Usaliti wa kiapo

Usaliti wa kiapo

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,190
Reaction score
34,526
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 1
+255 713 373731

TONY ni kijana mtanashati na mwenye muonekano maridhawa, tabasamu lake limekuwa likihadaa nyoyo za wasichana wengi. Sauti yake tulivu isiyo na mitetemo ilizidi kuwaburudisha wengi pindi ipenyapo masikioni mwao. Umaarufu wa Tony ulichagizwa na upekee wa falsafa na misimamo yake binafsi, kamwe hakuruhusu mtu afanye maamuzi kwa niaba yake. Juhudi na ubunifu katika kila alichokifanya ukampa Tony heshima ya kipekee na kuwa kifani kwa vijana wa rika lake.

Tony ni mtu anayependa kusoma na kufatilia vitabu na majarida mbalimbali ya wanafalsafa na wanasaikolojia, kwake yeye mwanamke ni kiumbe dhaifu kinachoendeshwa kwa hisia na mihemko lakini mwanaume siku zote ni bora anayeongozwa na nguvu ya kufikiri kwanza kisha hisia na mihemko huja baadaye. Misimamo yake ilimuaminisha kuwa Mapenzi ya kweli hupatikana zaidi kwenye riwaya na tamthilia, mwanamke yupo kwa ajili ya kumfurahisha na kumburudisha mwanaume, hivyo kwake kuwa na uhusiano na msichana zaidi ya mmoja halikuwa jambo la kushangaza. Tony ni kati ya vijana wachache waliojaliwa kuwa na maneno matamu na makali ambayo aliyatumia kama silaha ya kukata nyoyo za warembo wengi.

***************
Ni jioni moja tulivu iliyopambwa na mawingu mepesi huku mvua za rasharasha zikipunguza vumbi la mji mdogo na wa kitalii Bagamoyo, Sauti za ndege wanaorejea katika viota vyao zilichagiza kutoa melodi tamu masikioni mwa wapenzi wawili walioketi ndani ya sebule yao kubwa na yenye kupendeza wakiongea na kufurahi.

“Tony asante kwa mapenzi unayonionesha, nakili kuwa wewe ni mwanaume wa pekee sana,” alisema Theresa.
Theresa au Tedy amefahamiana na Tony kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa, lakini kwa jinsi alivyompenda Tony ni kama amekuwa akifahamiana naye kwa kipindi cha miaka, ukweli alihisi amechelewa sana kuwa naye.
“Tedy wewe ni msichana mrembo na mwenye uzuri wa asili mimi ni wako nawewe ni wangu tuu,” Tony alijibu huku akiishika mikono ya mpenzi wake.
“Kuwa nami hivi siku zote, niahidi kuwa tutakuwa pamoja hata baada ya kifo, mi nawe ni moyo mmoja katika miili tofauti, kuwa nami usiniache Tedy,” aliendelea kuongea maneno ambayo moja kwa moja yalimfanya mwanadada yule kupata msisimko wa ajabu na kujihisi kuwa yeye ni msichana mwenye bahati kuliko wengine wote.
“Asubuhi kwangu haijakamilika bila uwepo wako, napenda kukuona mchana na jioni kadharika, wewe ni maumivu yasiochosha, nitakupenda daima.”

Tony alizidi kuzama na kuchukua nafasi kubwa moyoni mwa binti yule, wakati akiendelea kuongea na kumfanyia vituko vya hapa na pale ghafla simu yake ikaita, kuiangalia akakuta ni swahiba wake wa siku nyingi Darmian, akakaa sawa na kuipokea,
“Niaje wa obey!”
“Hakuna cha obey wala uswazi leo, kisanga kinakuja kwako”, alijibu Darmian.
“Nini?” Tony alishtuka kusikia kauli hiyo ya rafiki yake.
“Yaani hadi dakika hii, ninavyozungumza Vanessa anakaribia kufika kwenu sasa kama upo bado na Tedy jua kazi unayo,” alisema Darmian na kukata simu.

Taharifa ile ilimchanganya kidogo Tony japo alikuwa mtu wa kuchanganya sana wasichana lakini haikutokea hata siku moja akawakutanisha, anayafahamu vizuri sana maumivu ya mapenzi. Alijitahidi kila awezavyo asije gonganisha magari, mabadiliko yale ya muda mfupi yalimshtua kidogo Tedy na kuanza kuhoji,
“Vipi mpenzi mbona umebadirika ghafla kuna tatizo gani?”
“Hamna kitu nipo sawa”
“Mbona kama unahofu hivi?”

Tony akashindwa kutoa majibu mazuri kwa mpenzi wake, akajikuta njia panda asijue afanye nini ili kuepusha fumanizi ambalo ndani ya muda mfupi linaweza kutokea. Wakati akiendelea kufikiri, akapata wazo la kumpigia tena Darmian ili aone kama anaweza kumsaidia kumzuia Vanessa asifike nyumbani. Akapiga simu ikaita kwa muda mrefu bila majibu, wakati akiendelea kuyafanya hayo Tedy nae akaanza kupata wasiwasi asielewe nini kimemkuta mwanaume wa ndoto zake.
“Babe! Mboni hivyo sikuelewi ujue,” alisema Tedy huku akisogea zaidi alipo mpenzi wake.
Tony akasimama na kusogea mbali kidogo na alipokaa Tedy, akatembea umbali mfupi kisha akageuka na kumtazama mahabuba wake kwa tabasamu zito.
“Dunia yangu ipo mikononi mwako, wewe ni zaidi ya paradiso kwangu, uko kama mashairi nami ni muziki, wewe ni matamanio yangu, nami ni mpendwa wako”

Maneno yale yakaondoa hofu ambayo Tedy alikuwa ameshaanza kuipata akajikuta akifurahi mno, lakini wakati Tony anayaongea hayo tayari Vanessa akawa amefika mlangoni hivyo akaanza kupiga makofi ya pongezi kwa Tony. Vanessa akashtuka sana alipokutanisha macho yake na Tedy, vivyo hivyo Tedy nae akabaki katika sintofahamu kuona uwepo wa msichana mwingine pale japo hawakuwa wakifahamiana wala kuonana kabla. Tedy akajikuta akisimama kumtazama Vanessa ambaye alikuwa akipiga hatua fupi fupi kuelekea alipo Tony.

Tony hakuonesha kushtuka ila akajikuta akiangua kicheko kilichowashangaza Tedy na Vanessa, akachukua rimoti na kuwasha muziki kwa sauti ya juu kidogo. Akamfata Tedy na kuanza kucheza naye alipokaa sawa akamgeukia Vanessa ambaye alionekana kama anataka kuuliza kitu lakini maswali yote yaliisha baada ya Tony kumshika mkono ivyo naye akajikuta anatulia, wakacheza muziki kwa muda wa kama dakika 5, kisha Tony akazima na kukaa chini, nao pia wakafanya vile vile.

Tony akachukua maji na kumimina kwenye Bilauri ya shaba na kunywa hili kuburudisha Koo lake lililokauka. Kisha akawatazama Vanessa na Tedy kwa uchangamfu wa hali ya juu,
“Nimeamini msemo ule wa kuwa mwanamke ni pambo la nyumba, uzuri wenu umeifanya nyumba yangu kuwa kama paradiso ndogo, harufu ya manukato yenu..............aaah so good” akashusha pumzi ndefu.
“Tedy huyu anaitwa Vanessa ni wifi yako,” Tedy akatoa tabasamu na kumpa mkono Vanessa.

Akamgeukia Vanessa na kusema maneno yale yale aliyosema kwa Tedy, Vanessa nae akatabasamu, alivyoona ametoa utambulisho ambao utakuja kuibua maswali ambayo hasingeweza kuyapatia majibu akatafuta namna ya kufanya hili wasigunduane kuwa ni wake wenza, Tony akafikiri kidogo kisha akamgeukia Vanessa na kumwambia,
“Wewe sio mgeni hapa, naomba ukajichukulie kinywaji ukipendacho na nikipendacho alafu tuje tusherekee”.
Van bila kusita akanyanyuka na kuelekea kule ambapo vinywaji vinaifadhiwa. Tony alivyoona Van ameenda akamsogelea Tedy na kumshika kiuno kisha kwa sauti ya taratibu akamwambia,
“Kuwa huru mpenzi wifi yako hana noma,” kisha akamsogeza karibu zaidi na kumbusu.
“Sawa honey nitakuwa huru”

