Useja si laana (Singleness isn't a curse)

Los santos

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
964
2,045
Andiko sio langu nimelikuta sehem na chini kbsa Kuna acknowledgement..

USEJA SI LAANA! (Singleness isn't a curse)

Ni kipindi cha uhuru wa kifikra unaokupa nafasi ya kujifunza mengi.

Singleness was meant to be enjoyable!

Ni kipindi kizuri cha kujitafuta na kujua kusudi la kuumbwa kwako na kuanza kuishi humo.

Daudi alimuua Goliathi na kuitwa Mwanajeshi shujaa, akawa na sifa kuliko mfalme akiwa seja, kijana mdogo tu.

Yakobo alimiliki Mifugo mingi na kumjua Mungu sana akiwa seja tu.

Yusufu alitawazwa kuwa Waziri mkuu akiwa Single.

Danieli, Meshack na Abednego hawakuwahi kuoa ugenini na walitawala nchi kama mawaziri.

Alafu ukimchunguza Yusufu na na hawa kina Danieli utagundua....walikuwa smart mno kichwani yet sexually pure. So wale wa propaganda za Sayansi inasema kama hufanyi sex akili haifanyi kazi vizuri naomba mnieleze kama mmewahi kufikiri na kuleta wazo likaiponya dunia nzima na njaa kama Yusufu.

Sexual purity is a foundation of all wisdom.

Did you know! Hata Mungu aliona SI VYEMA kwa Adamu kuwa peke yake baada ya kutunza vema bustani...

So Adamu alishajua kabisa "mimi Adamu niko hapa duniani kuanzisha, kutawala na kutunza (Establish/progene/Fathering, dominion and sustaining the creation ) ndio maana akaanzisha majina ya wanyama wote na ikawa hivyo, akatawala kila kitu na kuendeleza vizuri bustani bila tamaa ya vitu...thats why humkuti Adamu akimendea tunda alilozuiwa na Mungu!

Bro unataka kuoa?

Umeanzisha nini?

Unazalisha na kutunza nini?

Umeishinda tamaa ya macho, fedha na mwili?

Singleness is not a curse, it was meant to be enjoyable!

So, tunaposema '2045' haina maana tunapuuza suala hili muhimu...no si vyema lakini useja ni raha mno ukifanikiwa kujua kusudi la kuishi na ukafanikiwa kuanza kuishi.

Turudi kwa Adamu. Ukiangalia utaona ni miaka ilipita kabla Mungu hajajisemesha, si vyema mtu huyu awe peke yake, so ujue kuna muda ILIKUWA VYEMA.

Kuna muda alikuwa hajaweza kuji-master vema, hivyo hakufaa ku-master mtoto wa mama mkwe...sound right?

Dada zangu....

Hivi mnajua hakuna mwanamke kwa maandiko alikuwa 'desperate' halali, hali hanenepi, hafurahi kisa hajaolewa?

Of which is not wrong though!

Rebeka alikuwa 'pisi kali' na binti mwenye heshima na adabu sana, alikuwa ana-enjoy maisha na kuitumikia familia yake mpaka mme alimjia...

Pale kisimani Mtumishi wa Ibrahimu aliwaomba msaada mabinti wengi na ni mmoja tu aliyeonesha kufunzika vema na wazazi....Wema na adabu hata kwa mtu asiyemjua.

Ruthu je?

Alikuwa anaendelea kutenda mema mengi akimtunza mama mkwe...ijapokuwa alikuwa mjane aliolewa!

Nikukumbushe kuhusu Rahabu?

Ijapokuwa alikuwa malaya maarufu pale Yeriko bado Salmoni alimuoa kwa kusikka habari ya juhudi yake katika wema aliowatendea wapelelezi.

Nimuongelee Abigaili....hapana kasome Biblia yako!

Alafu ukiwaangalia hawa wote, wala hawakuwa na stress za kuolewa, walijaa furaha na wali-enjoy maisha huku watenda yanayopaswa kutendwa na mtu yeyote anayejitambua vema.

Hatumjui mme wa Mariam Magdalena na Martha lakini kazi zao zinajulikana vema...

Umegundua nini?

By dr. Min Kazabao Edson
+2557635755550
 
Nzuri ila hata Mungu mwenyewe aliona si vema na ndiyo maana akamletea Adam mke.

Laiti ingempendeza Mungu kwamba mzee Adam aishi peke yake asingempelekea bibi Hawa, so issue ya family bado ni muhimu kuliko useja!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom