USD 1200 kwa kila Mzanzibari!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..utafiti uliofanywa na Prof.Teddy Malyamkono na wasomi wenzake umebaini kwamba Zanzibar ni mzigo mkubwa kwa wa-Tanganyika.

..ningeshauri kila Mtanganyika asome kitabu cha Prof.Maliyamkono.

..ikiwezekana kitabu hicho kitumike mashuleni, kwenye madrasa,sunday school, jando, unyago, etc etc

The Political Plight of Zanzibar said:
ZANZIBAR A DRAIN ON UNION ECONOMY

The astronomical rise of Zanzibar’s financial dependence on the mainland government is the latest wave of criticism levelled at the Tanzanian union by leading academics.

They quantify the dependence at nearly 835 million US dollars in
transfers between 1983-84 and 1998-99 in a new publication, entitled
‘The Political Plight of Zanzibar’, launched after a two-year study in
the island.

“This, as the book points out, is equivalent to the mainland giving
every Zanzibari a gift of 1,202 dollars a year, or roughly five years
of Tanzania’s per capita Gross National Product,
” Teddy Maliyamkono,
the publication’s editor, says.

“It is also equal to the average total annual revenue of Zanzibar’s
government during the past six years,” he adds.

Further questions are raised as to why the Zanzibari constitution
refuses the semi-autonomous state to contribute to the union budget
although the union bore the expenses of supporting its annual balance
of payments deficit.

“By refusing to pay and making it their constitutional right not to,
Zanzibar is implicitly denouncing the union. Now the question is, why
is the mainland Tanzania paying a fortune to keep the union unless they
have an immeasurable intrinsic love for the people of Zanzibar!”
Maliyamkono, a political scientist, says in the book.

“It is argued in some quarters that the political and economic costs
of letting Zanzibar go on its own, could, by far, outweigh present
transfers and benefits which accrue to Zanzibar from the union,” he
adds.

Maliyamkono notes that the mainland sends much money to Zanzibar,
and subsidises its power consumption.

Some of the transfers, like smuggling, tax evasion and the money
sent into the island by Zanzibaris working on the mainland, are
invisible and cannot be quantified.

“From the economic point of view, there is no denying that it is
Zanzibar that needs the union more than mainlanders do. The union is
Zanzibar’s livelihood, there is no Zanzibar without the union,
” he
points out.

The political marriage of Tanganyika and Zanzibar in 1964 has been
plagued by a plethora of operational problems.

Zanzibar, which is heavily dependent on cloves to sustain its
economy, has been complaining that the mainland is benefiting too much
from the union and that it should, in the spirit of its ’sovereignty,’
be allowed to have its own flag.

But according to the authors of the book, there is no denying that
it is Zanzibar that needs the union the most.

Maliyamkono warns that dissolution of the union would be
economically disastrous to Zanzibar.
 
..utafiti uliofanywa na Prof.Teddy Malyamkono na wasomi wenzake umebaini kwamba Zanzibar ni mzigo mkubwa kwa wa-Tanganyika.

..ningeshauri kila Mtanganyika asome kitabu cha Prof.Maliyamkono.

..ikiwezekana kitabu hicho kitumike mashuleni, kwenye madrasa,sunday school, jando, unyago, etc etc

Hiki kitabu km kitasomwa na wengi (najua hatuna utamaduni wa kupenda kujisomea vitabu mbalimbali) basi watanganyika macho yatawafunguka na hawatakuwa tayari tena na MUUNGANO.
Wenzio wazenji wanasema wanamafuta msiwababaishe, wamesahau dunia inavyokwenda. Ilishaabiriwa kwamba soon watu wataacha kutumia mafuta yanayochimbwa ardhini!! Hawa muungano ukivunjia la hasha wataishia kwenye mikono ya sultani wa Oman!
 
"But according to the authors of the book, there is no denying that
it is Zanzibar that needs the union the most.

Maliyamkono warns that dissolution of the union would be
economically disastrous to Zanzibar."

