Ushahidi: Maelekezo kutoka juu Haumtoi mtu Hatiani

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
Awamu ya tano na masalia yake ndani ya awamu hii yalituvesha hii "bloody" tungo - Maelekezo kutoka juu.

Pamoja na kuwa hadi hapa tulipo kuna ya kujifunza kutokea kwa nduli Sabaya, habari ndiyo hiyo. Haupo utetezi hapo!

Wangalipo kina Sabaya wengi huru mitaani. Ni vizuri kwa mustakabala mwema wa haki ukaandaliwa utaratibu huru wa kuwatia adabu wote hao kwa uhalifu wao.

Awamu ya tano watu wengi wameuwawa, wameteswa, wametekwa, wamepotezwa, wamebambikiwa kesi, wamedhulumiwa nk na wahalifu husika kabisa, wapo huru mitaani wanakula maisha.

Hii haikubaliki na hatua stahiki zisipofuatwa hili tayari ni "a ticking time bomb!"

My take:

Waliotajwa kwenye kadhia hii yenye you uliopitiliza - Dr. Mpango na Prof. Kuoga ilikuwa busara wakajiuzuru.
 
Muhimu wahakikishe hayo maelekezo toka juu yanafuata sheria, yatambulike kisheria, ila kama hayatatambulika kisheria, basi muhimu mtoaji maelekezo aishi milele ili amlinde mbwa wake, lakini kama mtoaji maelekezo hataweza kuishi milele au atleast mpaka pale mpokeaji atakapotangulia kuondoka kwenye uso wa dunia, basi ni vyema mpokeaji maelezo akagoma kuyatekeleza kwa usalama wake mbeleni.
 
Sabaya alikuwa na haki ya kulia hadharani, alikuwa kafiwa kuliko wafiwa 😁😁.
 
Gambo namsifu sana. Sijui kitu gani kilitaka kumfanyia awe kama kina Bashite na Sabaya. Yani kuna wakati alishaanzaga kufuata maelekezo kutoka juu na kuonea watu. Lakini alishtuka akapunguza kasi alitakaga sana kumfurahisha nduli Jiwe kwa kuonea watu. Jamaa ni mjanja sana.
 
Gambo dume. Ikizingatiwa analalamika yeye kama mbunge ananyanyaswa vipi na RC au mteuliwa yeyote 😁😁?
 
Muhimu wahakikishe hayo maelekezo toka juu yanafuata sheria, yatambulike kisheria, ila kama hayatatambulika kisheria, basi muhimu mtoaji maelekezo aishi milele ili amlinde mbwa wake, lakini kama mtoaji maelekezo hataweza kuishi milele au atleast mpaka pale mpokeaji atakapotangulia kuondoka kwenye uso wa dunia, basi ni vyema mpokeaji maelezo akagoma kuyatekeleza kwa usalama wake mbeleni.
Nani alimtuma kufanya haya??View attachment 1976689View attachment 1976691
 
Habari wanajamii wenzangu, nmekuwa nikifuatilia majibu ya Ole Sabaya kwenye ushahidi wake kwamba alikuwa akipata maagizo kutoka juu ili atimize majukumu yake kifupi alikuwa alikuwa anatii mamlaka. Lakini hii imekaaje mpaka sasa Makamu wa rais, Waziri wa fedha na gavana wa BOT kutajwa kuwa walikuwa wanahusika kutoa maagizo kwa ole sabaya kutimiza yale ambayop leo yamemtia kitanzini . Tujikumbushe, Wakati Mh Lowasa anatajwa kwenye sakata la Richmond alijiuzulu kulinda heshima. Je kuna nini kwa hawa viongozi waliotajwa kwenye ushahidi wa kesi ya sabaya
 
Ndani ya hicho chama hakuna mwenye unafuu! Sabaya ametolewa tu kafara. Lakini tukiamua kwa dhati kabisa kama Taifa kumtafuta mchawi, basi hakuna atakayepona.
 
Kujiuzulu kwako kutawaaingza kwenye ktanz/hatia ya moja kwa moja kuw ni kweli na sijui kama sheria wao inawalinda.
 
Habari wanajamii wenzangu, nmekuwa nikifuatilia majibu ya Ole Sabaya kwenye ushahidi wake kwamba alikuwa akipata maagizo kutoka juu ili atimize majukumu yake kifupi alikuwa alikuwa anatii mamlaka. Lakini hii imekaaje mpaka sasa Makamu wa rais, Waziri wa fedha na gavana wa BOT kutajwa kuwa walikuwa wanahusika kutoa maagizo kwa ole sabaya kutimiza yale ambayop leo yamemtia kitanzini . Tujikumbushe, Wakati Mh Lowasa anatajwa kwenye sakata la Richmond alijiuzulu kulinda heshima. Je kuna nini kwa hawa viongozi waliotajwa kwenye ushahidi wa kesi ya sabaya
Hiyo sahau mkuu
Usikute hata namba yake ya simu wameshafutaga.
 
Baada ya Burudani, tuendelee kupata Somo toka kwa baba Askofu

Dr Benson Bagonza

KWA NIABA...

Unaweza kula kwa niaba..
Unaweza kunywa kwa niaba..
Unaweza kupokea kwa niaba..
Unaweza kupongezwa kwa niaba
Unaweza hata kupigwa kwa niaba

LAKINI

Huwezi kuiba kwa niaba..
Huwezi kuiba, kupora, kutesa, kubaka, kutukana, au kuua kwa niaba.
Huwezi kufa kwa niaba
Huwezi kuugua kwa niaba
Huwezi kufungwa kwa niaba nk

MAANA YAKE

1. Kwenye mazuri kwa niaba ipo

2. Kwenye mabaya kwa niaba haipo

3. Utii wa mamlaka una ukomo

4. Kinga ni ya mteuzi si Mteuliwa

5. Inaruhusiwa kupokea maagizo na
kuyapotezea

6. Inaruhusiwa kujiuzuru bila
kusema kwa nini ukiona
unaagizwa kutenda kinyume na
sheria

7. Ukiagizwa kuiba, ukaiba, aliyeiba ni
wewe hata kama haimwondolei
hatia nyingine aliyekuagiza.

Hili ni somo la MAADILI YA MADARAKA (Ethics of Power). Hili ni tofauti na somo la MAADILI YA UONGOZI/UTAWALA (Leadership Ethics).

Kwenye MAADILI YA MADARAKA unafundishwa kutoiba. Kwenye MAADILI YA UONGOZI/UTAWALA unafundishwa usiibe lakini kama ukiiba usikate tamaa na usikamatwe. Kukamatwa ni kosa kubwa kuliko kuiba!
 
Nakazia:

.. Huwezi kuiba kwa niaba
.. Huwezi kupora, kutesa, kubaka, kutukana, au kuua kwa niaba.
.. Huwezi kufa kwa niaba
.. Huwezi kuugua kwa niaba
.. Huwezi kufungwa kwa niaba
.. Utii wa mamlaka una ukomo

.. Kinga ni ya mteuzi si Mteuliwa
.. Inaruhusiwa kupokea maagizo na
kuyapotezea

.. Inaruhusiwa kujiuzuru bila kusema kwa nini ukiona unaagizwa kutenda kinyume na sheria
.. Ukiagizwa kuiba, ukaiba, aliyeiba ni wewe hata kama haimwondolei hatia nyingine aliyekuagiza.

Abarikiwe sana baba askofu Dr. Benson Bagonza.
 
Back
Top Bottom