungeni?
Mamlaka ziwe makini zinapompima mtu based on elimu pekee. Waende beyond vyeti. Kwa mfano haikuwa busara kuwatoa madereva wazoefu kazini eti kwa vile tu hawakuwa na chetu cha form 4.
Sioni mantiki ya kumwamini zaidi dereva mpya kwa vile tu amemaliza kipato cha nne ukamwacha mzoefu wa miaka 20!
Hii homa homa ya shahada na PhDs inahitaji vidonge. Shahada haikufanyi kuwa nesi mzuri zaidi kama huna wito na kazi hiyo.
Wala uprofesa haukufanyi kuwa waziri bora zaidi kuliko akina Mzee Kawawa kama sio mzalendo. Vyeti havifanyi kazi. Get out of the bottle!!!
wabunge wasiwe na elimu wakajadili nn mule ndani sasa. au ndo yes kwenye kila kitu...yaaaana mie naona wabunge wote wawe kuanzia na diploma kwenda mbelee...aya mambo ya kujua kusoma na kuandikaa naona ni ujinga mtupuuu
 
Back
Top Bottom