Huo ni upotoshaji wa hali ya juu. Anataka kutuaminisha kuwa Zanzibar haiwezi kusimama peke yake kama Taifa bila kuwa ndani ya Muungano? Du! I can not buy that idea. Hata kama mimi ni mtu wa bara I believe for sure that Maendeleo ya Zanzibar yamecheleweshwa kwa kuwa ndani ya Muungano. Kadri umaskini unavyoongezeka bara ndivyo unavyosambaa mpaka visiwani. Mbona visiwa vya sychelles na Mauritius vina mazingira kama ya Zanzibar havijaungana na nchi yoyote na bado vinapeta kuichumi? Tafiti zingine hufanywa kuwaridhisha wale waliowapa tenda ya kufanya hizo utafiti. Tusichukulie tafiti for granted lazima ziwe subjected to scrutine.
 
Visiwani ni mzigo mkubwa sana kwa Bara na hii inajulikana kwa siku nyingi!

Yet Visiwani hawaachi bado kulalamika na kulia lia kila siku!

Sasa komoro nao wanaomba kujiunga na bara..sasa sijui mizigo yote ya Zanzibar na Komoro- je bara wataweza?
 
andindile said:
Kadri umaskini unavyoongezeka bara ndivyo unavyosambaa mpaka visiwani. Mbona visiwa vya sychelles na Mauritius vina mazingira kama ya Zanzibar havijaungana na nchi yoyote na bado vinapeta kuichumi?

andindile,

..umedai Tanganyika ikiwa masikini basi hali hiyo husambaa mpaka Zanzibar.

..je Tanganyika ikiwa tajiri utajiri huo husambaa na Zanzibar pia?

..vipi Zanzibar ikiwa tajiri?? je utajiri huo husambaa mpaka Tanganyika?

..Zanzibar ikiwa maskini what happens to Tanganyika? je, tunabeba mzigo wa kuwahifadhi wakimbizi wa kiuchumi toka Zanzibar?

NB:

..kama Zanzibar inaweza kuwa kama Seychelles au Mauritius kwanini haijafanya hivyo mpaka sasa hivi?

..kwa misaada, ruzuku, na soko kubwa liloko Tanganyika, Zanzibar walipaswa kuwa wameendelea kuliko hao kina Seychelles na Mauritius.

..Seychelles wamejikwamua kiuchumi kwa kuimarisha utalii. sasa nini kinawashinda Wazanzibar kuimarisha sekta moja tu ya uchumi kama utalii?
 
Kwa mfumo wa Muungano tulionao ni vigumu sana kwa Zanzibar kusonga mbele. Si unakumbuka sakata la bandari pale Zanzibar ilipokuwa katika harakati ya kuifanya bandari ya Zanzibar kuwa bandari huru na mwisho wake ulikuwaje kiuchumi kwa Zanzibar.Viongozi wengi ni hand picked tokea bara hivyo hawana dira yoyote na mstakabari wa Zanzibar. Wameishia kutekeleza matakwa ya wale waliowaweka madarakani na kuendelea kutuaminisha kuwa Zanzibar bila bara haiwezi kusonga mbele kama wanavyotuaminisha kuwa Tanzania ni nchi maskini wakati tumekalia raslimali kibao. Wale ambao wanaonekana kuwa na dira na nchi ya Zanzibar wameishia kwenye misukosuko mfano hayati Karume, Jumbe, na Hamadi. wengine waliobaki wangi wao wanafanana na viongozi wenzao wa bara katika kuendesha nchi pasipo na mpangilio maalum.
 
..utafiti uliofanywa na Prof.Teddy Malyamkono na wasomi wenzake umebaini kwamba Zanzibar ni mzigo mkubwa kwa wa-Tanganyika.

..ningeshauri kila Mtanganyika asome kitabu cha Prof.Maliyamkono.

..ikiwezekana kitabu hicho kitumike mashuleni, kwenye madrasa,sunday school, jando, unyago, etc etc