Jibu lile lilimfurahisha Tony ambaye aliamua kutumia nguvu kubwa kucheza na akili za wasichana hao hili wasije kugundua kuwa wote wana nafasi sawa kwake, akaamua kucheza mchezo huo wa kumfanya mmoja dada na mwingine mpenzi kwa kuwatambulisha kila mmoja kuwa ni wifi wa mwenzie. Hama kweli mwanamke ni kiumbe kinachoongozwa na hisia bila kuwa na uwezo wa kufikiri kwa haraka, sijajua kwanini warembo wale hawakuhoji zaidi wakabaki kusadiki maneno yake na kila mmoja kujiona bora.

Tony akamwachia Tedy ambaye hakutamani kuachiwa hata kwa dakika moja,
“Honey naona wifi yako anachelewa kurudi ngoja nikamwangalie kwanza amekutwa na nini,” alisema Tony na kuanza kupiga hatua ndefu kuelekea kule alipo vanessa, lakini kabla hajafika akakutana naye njiani.
Mhmh! Ni nini kitakuwa kimetokea…
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 2
+255 713 373731

ILIPOISHIA………
Katika sehemu ya kwanza tulishuhudia Tony akiwahadaa wasichana wawili kwa wakati mmoja pasipo wenyewe kujielewa, je mambo yatakuwaje Vanessa na tedy watashtukia mchezo huo…..

Tuendelee…………

Tony akamshika mkono na kurudi naye kwenye stoo ya Vinywaji. Nyumba ya Tony ni kubwa mno na alitumia ubunifu wa hali ya juu kuhakikisha kila hitaji linakuwa na sehemu yake, alijitahidi kuweka maktaba ndogo ambapo huwa anajisomea vitabu na majarida mbalimbali, pia kukawa na sehemu ya kuhifadhia vinywaji tofauti na kwenye jokofu. Tony hakuacha kutenga sehemu maalumu kwa ajili ya kufanyia sala zake kwa Mungu japo changamoto za ujana zilimzidi nguvu.

Akaichukua ile chupa ya mvinyo aliyoishika Vanessa na kuiweka pembeni, hakupoteza muda akamvuta kwa karibu na kuanza kumbusu, Mapigo ya moyo ya Vanesaa yakaanza kwenda mbio kuliko kawaida,
“Kwanini umekuja bila kunitaarifu mapema, ona sasa nakosa uhuru wa kukubusu kutokana na heshima yangu kwa wifi yako”
“Samahani mpenzi sikuwa nafahamu kama una mgeni leo,” Vanessa alijibu.
Tony akaendelea kuvuluga akili ya mwanadada yule kwa kumshika na kumbusu kila mahali,
“I real missed you (nimekupeza sana),” alisema Tony
“I missed you too honey (nimekupeza pia mpenzi), Van akarudisha majibu.
Tony alivyoona amefanikiwa kwa kiwango kikubwa akamwachia Van na kuichukua ile chupa ya mvinyo,
“Twende wifi yako asije kujisikia mpweke”.
Wakaongozana hadi alipo Tedy kisha kwa pamoja wakafungua mvinyo ule na kuanza kuunywa taratibu huku wakisindikizwa na muziki laini.

******************

Darmian baada ya kuona kuwa Tony alimpigia sana bila ya yeye kujibu akahisi hali ya hatari kichwani mwake. Ingawa alichoshwa na tabia ya rafiki yake ya kucheza na nyoyo za wasichana wengi kwa wakati mmoja lakini akaamua atafute namna ya kwenda kumsaidia hivyo akaamua ampigie rafiki yake mwingine,

“Oyah upo wapi wewe?” akauliza Darmy baada ya simu kupokelewa.
“Ndio nimetoka kazini naelekea nyumbani,” akajibu Yassir.
“Sasa tukutane basi hapo Mapinga twende kwa Tony naona ana tatizo kidogo”
“Tatizo!” akauliza Yassir kwa mshangao.
“Ndio! Jamaa naona leo kapata fumanizi”.
“Duuh! Kwa hiyo kawakutanisha Mirrium na Vanessa au?”.
“Aah! Mirrium mbona alishaachana naye kitambo sasa hivi ana mwingine anaitwa Tedy”.
“Duuh! Kweli ni shida, poa nipe dakika 10 nitakuwa hapo”
“Sawa usikawie asee”.
Darmian akakata simu na kuanza safari ya kuelekea walipopanga kukutana na Yassir.

