If this is the case that Zanzibar is a burden to Tanganyika, in so called United Republic of TZ why do you not open the so called joint account for union incomes separate from money aqured by TZ mainland only ?
SURA YA SABA MASHARTI KUHUSU FEDHA ZA JAMHURI YA MUUNGANO SEHEMU YA KWANZA MCHANGO NA MGAWANYO WA MAPATO YA JAMHURI YA MUUNGANO Akaunti ya Fedha ya pamoja Sheria ya 1984 Na.15 ib.42 Tume ya pamoja ya Fedha Sheria ya 1984 Na.15 ib.42 133. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akauti maalum itakayoitwa "Akaunti ya Fedha ya Pamoja" na ambayo itakuwa ni sehehmu ya Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambamo kutawekwa fedha yote itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasi kitakachoamuliwa na Tume ya pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano. 134.-(1) Kutakuwa na Tume ya pamoja ya Fedha yenye wajumbe wasiozidi saba ambao watateuliwa na Rais kwa mujibu wa ibara hii na masharti ya sheria iliyotungw na Bunge. (2) Majukumu ya Tume yatakuwa ni: (a) kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu utekelezaji wa Mambo ya Muungano, na kutoa mapendekezo kwa Serikali mbili kuhusu mchango na mgawo wa kila mojawapo ya Serikali hizo; (b) kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha wa Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mambo ya kifedha kati ya Serikali mbili; (c) kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama Rais atakavyoagiza, na kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.