Mkuu kinapatikana wapi kitabu hichi? i need it
 
andindile said:
Kwa mfumo wa Muungano tulionao ni vigumu sana kwa Zanzibar kusonga mbele. Si unakumbuka sakata la bandari pale Zanzibar ilipokuwa katika harakati ya kuifanya bandari ya Zanzibar kuwa bandari huru na mwisho wake ulikuwaje kiuchumi kwa Zanzibar.Viongozi wengi ni hand picked tokea bara hivyo hawana dira yoyote na mstakabari wa Zanzibar. Wameishia kutekeleza matakwa ya wale waliowaweka madarakani na kuendelea kutuaminisha kuwa Zanzibar bila bara haiwezi kusonga mbele kama wanavyotuaminisha kuwa Tanzania ni nchi maskini wakati tumekalia raslimali kibao. Wale ambao wanaonekana kuwa na dira na nchi ya Zanzibar wameishia kwenye misukosuko mfano hayati Karume, Jumbe, na Hamadi. wengine waliobaki wangi wao wanafanana na viongozi wenzao wa bara katika kuendesha nchi pasipo na mpangilio maalum.

andindile,

..Tanganyika ilipinga masuala ya bandari huru Zanzibar kwa kuogopa Zanzibar kuwa a Tax evasion haven. baadaye Zanzibar walipitisha uamuzi wa kuwa bandari huru na mpaka sasa hivi hatujaona mafanikio.

..vilevile ujenzi wa gati ya bandari ya Zanzibar ulikuwa uwarded kwa contractor asiye na uwezo, au sijui walishindwa kumsimamia, lakini kazi ilikuwa ya kiwango cha chini sana. sijui kama hilo nalo wanaweza kuwatupia lawama Tanganyika.

NB:

..MAFANIKIO YA BANDARI HURU YA ZANZIBAR NI YAPI?
 
Huo wasiwasi unakuja kwa sababu ya mfumo wa Muungano wangekuwa nje ya muungano wala kusingekuwa na mvutano. Sina hakika kama Zanzibar ni bandari huru kwa sasa. Ufisadi unaoendelea Zanzibar ni mwendelezo wa unaoendelea Bara. Ndio maana hata mawaziri Zanzibar utakuta wanatembelea mashangingi kama mawaziri wa bara. Hawaangalii manzingira yao na kipato cha zanzibar. Yote hayo ni upotofu uliopo katika uongozi mzima wa chama tawala
 
Nziku said:
Mkuu kinapatikana wapi kitabu hichi? i need it

Nziku,

..Title ya Kitabu ni: The Political Plight of Zanzibar.

..ni mchango wa wataalamu wa fani mbalimbali kama Uchumi na Sociology. kimekuwa na Prof.Teddy Maliyamkono.

..naamini kinaweza kuwepo UDSM.
 
andindile said:
Huo wasiwasi unakuja kwa sababu ya mfumo wa Muungano wangekuwa nje ya muungano wala kusingekuwa na mvutano. Sina hakika kama Zanzibar ni bandari huru kwa sasa. Ufisadi unaoendelea Zanzibar ni mwendelezo wa unaoendelea Bara. Ndio maana hata mawaziri Zanzibar utakuta wanatembelea mashangingi kama mawaziri wa bara. Hawaangalii manzingira yao na kipato cha zanzibar. Yote hayo ni upotofu uliopo katika uongozi mzima wa chama tawala.

andindile,

..si kweli kwamba ufisadi unaoendelea Zenj ni muendelezo wa ufisadi wa Tanganyika. labda utueleze ni Mtanganyika gani, au fisadi gani toka Bara, anayefanya ufisadi huko Zenj.

..ufisadi huku Tanganyika ulianza kuota mizizi wakati wa utawala wa Mzee Ruksa.

..tena vinara wa ufisadi wakati huo walikuwa ni Mawaziri wa kutoka Zenji kama Ahmed Hassan Diria na Juma Hamad Omari.

..hata Zanzibar wakiwa nje ya Muungano bado mivutano itakuwepo kwasababu ya ujirani na ukaribu wetu.

..Zanzibar ilianzisha bandari huru kwa kutegemea ku-offload bidhaa zake huku Tanganyika. sasa lazima wa-Tanganyika tuwe-concerned na hatima ya viwanda vyetu.
 
Watanganyika wanafanya ufisadi Zenj indirectly kwa kuwacontrol viongozi wa Zanzibar. Pia kumbuka CCM hawawezi kumwajibisha kiongozi zanzibar kwa kufanya ufisadi as long as anatetea Muungano

Naamini ni mwendelezo kwa sababu katika CCM hakuna kuwajibishana. CCM inatawala bara na visiwani. Hivyo mafisadi ndio wanaongoza nchi wala hawana wasiwasi kuwa watachukuliwa hatua.

