Mchange
Senior Member
- Jul 21, 2009
- 158
- 326
Wakuu.
mtakumbuka kuwa mwaka 2013 mwishoni, bila huruma, bila kujiuliza mara mbilimbili, mitandaoni kote, vijana kwa wazee walisimama kidete kumshambulia aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chadema kipindi hicho ndugu Zitto Kabwe kuwa amehongwa mabilioni na wanaCCM kukihujumu chama chake.
jana kukazuka mjadala kama huo ulioanzia mitandaoni humu humu kumuhusu mwanasiasa kijana mwengine January Makamba safari hii huyu akihusishwa na dada yake kutumia vibaya madaraka na kujinufaisha mpaka kufikia kiasi cha kudaiwa kumdhulumu aliyeitwa muitaliano Vincenzo Nizzolino.
leo Raia huyo wa Italia Vincenzo Cozzolino aliyesababisha mtafaruku mkubwa jana baada ya kuvujisha mazungumzo yake kwenye mitandao ya kijamii na mpenzi wake wa zamani Mwamvita Makamba amejitokeza hadharani na kuomba radhi kwa kuihusisha familia ya Makamba na ufisadi.
Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo mchana, Vincenzo amesema alifadhaika kutokana na familia ya Makamba kushindwa kumsikiliza baada ya ugomvi wao na kuongeza kuwa hakuwahi kutoa kiasi chochote cha pesa kwa January wala hakuwahi kumuomba amsaidie katika biashara zake. Pia amesikitishwa na kitendo cha Mange Kimambi kuingiza masuala ya siasa katika mtafaruku wake na Mwamvita. Kwa Habari zaidi, soma taarifa yake aliyoituma kwa Neville Meena, Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima hapo chini;.
ushauri.
kabla hatujahukumu, ni vema tukajiridhisha kwanza kuhusiana na tuhuma mbalimbali, hata kama tunawachukia namna gani watu waliotajwa.
wasalaam.