Fbn
JF-Expert Member
- Jul 31, 2016
- 14,138
- 33,525
Je, Kwa Nini USDT (Tether) Inaonekana Kama Sarafu ya Kidijitali Inayoshikilia Thamani ya Pesa?.
Tuje kwenye Historia
Kabla ya kuibuka kwa USDT, watu waliokuwa wakitumia sarafu za kidijitali kama Bitcoin au Ethereum walikumbwa na changamoto kubwa ya mabadiliko makubwa ya bei (volatility). Hii iliifanya cryptocurrencies kutokuwa bora kwa malipo ya kila siku au kuhifadhi thamani.
Ilibidi kuwepo na njia mpya — sarafu ya kidijitali ambayo ina thamani thabiti na inaweza kutumika kama “daraja” kati ya dunia ya fedha ya kawaida (fiat money) na teknolojia ya blockchain.
jina la “Realcoin” mwaka 2014, ukianzishwa na Brock Pierce, Reeve Collins, na Craig Sellars. Lengo lao lilikuwa kujenga token ya blockchain iliyofungiwa kwa thamani ya dola moja ya Marekani ($1).
Mwaka huo huo, jina Realcoin lilibadilishwa kuwa Tether — jina ambalo linamaanisha “kufunga” au “kufunga thamani”.
Mnamo mwezi Novemba 2014, Tether ilizinduliwa rasmi kama stablecoin ya kwanza duniani
Tether (USDT) ilijengwa kwenye kanuni rahisi:
Kila token moja ya USDT inawakilisha dola moja ($1) inayohifadhiwa kwenye akaunti ya benki.
Hii inamaanisha kuwa kwa kila USDT inayozunguka katika soko, kampuni ya Tether inatakiwa kuwa na akiba halisi ya dola sawa na hiyo.
Tether ikawa ya kwanza kuleta dhana ya “fiat-backed stablecoin” – ambapo sarafu ya kidijitali inahakikishiwa kwa sarafu ya kawaida.
Tuje kwenye mada ambapo Katika zama hizi za maendeleo ya kiteknolojia, watu wengi wanaanza kusikia au kutumia maneno kama “USDT”, “crypto”, “blockchain” na “stablecoin”. Lakini wakati huohuo, wengi wetu tumeshazoea kutumia mifumo ya kifedha kama M-Pesa, Airtel Money au Tigo Pesa. Kwa hiyo swali linakuja Kwa nini sarafu kama USDT zinaonekana kuwa ndio “pesa halisi ya kidijitali” na siyo M-Pesa au sarafu zetu za kawaida?
Tofauti ya Kimsingi: Mifumo ya Kawaida (M-Pesa) vs Sarafu ya Kidijitali (USDT)
M-Pesa ni mfumo wa malipo, siyo sarafu huru ambayo M-Pesa ni njia ya kuweka na kuhamisha fedha kwa kutumia simu. Pesa unayoweka kwenye M-Pesa bado ni Tanzanian Shilling (TZS) au sarafu ya nchi nyingine. Hii ni pesa ya kawaida (fiat) inayodhibitiwa na benki kuu, serikali, na kampuni ya simu kama Vodacom.
Unapohifadhi pesa kwenye M-Pesa, unaiweka kwa jina lako kupitia kampuni ya simu. Unahitaji usajili wa laini, mtandao wa simu, na mara nyingi – kitambulisho.
USDT ni sarafu ya kidijitali ya kimataifa kwa kuwa USDT (Tether) ni aina ya stablecoin – yaani sarafu ya kidijitali ambayo thamani yake ni sawa na dola moja ya Kimarekani ($1). Hii inaifanya kuwa digital dollar kama nilivyoeleza hapo mwanzoni kuhusu historia yake.
USDT inafanya kazi kwenye mitandao ya blockchain kama Ethereum, Tron, nk. Unapomiliki USDT, unaishikilia moja kwa moja kwenye wallet ya kidijitali, bila kuhitaji akaunti ya benki au laini ya simu.
Thamani Yake Inayoshikika na Kubadilishika na hii imesababisha Watu wengi katika nchi zenye uchumi usio imara wanapendelea USDT kwa sababu Thamani yake haiporomoki kama sarafu za ndani pia Inaweza kutumika kimataifa, bila mipaka.
Inahifadhi thamani dhidi ya mfumuko wa bei au kushuka kwa thamani ya shilingi kwa Mfano, kama shilingi inapoteza thamani kila mwaka, USDT bado itakuwa na thamani ya karibu $1 kila wakati — jambo linalolinda uwezo wa kununua.
Udhibiti na Uhuru wa Mtumiaji
Kipengele mfano M-Pesa/Airtel/Tigo zina mamlaka
na Kampuni ya simu, serikali Lakini USDT (Tether) Hakuna mamlaka kuu.
Kwa USDT Hakuna mtu anaweza kufungia akaunti yako.
Unaweza kutuma pesa bila kupitia mtu wa kati (peer-to-peer).
Gharama ya kutuma fedha (hasa kwenye Tron) ni karibu sifuri.
Maisha Katika Dunia ya Kidijitali
Katika dunia ya leo Biashara zinakua mtandaoni (online businesses) na kupelekea njia nyingi za Malipo yanaenda kimataifa (freelancing, ecommerce, crypto jobs)
Kwa dunia ya sasa mifumo mingi imefikia kwenye matumizi ya Fedha zinazotumika ni crypto kama USDT, BTC, ETH
Watu wanaolipwa kutoka nchi za nje wanapendelea USDT kwa sababu Ni ya haraka, Ni salama, Haina ada kubwa kama benki.
USDT ni kama Njia ya Kuepuka Hatari za Kiuchumi Katika nchi kama Zimbabwe, Venezuela, Lebanon, hata baadhi ya mataifa Afrika Sarafu za ndani zimeporomoka kufanha Wananchi wengi wamekimbilia stablecoins kama USDT kulinda fedha zao.
Hii inaonyesha kuwa watu wanaanza kupendelea sarafu huru, ya kimataifa, na ya kidijitali ambayo haiathiriwi na siasa au benki za nchi zao.