Kwa kuwa concerned na hatima ya viwanda vyetu hapo ndipo tumewamaliza kabisa kiuchumi Zanzibar. Wangekuwa nje ya muungano tusingewafanya kitu maana yanakuwa ni maamuzi yaliyopo ndani ya uwezo wao.
 
andindile,

..zaidi ya mgombea Uraisi wa Zanzibar kwa ticket ya CCM hakuna kiongozi yeyote wa Zenj anayechaguliwa kwa mkono wa Tanganyika.

..muundo wa CCM ni kwamba huwezi kuwa mgombea wa Uraisi wa Zenj bila kupata kura za wajumbe wa Bara. pia huwezi kuwa mgombea wa Uraisi wa Tanzania/Tanganyika bila kushinda decisively kura wajumbe toka Zanzibar.

..wanaolalamikia utaratibu huo wa CCM ni wale walioshindwa kuusoma mfumo wa uchaguzi na kura ndani ya chama chao na kuutumia to their advantage.

..hata CUF wanaolalamika kwamba masuala ya Zenj yanaamuliwa Dodoma wamekuwa wakifanya mikutano ya mikuu ya chama Tanga na Dar-Es-Salaam.

..nimekueleza kwamba bandari huru ya Zenj nia yake ilikuwa ni kuifanya Tanganyika dampo la bidhaa toka Zenj. hilo linawezekana as long as Tanganyika inaendelea kuwa chini kiviwanda. sasa ulitegemea Tanganyika wataruhusu hali hiyo iendelee mpaka lini?

..lakini Zenj mwisho wake walipitisha sheria ya Zenj kuwa bandari huru. swala kujiuliza ni kwamba wako wapi sasa? nini mafanikio ya bandari huru?

..Zanzibar wangekuwa nje ya Muungano, na wakaamua kuanzisha bandari huru, basi Tanganyika wangeweza na hiari ya kuzuia chombo chochote kile cha majini kinacholeta bidhaa toka Zanzibar.
 
JokaKuu

Unakumbuka sakata la Bilah na Karume? nani aliongoza kura Zanzibar na nani alichaguliwa kwenye vikao vya bara? Hapo ndipo penye Tatizo.

Hayo ya bandari siwezi kusema sana maana maana sina uhakika kama bandari ya Zanzibar inaoperate kama bandari huru kwa sasa pamoja na kuwa sheria ilipitishwa.
 
Jokakuu:

Wakazi wa Manispaa ya Kinondoni pekee yake ni wengi kuliko wakazi wote wa Zanzibar.

Na kwa sasa hivi jiji la DSM ni zaidi ya mara tatu ya wakazi wa Zanzibar. Ukweli wa mambo unabaki kuwa kwa Tanzania bara inatakiwa iwe na uchumi imara kuhimili negative impact yoyote ya Zanzibar.

Na kwa maoni yangu sio Zanzibar pekee yake. Tulitakiwa kuwa na uchumi imara kuhimili shinikizo lolote la nchi za Burundi na Rwanda.
 
Sasa mnaidai Tanganyika au mnataka kuuvunja ,hebu semeni msikike sio mnasema hili na lile kama Zanzibar ni mzigo mzito jamani utuweni .
G55 wapo wapi au hicho kitabu Baba yenu wa Taifa alikificha ,yaani kukwiba mnakwiba na waindi watatu tu wanawapeleka puta ,sasa hasira eti Zanzibar wanapata gift ,huyo profesa uchwara ni kibaraka wa CCM tu maana kama asingekuwa kibaraka aeleze Zanzibar walichangia kiasi gani ilipoanzishwa BOT na hadi leo ni faida kiasi gani wamegawiwa au gawio lao anakula nani ? Ni juzi tu kuna wachunguzi wa mahesabu hebu katazameni wamesemaje kuhusiana na malipo ambayo Zanzibar inabidi walipwe ?
 
Ni kweli kwamba kiuchumi Wazanzibar wanafaidi Muungano kuliko Wabara. Kila bajeti ya serikali...lazima fungu kubwa litengwe kwa ajili ya kuendesha serikali ya Tanzania visiwani. Tunachofaidi sisi wabara in Usalama tu. Tunalipa hela nyingi sana kwa ajili ya kununua usalama na amani kwa Tanzania Bara hasa mikoa ya Pwani kwani pindi tukitengana tu....kuna kila dalili za Pemba na Unguja kutunishiana misuli......ndio hapo Mikoa yote ya pwani itajaa wakimbizi kutoka visiwani...........shauri yenu..ipo siku tutawaachia....
 
andindile,

..naielewa sana sakata ya Bilali na Karume.

..Dr.Bilali alishindwa kuuelewa utaratibu unaotumika kuchagua wagombea Uraisi[Zenj na Muungano] kwa tiketi ya CCM.

..Kikwete naye alishindwa kuuelewa utaratibu huo and it cost him the opportunity to run in 1995. Mkapa alimshinda Kikwete kwa kucheza deal ya dakika za mwisho na wajumbe wa Zanzibar kwa kumtumia Salmini Amour.

..Dr.Bilali alishindwa kutokana na uzembe wake mwenyewe. ni sawa na Hillary Clinton ambaye alidharau caucus states na matokeo yake akashindwa ku-close the gap btn her and Obama.

..kwa msingi wa matukio hayo sioni kwanini wa-Zenj walalamikie utaratibu huo wakati unaathiri pande zote za Muungano sawasawa.

..Dr.Salmini alishatangaza kwamba Zanzibar ni free port. sasa ndiyo nauliza tangu ametoa matamshi yale hali imebadilika vipi huko Zanzibar?

..binafsi nadhani tatizo la wa-Zenj ni kuwa wako too preoccupied na kujaribu kuwa Waarabu, au nchi ya Kiarabu.

..kuna opportunities nyingi sana wangeweza kuzitumia kwa manufaa ya pande zote za Muungano lakini kinachowasumbua wao ni kutaka kuwa kama Oman au Dubai.

..kwa mfano badala ya kujaribu kuwaiga Dubai na huu mradi wa free port kwanini Zanzibar haianzishi viwanda vya ku-process matunda toka Tanganyika na kuyauza kwa nchi nyingine?

..vilevile Tanganyika ina uhaba mkubwa sana wa sukari. kwanini Zanzibar haifanyi juhudi zozote kufufua kiwanda cha sukari mahonda na ku-export sukari kuja Tanganyika?

..ninavyoelewa mimi Mauritius ina a very advanced sugar industry. tena wawekezaji wa sukari Tanganyika baadhi yao wana-operate na Mauritius. sasa ungetemea wa-Zenj waige mfano wa Mauritius, lakini la hasha. wanataka wawe kama Dubai/Waarabu, siyo Mauritius.

..hivi mnataka kuniambia Free Port itainua hali ya wa-Zenj wengi zaidi kuliko investments kwenye viwanda?

Zakumi,

..Tanganyika ni kubwa sana kuliko Zenj.

..wa-Tanganyika wengi hawana hata habari kwamba kuna Muungano. ndiyo maana husikii wakipiga kelele uvunjwe.

..tatizo ni kwamba wa-Zenj wakitaka kuingiza bidhaa zao Tanganyika bila kulipa ushuru wanaleta kisingizio kwamba wao ni sehemu ya Muungano. baadaye wakitaka kuanzisha bandari huru wanadai wao ni taifa huru waachiwe waamue mambo yao bila kuingiliwa.

Nobo

..kukitokea vurugu Zanzibar siyo Tanganyika peke yake itakayobeba mzigo wa wakimbizi. wengine wanaweza kukimbilia Kenya.

..kama sijakosea Sultani alipopinduliwa alikimbilia Mombasa Kenya. Mzee Kenyatta alimkataa, ndipo akaja Dar-Es-Salaam.
 
Si wameolewa wazanzibari, ubaya gani tena kuwapa mahari kila Mwaka kila mzanzibari 1202$ ?

Nikiwa mke na hutaki niendelee, unlaumiani?
kwanza umeniowa kwa ndoa isio na talaka, kila miaka mitano untia mimba ya mtoto wako, kisha wamsingizia mwanharamu! hee mdanganyika, unzidi!

Niache basi na ndoa iso talaka, uone nafa au ntaishi!

Hivi hii posa ya muungano aliyeileta nani?
 
Back
Top Bottom