Baada ya muda mfupi wakawa wamekaribia kabisa kufika nyumbani kwa swahiba wao, wakakuta geti limerudishwa tuu halikufungwa vizuri na kwa kuwa walishazoea kwenda mara kwa mara, wakaingia bila kusubili kukaribishwa. Wakapita katika bustani iliyo mbele ya nyumba na moja kwa moja hadi kwenye mlango mkubwa, lakini kabla hawajaingia ndani wakashangaa kusikia watu wakiongea na kufurahi. Maswali yakaanza kuzunguka vichwani mwao, shauku ya kutaka kujua nini kilichojili ikaongezeka.

Wakasikia watu wakiongea na kucheka mno, wakatazamana kwa mshangao kidogo sababu walijua wangekuta ugomvi mzito. Kwa pamoja wakaingia ndani na kukuta Tony akiwafanyia vituko vilivyowafurahisha mno, Tony alivyowaona akashusha pumzi ndefu na kunyoosha mikono juu kushukuru,
"Karibuni sana," akawakaribisha.
"Asante," Darmy akaitikia.
"Mambo zenu warembo," Yassir akawasalimu.

Tedy na Van nao wakaitikia na kwa pamoja wakakaa na vinywaji vikaongezwa wakaendelea kunywa na kuongea hili na lile.
Darmy akaendelea kufikiri juu ya mchezo alioucheza Tony asipate jibu akatamani kujua nini kilijili lakini hakuweza kuuliza kwa wakati ule. Ikamlazimu avute subira Zaidi hadi warembo wale watakapoondoka, matamanio yake yalitimia baada ya muda mfupi pale Vanessa na Tedy walivyoaga kwa pamoja kuwa muda umeenda na wanahitaji kurejea majumbani mwao. Tony alihofia mno kwa wasichana wale kama wangeongozana peke yao lolote lingetokea katika maongezi yao, akafikiri kitu kidogo kisha akasema,

“Vanessa Subiri kidogo acha nimsindikize Tedy”
“Kweli Van endelea kubaki nasi kidogo, kwanza mama hana shida alafu nyumbani ni hapo tuu karibu, acha Tony amsindikize Mgeni sisi tuendelee kupiga soga,”alisema Yassir.
Van bila kipingamizi akakubali, Darmy akamuangalia Tony na kumuonesha ishara ya dole gumba kuashiria kuwa asihofu kila kitu kiko sawa.
Tony akatoka na kimwana yule na kuwasha gari tayari kwa safari ya kumrudisha kwao,
“Asante mpenzi nimefurahi sana kuwa na wewe leo, hata wale rafiki zako na yule wifi yangu kwakweli ni wachechi mno,” Tedy alisema.
“Usijali mpenzi, nafanya yote kuhakikisha unafurahi”
Jibu lile liliiburudisha nafsi ya Tedy pasipo kujua kuwa ana wenzake wengi tuu, safari iliendelea hatimaye wakafika, Tedy akamtazama Tony kisha akambusu na kushuka kwenye gari.
Tony akamsindikiza kwa macho hadi alipoingia ndani akageuza gari na kurejea kwake ambapo akamchukua vanessa na kumfikisha nyumbani kisha akawasindikiza na maswahiba zake,
“Ebhana eenh leo umewezaje kuwa na wanawake wawili kwa wakati mmoja na wasifahamiane?” Yassir akafungua maongezi maana ya kimya kifupi kupita.
“Nilicheza tuu na saikolojia zao, nikaizuia hofu kwangu na kumfanya kila mmoja afurahi kwa nafasi yake,” akajibu Tony.
“Ila uoni kama ni hatari kuendelea kuwachanganya hivi, kwanini usichague mmoja ukatulia naye,” Yassir akaendelea kusema.
Kauli ile ilimfanya Tony afunge breki ya ghafla ambayo iliwashtua wote, kisha akapiga piga usukani kwa hasira na kumgeukia Yassir,
“Lini umekuwa na kichwa cha panzi kiasi cha kusahau yote ndani ya muda mfupi, leo hii wewe umekuwa wa kuniambia nitulie na msichana mmoja,” Tony aliongea kwa hasira mno.
“Kweli Tony wakati umefika lazima ufanye maamuzi magumu, chagua yule unayeona unampenda kuliko wengine,” Darmy naye akaongozea.
“Kupenda! Mnajua nini nyinyi kuhusu kupenda, mmesahau kisa cha mpendwa kupenda asipopendwa akatendwa na kwenda, lakini kule alikopendwa hakupenda!”.
Tony akashusha pumzi ndefu kisha akaendelea kuongea,
“Ninyi ni marafiki zangu wa muda mrefu sana, najua mna nia njema kwangu lakini kwa hili naomba mniache tu”
“Kweli sisi ni rafiki zako lakini unatupa wakati mgumu sana, hivi hao wanawake wakija kugundua kuwa unawachezea watatufikilia vipi sisi. muda ndio huu funika yaliyopita na usonge mbele, binafsi leo ndio mara ya mwisho siwezi tena kujiingiza kwenye ujinga wako,” aliongea Yassir kisha akafungua mlango na kushuka kwenye gari na kuondoka, Darmy nae akafanya vile vile na kumuacha Tony akiwa mwenye kuwaza sana.

Mhmh nini hatma ya marafiki hao je Tony atakubali kubadirika?
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 3
+255 713 373731

#ILIPOISHIA………
Tony akashusha pumzi ndefu kisha akaendelea kuongea,
“Ninyi ni marafiki zangu wa muda mrefu sana, najua mna nia njema kwangu lakini kwa hili naomba mniache tu”
“Kweli sisi ni rafiki zako lakini unatupa wakati mgumu sana, hivi hao wanawake wakija kugundua kuwa unawachezea watatufikilia vipi sisi. muda ndio huu funika yaliyopita na usonge mbele, binafsi leo ndio mara ya mwisho siwezi tena kujiingiza kwenye ujinga wako,” aliongea Yassir kisha akafungua mlango na kushuka kwenye gari na kuondoka, Darmy nae akafanya vile vile na kumuacha Tony akiwa mwenye kuwaza sana.

#Tuendelee…………
Tony ni mmoja kati ya waongozaji wa filamu wenye mafanikio na upekee katika kazi zake, ubunifu, umakini na kujituma kwake kukaifanya kampuni ya STUDIO 7 MEDIA LTD. kukua na kutambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, mbali na mtazamo hasi juu ya wanawake lakini hakuwanyima fursa ya kufanya kazi walau kwa majukumu machache.
Upekee wa kampuni hiyo ndio uliosaidia kupata nafasi ya kuingia ubia na kampuni moja ya kikorea iliyofahamika kwa jina la TAE XHIANG SUNG GROUP, kampuni hii imejikita Zaidi katika maonesho ya mitindo na matangazo mbalimbali hivyo kwa kampuni ya Tony ilikuwa nafasi muhimu sana ya kuzidi kutanua wigo wa kazi yake.

Ni asubuhi moja tulivu yenye mawingu mepesi yaliyofanya siku hiyo kuwa na baridi kiasi, Tony akiwa kitandani akashtushwa na mlio wa simu yake, akaamka na kuangalia akagundua kuwa ni alarm aliyoitega ili imuamshe. Siku hiyo alikuwa na kikao cha muhimu sana, kitakachotoa mpango kazi kati ya kampuni yake na ile kampuni ya kikorea iliyofungua tawi hapa nchini, hivyo ikabidi ajiandae haraka tayari kwa ajili ya safari ya kwenda Ubungo plaza ambapo kikao kimepangwa kufanyika. Alipojaribu kuwasha gari likakataa kuwaka, hakupoteza muda kujua tatizo ni nini akaamua atumie usafiri wa umma kwa siku hiyo. Gari lilisimama karibu kila kituo jambo ambalo lilimkera Tony na akaanza kuona dalili za kuchelewa kikao.

