Usaliti

Usaliti

Kuna mambo nayafikiria hapa:-
1.Yawezekana ameona unampenda sana na hauwezi kufanya chochote
2.Labda amekuwa msaada mkubwa upande wa familia yako so unakosa hata nguvu ya kwenda kushitaki
3.Labda unahisi kuolewa umebahatika na ukiachana naye mambo yako hayataenda kwakuwa anakutimiza kila kitu so unachukulia poa machoni huku moyoni unaumia
4.Umejiolesha bila wazazi kujua maarufu "kama karibu tuishi"
Ushauri wangu:
  • Fanya maamuzi kwa mstakabali wa maisha yako ya baadaye,simaanishi umuache kwakuwa inaonyesha umempenda kamshitaki kwa wazee mkae myamalize
  • Achana naye maana hakuna maana ya kukuoa wakati ana wengine tena ankuambia live(hapo anamaanisha hakutaki ila unamng'angani) wenzake huwa wanajificha tena wanafanyia mbali kama anaishi bunju anaenda kufanyia Gongo la mboto sasa wewe iweje anakuambia live na bado umebweteka?
  • Fuata moyo wako unavyokuambia
 
Pole my dear dada! naomba nikuulize dada je wakati anakwambia hayo mlikuwa katika khali ya ugomvi au? Kuwa wazi dadaangu au ndani kunako 6x6 unanyima. Jaribu kuchunguza chanzo cha kukwambia hayo maneno. Hayo ni makavu live usiyapuuze hata kidogo.
 
Humiliation.
Kwani wewe hufanyi makosa?Wewe huna mapungufu ama madhaifu?Wewe ni malaika?

Kwahiyo ukifanya makosa ndo usiadhibiwe??! This is too much...huyo mshikaji hajafanya jambo jema kabisa.
 
Kanichanganya hapo, anakupenda lakini ana mwanamke mwingine??? sijui unaibebaje hiyo.!
 
Pole sana,hadi mimi imeniuma sana nahisi mzuka,lakini hapo dawa yake taratibu tafuta jibwana la maana halafu unaanza kuhamisha nguo moja moja atashangaa tu unakuja kumwalika Kwenye harusi yako hata ya bomani pouwah tu!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mwambie hata wewe una mwanaume wa nje ila unampenda sana.

Ndo maana dirisha dogo la usajili huwa halifungwi.....
 
Ndo walivo tu hawa viumbe ishi nae huku ukijua ndo alivo.,
anakupenda masaa 24 anakuambia anakupenda na bado mitongozo na kutoamba vipo tu nyambaf
 
Fanya yafuatayo:

1. Kapime VVU haraka sana.
2. Mchukue mumeo akapime na yeye VVU
3. Kama majibu ni Negative tumia CONDOMS
4. Baada ya miezi mitatu kapime tena wewe na yeye
5. Kama majibu ni Negative endelea kutumia condom na mumeo MAISHA YOTE as long as anaendelea mahusiano yake huko nje na kama hautaweza utakuwa kwenye hatari ya:- (i)Kupata magonjwa ya zinaa
(ii)Kuambukizwa VVU
au achana nae sio muaminifu.
6. Kama majibu ni Positive anza kutumia dawa za kurefusha maisha

Umeshauri kama mtu anayetoa nasaha juu ya gonjwa hili. Zaidi ya yote naona akifanya hivyo atakuwa amebariki ndoa ya nje. Kama dada ni mkristo ajue tayari kuwa mumewe ameamua kuwa mzinzi na muasherati. Biblia imesisitiza juu ya ndoa ya mke na mume mmoja kwa mkristo anaemfuata Yesu. Kama hilo limeshatokea anapaswa kulifikiria mara saba saba na kulichukulia umakini katika maamuzi.
 
Back
Top Bottom