MAGEUZI KWELI
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,947
- 253
Hili nalo kilaza kweli....Hapa ni kama kusoma biblia msikitini au Qran Kanisani wakati hayakuhusu.....Kalakabaho mchanga wewe
Kama umri wa Zitto utakuwa bado basi wa Dr Slaa utakuwa umepitiliza manake sasa hivi ameanza kupukutika mpaka nywele.
kwa taarifa nilizo nazo ni kuwa zitto ana mchumba tayari na sikusikia jina la zawadi ngoda,ila kwa kuwa zitto ni mwislam endelea na jitihada unaweza kuja kuwa first lady wa kufikirika.
safari tuliyo nayo na aina ya gari tulilonalo dereva kwa wakati huu hatakiwi kuwa machachari,tunataka dereva mwenye kuijua njia ya kitonga kona zote mbaya na hila za wahalifu ccm katika hizo kona mbaya,tukifika njia tambarare ndio tutafikiria kumpa dereva machachari ili aonyeshe mbwembwe za kupiga gia na kupiga change down.
. Je, huu sio udikiteta uliokithiri? Na watu kama hawa wakichukua nchi mnategemea nini?
Demokrasia ya kweli ni lazima ianzie katika vyama vya kisiasa. CHADEMA ni chama pekee katika vyama vikubwa TZ kilichoonyesha uchanga mkubwa wa Demokrasia hususan katika chaguzi za nafasi za juu ndani ya chama hicho.
Mtihani wa kwanza mkubwa ulikipata chama pale Mh Zitto Kabwe alipojitokeza kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho. Wahasisi wa chama hicho walifahamu fika kwamba Mh Mbowe asingeweza kumshinda kijana matata na mashuhuri huyo. Ni wazi kuwa ukilinganisha elimu zao ni sawa na mlima Kilimanjaro (Zitto) na kichuguu (Mbowe) sikwambii mambo mengine. Hapo kura ya VETO ikatumika, wajiitao wahasisi au wazee wa chama wakamlazimisha Kabwe ajitoe,-Udikiteta ukatumika.. Wakafanikiwa.
Safari hii CHADEMA wameingia katika mtihani mkubwa zaidi, Kijana huyu ametangaza dhamira yake ya kugombea Urais. Safari hii anataka kumpangua Katibu wake- Mh Slaa ambaye naye anahitaji kugombea Uraisi kwa mara ya pili. Nilikuwa Arusha wiki mbili zilizopita na kuzungumza na wakuu wa ngazi za juu CDM (majina ninayo). Wamesema, huyu kijana ana ndoto za mwendawazimu, ni heri chama kife kuliko Kabwe kupewa nafasi hiyo ya kugombea urais. Hapa najiuliza, hivi watafanya nini? Lakini kama waliweza kumshinyikiza ajitoe kugombea Uenyekiti, nafikiri ni mbinu hizo hizo zitatumika Kumtupilia mbali. Huu ni UDIKITETA MKUBWA KABISA.
Kuna kila sababu ya kumuelewa Mh Sitta alipomwita Mh Slaa "Dikiteta", kwani kinachotakiwa ni uchaguzi wa vidole na sio nguvu za KI-Idd Amini Amini Dada. Na ni katika mazingira haya CHADEMA Ipo katika TEST kubwa sana. Mh Zitto Kabwe kadhamiria, na ametangaza mara nyingi tu Dhamira yake hiyo.
Safari hii ni lazima Vidole vitumike, ama sivyo Tendwa atalazimika kukifuta Chama hicho kwa kukiuka kanuni za vyama vya siasa. Kwa jinsi ninavyowafahamu akina Mtei, watatumia udikiteta na kumtupa nje kabla hajaingia hatua ya vidole. Je, huu sio udikiteta uliokithiri? Na watu kama hawa wakichukua nchi mnategemea nini?
Ni haki yako kuandika hivyo ila ungetuonesha namna ulivyo critical analyst kama ungeanzia kuonesha democrasia ya chama tawala CCM. ungeanza kueleza namna walivyomfanya Samweli Sita alipochukua form kugombea tena uspika na baadae kuja na hoja isiyokuwepo ya kutaka spika awe mwanamke. Tuone uchaguzi mkuu ujao kama watakuja na hoja hiyo. Umeyanyamazia pia pale Kikwete alipopinduliwa na kuwekwa Mkapa kwa hoja nyepesi kwamba umri mdogo ilhali wakati anagombea na kupigiwa kura Halmashauri kuu wakijua umri wake. Unazungumzia udikteta lakini unasahau namna alivyoletewa zengwe Salim Ahmedi Salim na kuambiwa siraia wakati amekuwa balozi kwa miaka mingi tu. hayo ni machache tu ambazo ni rafu na udikteta uliokithiri ambao huuoni. inawezekana nawewe unagamba INABIDI UBANDULIWE.