Walipofika maeneo ya makongo wakakuta kuna foleni kubwa uliyoenda hadi mwenge na alivyotazama saa yake akaona amebakiwa na nusu saa kabla ya kikao kuanza, ikabidi ashuke na kupanda pikipiki. Akamuhimiza dereva wa pikipiki ile aongeze mwendo ili aweze kuwahi. Nausifu ujanja wa dereva yule kwani alijitahidi kupenyapenya kukwepa foleni ile lakini walipofika maeneo ya mawasiliano dereva alipoteza umakini kidogo na kujikuta akielekea kuivaa gari ndogo aina ya Ferrari akajitahidi kufunga breki lakini akuweza na kujikuta akiigonga kwa nyuma. Wote wakaanguka na kwa bahati nzuri hakuna aliyeumia zaidi ya ile pikipiki na gari, ndani ya sekunde kadhaa watu wakawa wamezunguka eneo lile, ugomvi ukazuka na wote wakataka kumpiga dereva wa pikipiki kwa kutokuwa makini.

“Jamani msimfanye chochote huyu dereva, kosa ni langu mimi ndiye niliyekuwa nikimchochea aongeze mwendo kwani nina kikao cha muhimu nahitaji kuwahi,” Tony alitoa utetezi wake.
“Mpumbavu wee! kikao ni muhimu kuliko usalama wako?” akasema mwananchi mmoja ambaye sikumfahamu Jina Lake.
“Naweza kusema hivyo ila tafadhalini sana msifanye lolote na naomba kuongea na mwenye gari sina muda zaidi wa kukaa hapa,” alisema Tony.

Mzozo uliendelea na ndani ya muda mfupi akatokea msichana ambaye kuwepo kwake tuu, kulifanya watu wote wakae kimya na kila mmoja aliduwazwa na uzuri wake. Akasogea akaliangalia lile gari kisha akamuangalia dereva wa pikipiki na kisha kumtazama Tony, ama kwa hakika ukimuangalia analipsi za kuvutia, kidevu ndio sisemi kitu jamani, macho yake ang’avu yalifanya nyoyo za vidume wengi kukimbia zaidi ya kawaida, umbo namba nane na mwenye mvuto zaidi ya maua wanaume wengi wakajikuta wakitaka kuonesha ubavu wao kumsaidia mrembo yule,

“Samahani sana dada yangu ni bahati mbaya tuu,” aliongea dereva wa pikipiki.
Yule mwanadada akamuangalia kwa dharau sana kisha akasonya,
“Unajua thamani ya hii gari? Unajua ni kiasi gani cha pesa unachotakiwa kulipa kwa ajili ya hii gari, nafikiria kukuweka polisi kwa muda hadi utakapolipa pesa yangu,” aliongea mrembo kwa dharau na hasira kidogo.
“Naomba nilipe mimi gharama za kutengeneza gari lako, haya yote yametokea kwa sababu yangu” Tony akazungumza.
Yule msichana akamuangalia Tony kisha akacheka kwa dharau sana, Tony alivyoangalia saa yake akagundua kuwa zimebaki dakika 5 kikao kuanza akakosa Amani na akahofu zaidi nini kitatokea endapo atakikosa kikao kile muhimu.
“Tafadhali dada yangu nina haraka mno, naomba tusifanye mambo kuwa makubwa binafsi nitalipa deni hili”
“Lipa sasa hivi! Asiondoke bila kulipa huyo! Wamezoea hao!” yalikuwa maneno ya baadhi ya watu waliokuwa eneo lile.
Tony akamshika mkono mrembo yule na kumsogeza pembeni lakini kitendo kile kikamchukiza mara dufu msichana yule, akanyanyua mkono wake na kumzaba kofi Tony, asee nafsi ilimuuma mno akatamani ajibu mapigo lakini akajiona mjinga endapo atafanya tukio lile, akajitahidi kujizua kisha akamuangalia usoni mwanadada yule,
“Huna hadhi ya kuhushika mkono huu masikini wewe na usirudie tena kunigusa, kwa kuwa umenianza mimi namaliza lazima ulale kituo cha polisi leo, unajua mimi ni nani?” msichana aliendelea kuongea kwa vitisho.

