Ushamba wa mapenzi. Keep personal things personal

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
KEEP YOUR PERSONAL THINGS PERSONAL

Ndugu zangu, marafiki zangu, dada zangu , kaka zangu, wadogo zangu
kuna vitu vya kuandika kwenye social media na kutangaza kwa rafiki zako au ndugu zako na ambavyo si vya kuandika wala kusema ambavyo baadae huwa vinatuumbua wenyewe, mfano

1. Umegombana na mwenzi wako kutwa nzima ni mafumbo na kumuongelea mabaya kesho mkipatana unapost sijui together 4ever sijui nn wakati ulichokiandika kwa watu hakijafutika

2. Mwanaume umempata mwanamke. Kakupa uroda\penzi. Alafu baada ya muda unaenda kutangaza nimemgonga jane. Mara mchafu. Huo ni ushamba sana. Unaweza jiona kidume ila ni umboyoyo wa mapenzi. Umepewa uroda kausha umetosheka kausha kiume sio umbea. Imekua desturii nisha gonga yule. Ushamba.

3 . Mwanaume unasema na kujitangaza nimepiga demu fulani wakati hata paja hujawahi kuliona ni ushamba au ujinga uliozidi mipaka. Mwanaume kamili hajisifu huo ujinga tena ni uongo. Kuwa mwanaume wa kweli.

4. Unakuta mwanamke yupo ndani ya ndoa anafichua siri na ujinga wa mumewe. Fikiria hao unaowaambia wanamtizamaje mumeo na wanakuonaje wewe ulioolewa na mjinga. Huo ni upuuzi. Umeona kasoro zirekebishe. Hata mwanaume akiwa na tabia hizi hana tofauti nawa kike mwanaume kamili husimamia ndoa yake.

5. Mmeshawishiana mkapiga picha za ovyoo. Na kujirekodi video mmegombana unazitoa. Ni ushamba na kujidhalilisha kupita maelezo. Sasa video zenu wana download na kuzitizama bure kwenye mitandao. Una google tu "bongo x video" unawatizama. Watanzania wanafanya yao. Nakwambia video au picha ikiwa kwenye mitandao kutoa haitoki tenaaaa.

Zingine ni zipi ambazo nimesahau ambazo watu hupost bila kujua madhara yake ya baadae?
 
Kwa hiki kizazi cha nyoka ni wachache sana watakao kuelewa kwa jinsia zote nashindwa kuelewa tumeelimika na kustaarabika kuliko mababu na mabibi zetu ila tunafanya mambo ya kipuuzi karne mbili kabla ya mababu zetu.
 
Nakuelewa kaka sana,imekua tabu sasa ,watu wanadai ndoa watu wawili ila siku hizi ndoa ni ya jamii nzima.aibu nyingi,kabla hujaona pungufu la mwenzio jilaumu kwanini umeolewa au kuoa tatizo na wasiokua na shida walikuepo
 
Kwa hiki kizazi cha nyoka ni wachache sana watakao kuelewa kwa jinsia zote nashindwa kuelewa tumeelimika na kustaarabika kuliko mababu na mabibi zetu ila tunafanya mambo ya kipuuzi karne mbili kabla ya mababu zetu.
Sio wote wamestarabika sema wanajua kutumia teknolojia tuuu. Ila zero.
 
KEEP YOUR PERSONAL THINGS PERSONAL

4. Unakuta mwanamke yupo ndani ya ndoa anafichua siri na ujinga wa mumewe. Fikiria hao unaowaambia wanamtizamaje mumeo na wanakuonaje wewe ulioolewa na mjinga. Huo ni upuuzi. Umeona kasoro zirekebishe. Hata mwanaume akiwa na tabia hizi hana tofauti nawa kike mwanaume kamili husimamia ndoa yake.

Zingine ni zipi ambazo nimesahau ambazo watu hupost bila kujua madhara yake ya baadae?
Hii ni funga kazi.
 
Mwanamke unakuta yuko saluni au huko kwenye vikao na mashoga zake anaanza kujishebedua eti ooh Mme wangu kiboko kwenye mambo yetu Yale ,hajui kuna watu wanalilia hao wanaume anakuja kushtuka shoga ake wa karibu kashambeba mmewe juu juu anaanza kutoa macho oooh nimeibiwa Mme wangu....ushamba
 
mtu amezaa mtoto sijui wa kwanza alafu kila siku ni kumtangaza mtoto wangu kafanya hivi kafanya vile, au kututangazia demu wako au man wako anakupenda na kukuwaza au kukujali saaana wakati penzi lenu bado ni changa, utafikiri wengine hawajawahi kupendwa (alafu wakasalitiwa anyway), huu ni upuuzi kwa kweli
 
Kimekua kilio kaniibia.
 
Ulimbukeni.
 
Back
Top Bottom