Ushahidi mtumishi wa TRA waiva

Ushahidi mtumishi wa TRA waiva

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema itaanza kusikiliza ushahidi wa Jamhuri dhidi ya kesi inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Jennifer anayekabiliwa na tuhuma za kumiliki magari 19 na kuishi maisha ya juu kuliko kipato chake kama mtumishi yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 530.8.

Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri uliomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa kuwa mashahidi hawajapatikana kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Wakili wa Serikali Vitalis Peter alidai kuwa kutokana na mashahidi kuwa na majukumu mengine ya serikali wameshindwa kuwapata kwenda kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa huyo.

Hakimu alisema mahakama yake itaanza kusikiliza ushahidi wa Jamhuri Aprili 9.

Katika kesi ya msingi, Peter alidai kati ya Machi 21, 2016 na Juni 30 mwaka huo mahali tofauti jijini Dar es Salaam, akiwa mtumishi wa TRA, mshtakiwa huyo alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Alitaja mali hizo kuwa ni magari 19 ya Toyota Rav4, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry, Toyota Ipsum, Toyota Wish, Toyota Mark II, Toyota Regius, Toyota Estima, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Passo na Suzuki Carry, yote yakiwa na thamani ya Sh. milioni 197.6.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kati ya Machi 21, 2012 na Machi 30, 2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiri wa TRA aliishi maisha ya hali ya juu tofauti na kipato chake, yenye thamani ya Sh. 333,255,556.24.

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana.

Chanzo:
IPP
 
Bora hata sijawa Hakimu au Jaji kwani kwa jinsi ninavyojijua nilivyo na kwa Urembo wa huyo Dada hiyo Kesi ningeshaifutilia mbali zamani sana na pengine hata huyo Dada sasa angekuwa Mke wangu wa Saba ( 7 ) na Mimba tayari nikiwa nimeshampachika tena ya Mapacha Watano.
 
Dada kaumbika vizuri mno, ila sidhani kama watu wamekuelewa uliposema mimba, strategy nzuri sana ya kukwepa jela..
 
Haya mambo mengine ni ulimbukeni tu, unanunuaje magari 19 yakutembelea, si bora ukanunue viwanja huko, Sema yawezekana waliokuwa wanampa dili kawanyima papuchi sasa wanamshughulikia
 
Tanzania kuna vituko eti mtu anashitakiwa kwa kumiliki Magari kumi na tisa tena Toyota tupu na kuishi maisha ya juu tofauti na mshahara wake. Yule ni mwanamke kuishi maisha ya juu huenda ana tumia part time yake vizuri au kwao zipo kwanini asiishi vizuri. Na hayo magari angalau ingekuwemo Range, V8, Land cruiser, Hammer, Posh na ndinga nyingine kali. Swali Mshahara wanapanga wao na matumizi apange nani?
 
Kaajiriwa TRA, mishahara yao ni ina range 2m-3m kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi ya kula, nguo, pango, fuel, luku, maji, misc wabakiwa labda na 1m, hapo kama huna watoto, kama unao, wabakiwa na ndogo zaidi, sasa ndio kujiuliza magari 19 na hiyo nyumba aliyojenga amewezaje?! tena anaonekana kijana tu, sidhani kama ana zaidi ya 10 yrs TRA, jibu ni wizi, uwe ulaya, marekani au asia, dola huwa zinachunguza vipato vya watu..
 
Kwahiyo kwa mshahara huo alitakiwa amiliki vitu kiasi gani na aishi maisha ya gharama gani? na je? angeamua kuweka mali zake katika majina tofauti ingekuwaje. Kama aliuza mali yake au mali ya urithi hiyo ni nje na kazi yake itakuaje? je? kama alivuta mkopo napo itakuwaje. Angalia thamani ya magari yote haya fiki hata bei ya Ndinga za maana.
 
Kaajiriwa TRA, mishahara yao ni ina range 2m-3m kwa mwezi, ukitoa matumizi ya mwezi ya kula, nguo, pango, fuel, luku, maji, misc wabakiwa labda na 1m, hapo kama huna watoto, kama unao, wabakiwa na ndogo zaidi, sasa ndio kujiuliza magari 19 na hiyo nyumba aliyojenga amewezaje?! tena anaonekana kijana tu, sidhani kama ana zaidi ya 10 yrs TRA, jibu ni wizi, uwe ulaya, marekani au asia, dola huwa zinachunguza vipato vya watu..
Hakuna mfanyakazi TRA nanaanza analipwa 2M. Hiyo mishahara ni level za meneja wa wilaya au principal tax officers.

Gross ya TRA ni laki 8. Transport & Housing allowance ni 160,000.

Ukiona mtumishi wa TRA anaishi maisha nje ya huo mshahara ujue ni wizi au rushwa.

Watu mna imaginations za ajabu sana kuhusu mishahara ya TRA.

Rudia kusoma mashitaka ya awali ya huyo dada, walitaja na mshahara wake hadi kufikia june 2016 ambao hauzidi 1.2M na ana miaka 7 sasa kazini.

TRA nje ya rushwa ni maisha ni ya kawaida sana.
 
hata kama ana papuch inayomwingizia 4m kwa mwezi?
 
Lazima aonyeshe ushahidi mahakamani kua papuchi ndio ilikua inamuingizia hicho kipato, kiwe ni kipato halali ambacho kinalipa kodi.

Kama kipato sio halali atapatikana na kosa la kutakatisha pesa chafu na kuziingiza kwenye uchumi, atakua na kosa la kukwepa kodi na mwisho atakua na kosa la kuhujumu uchumi.

Huyo binti hana pa kutokea.
 
Back
Top Bottom