Ushahidi wa Udikiteta ndani ya CHADEMA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushahidi wa Udikiteta ndani ya CHADEMA.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Sep 21, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Demokrasia ya kweli ni lazima ianzie katika vyama vya kisiasa. CHADEMA ni chama pekee katika vyama vikubwa TZ kilichoonyesha uchanga mkubwa wa Demokrasia hususan katika chaguzi za nafasi za juu ndani ya chama hicho.

  Mtihani wa kwanza mkubwa ulikipata chama pale Mh Zitto Kabwe alipojitokeza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho. Wahasisi wa chama hicho walifahamu fika kwamba Mh Mbowe asingeweza kumshinda kijana matata na mashuhuri huyo. Ni wazi kuwa ukilinganisha elimu zao ni sawa na mlima Kilimanjaro (Zitto) na kichuguu (Mbowe) sikwambii mambo mengine. Hapo kura ya VETO ikatumika, wajiitao wahasisi au wazee wa chama wakamlazimisha Kabwe ajitoe,-Udikiteta ukatumika.. Wakafanikiwa.

  Safari hii CHADEMA wameingia katika mtihani mkubwa zaidi, Kijana huyu ametangaza dhamira yake ya kugombea Urais. Safari hii anataka kumpangua Katibu wake- Mh Slaa ambaye naye anahitaji kugombea Uraisi kwa mara ya pili. Nilikuwa Arusha wiki mbili zilizopita na kuzungumza na wakuu wa ngazi za juu CDM (majina ninayo). Wamesema, huyu kijana ana ndoto za mwendawazimu, ni heri chama kife kuliko Kabwe kupewa nafasi hiyo ya kugombea urais. Hapa najiuliza, hivi watafanya nini? Lakini kama waliweza kumshinyikiza ajitoe kugombea Uenyekiti, nafikiri ni mbinu hizo hizo zitatumika Kumtupilia mbali. Huu ni UDIKITETA MKUBWA KABISA.

  Kuna kila sababu ya kumuelewa Mh Sitta alipomwita Mh Slaa "Dikiteta", kwani kinachotakiwa ni uchaguzi wa vidole na sio nguvu za KI-Idd Amini Amini Dada. Na ni katika mazingira haya CHADEMA Ipo katika TEST kubwa sana. Mh Zitto Kabwe kadhamiria, na ametangaza mara nyingi tu Dhamira yake hiyo.

  Safari hii ni lazima Vidole vitumike, ama sivyo Tendwa atalazimika kukifuta Chama hicho kwa kukiuka kanuni za vyama vya siasa. Kwa jinsi ninavyowafahamu akina Mtei, watatumia udikiteta na kumtupa nje kabla hajaingia hatua ya vidole. Je, huu sio udikiteta uliokithiri? Na watu kama hawa wakichukua nchi mnategemea nini?
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mods futeni huu uchafu.Tumechoka na upumbavu wa maneno haya kila siku.
   
 3. M

  Magesi JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mods mfungien maisha huyu kanjanja wa siasa
   
 4. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Acha Jazba, jibu hoja. Hivi hapa ni nini kisicho cha ukweli. Kuhusu Kabwe kugombea nafasi ya uenyekiti au kuhusu dhamira yake ya kugombea urais.

  Kwa nini mna maamuzi ya haraka haraka ya kushauri kufuta thread? Kweli siwaelewi. Kama Kabwe hakujitoa katika kugombea uenyekit baada ya kukutana na wazee wa chama, nieleze hilo. Tuanze hapo.
   
 5. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sio kosa lako!

  JITAHIDI KUTUMIA UBONGO KUFIKIRI NA KUPAMBANUA MAMBO, MAKALIO YAACHIE KAZI YAKE.
   
 6. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wewe na sheikh ponda lazima ni ndugu!
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Inachosha!
   
 8. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Zitto akitaka kupata fursa ya kugombea urais kupitia CHADEMA labda abadili ukanda na kuwa Ukaskazini, bila ya hivyo atasugua benchi na ubunge bila kupandishwa daraja kamwe.

  Hawa watu ni wabaguzi na wanakubalika vijijini kwao tu, taifa haliwezi kuunga mkono huu UKANDA HATA KIDOGO.
   
 9. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  haya maneno kama akiyasoma alieleta huu uzi basi hapana shaka atayaacha makalio yake yafanye kazi yake
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  haya zawadi tumekusikia,,,, usiku mwema & have sweet dreams........
   
 11. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoto mchokozi akipigwa utasikia, mamaaaaaa
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma.
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  zawadi ni kwanini unatumia muda na nguvu nyingi kushughulika na mambo chadema kuliko muda unaoutumia kuijenga ccm?
   
 14. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ukishindwa hoja, ndoto yako kubwa ni kummaliza mpinzani wako kwa maguvu. Hizi ndizo zilikuwa mbinu za Akina Idd Amini Dadaa.

  Ushauri wa bure: Unajisikiaje kama ungekuwa Balozi mzuri wa kueneza maneno ya ki-Demokrasia kuliko kuendeleza lugha ya kidikiteta. Fikiria sana hili litakusaidia mbele ya safari.
   
 15. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nape amekulipa shiling ngap mama hulali sa hizi unatunga huu uharo hapa?
   
 16. n

  nakuru Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini mnatumia muda mwingi kumjadili Zito? mafanikio Chadema iliyofikia ni kwa ajili ya uongozi wa Mh. Mbowe na Dr. Slaa, mwili wa zito uko chadema na roho yake iko ccm.........zito na shibuda ni kitu kimoja.
   
 17. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ni kweli natumia muda wangu mwingi kwa vyama vya Upinzani, si CHADEMA pekee. Kwa sababu vyama vya upinzani tunavihitaji sana kwa maendeleo ya Tanzania. CCM haiwezi kujikosoa yenyewe ni lazima ikosolewe na vyama vya upinzani, vinginevyo italala na kutupeleka shimoni.

  Ili vyama vya upinzani viikosoe CCM, ni lazima vyenyewe viwe visafi na viwe na dira. Kwa bahati mbaya mpaka sasa hivi vyama vya upinzani hatuna, na tatizo kubwa ni Udikiteta uliopo ndani ya vyama hivyo na kutoruhusu vijana chipukizi kuleta mawazo mapya ndani ya vyama hivyo.

  Nafikiri nimekujibu kifupi, kwanini natumia (sio kupoteza, kwa vile nafanya hivi kwa faida ya vizazi vijavyo.) muda WANGU MWINGI KWA VYAMA VYA UPINZANI IKIWEMO CHADEMA.
   
 18. Du Bois ideas

  Du Bois ideas JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sitoki kanda ya Kaskazini lakini sikubaliani na zitto kugombea sasa urais CDm, namuona bado saana. Panahitajika mtu mwenye kufanya maamuzi mazitto. kabwe bado asubiri. Namuona bado anapwaya katika nafasi ya Urais. Ubunge sawa na vyeo vingine lakini hapo ukweli lazima uwekwe wazi. Zitto subiri upikwe kwanza.
   
 19. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mawazo yako yana muelekeo wa kutokubali mabadiliko. Na hili ndilo tatizo lenu kubwa. Viongozi wa vyama tofauti ni muhimu kukaa pamoja na kujadili mustakabali wa nchi yetu, huu si usaliti.

  Pili, Pale mwenzako anapofanya vizuri hata kama ni mpinzani au chama tawala, ni muhimu umuunge mkono. Unajua, logic ni rahisi sana- ikiwa Daraja la Kigamboni litajengwa wote tutafaidika nalo, kwa nini tusiunge mkono jambo kama hilo? Amkeni.
   
 20. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hayo maneno yenye RED,haueleweki kabisa, ni kama sijui umetumia lugha gani. Come again, huu uzi ni wa kusadikika, unakosa ngvu ya kushawishi mtu achangie chochote.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...