Tony alizidi kuumia nafsini kwani hata siku moja hakukubali kudhalilishwa na mwanadamu hasa wa kike, hasira zikampanda akamwangalia mwanadada yule kisha akajikuta anacheka mno,
“Sawa fanya unalojisikia ila huyu dereva muache aende,” Tony akasema na kumpa kiasi kidogo cha fedha dereva yule wa pikipiki ambaye alishangaa sana ukarimu wa Tony kwani toka aanze kufanya kazi ile hakuwahi kukutana na mteja wa namna ile akashukuru na kuondoka.

Mrembo bado akawa na nia ya kumdhalilisha Tony mbele ya watu ambao wengi walishaanza kupiga picha na kurekodi kwa simu zao tayari kwa kuziachia kwenye mitandao ya kijamii, Tony akatoa kitambulisho chake cha taifa na akatoa namba zake za simu na kumkabidhi yule msichana,
“Nakuamini na naomba uniamini, peleka gari yako gereji yeyote kisha baada tu ya kikao kuisha nitakuja hapo kulipa gharama zote, nitumie ujumbe wenye malekezo ya hiyo gereji kwa sasa naomba uniache niende”
Tony akusubili kuambiwa nenda akaanza safari baada tu ya msichana yule kuipokea ile dhamana, ya kitambulisho.

*************

Kikao kikaanza bila hata ya Tony kuwasili, wadau wakaanza kujadili mambo mbalimbali juu ya uendeshwaji wa kampuni izo mbili ilipofika zamu ya STUDIO 7 MEDIA LTD kuelezea namna kazi itakavyoenda kila mmoja akashangaa kutokumuona mkurugenzi wa kampuni hiyo, ikabidi mkurugenzi wa kampuni ya kikorea asimame na kuongea kwanza,

“Nasikitika katika kikao cha kwanza mshirika mwenzetu kushindwa kufika, hii inanipa wasiwasi kidogo mimi kama mwakilishi na msimamizi wa kampuni hii ya TAE XHIANG SUNG GROUP kwa hapa Tanzania, japo sijajua ni sababu gani zilizomfanya hadi muda huu asiweze kufika lakini huu naweza kuuita uzembe usiweza kuvumilika,” aliongea Martha ambaye ni msimamizi wa kampuni ile.

Martha ni msichana anayejiamini mno katika kila analolifanya, yeye asili yake ni mtanzania japo kwa muda mrefu sana alikuwa nchini Korea kimasomo na kubahatika kufanya kazi huko huko ivyo kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi kufungua tawi hapa nchini ilitokana na juhudi zake binafsi,

Mhmh! Je Tony atawahi kikao kile cha muhimu na vipi kuhusu deni atalilipa au atalipotezea?
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 4
+255 713 373731

ILIPOISHIA………

“Nasikitika katika kikao cha kwanza mshirika mwenzetu kushindwa kufika, hii inanipa wasiwasi kidogo mimi kama mwakilishi na msimamizi wa kampuni hii ya TAE XHIANG SUNG GROUP kwa hapa Tanzania, japo sijajua ni sababu gani zilizomfanya hadi muda huu asiweze kufika lakini huu naweza kuuita uzembe usiweza kuvumilika,” aliongea Martha ambaye ni msimamizi wa kampuni ile.
Martha ni msichana anayejiamini mno katika kila analolifanya, yeye asili yake ni mtanzania japo kwa muda mrefu sana alikuwa nchini Korea kimasomo na kubahatika kufanya kazi huko huko ivyo kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi kufungua tawi hapa nchini ilitokana na juhudi zake binafsi,

Tuendelee…………

“Tumeipa nafasi kampuni ya STUDIO 7 MEDIA LTD kwa kuwa tuliamini ni kampuni yenye watu makini na ubunifu mwingi katika kazi lakini huu uzembe…………” kabla hajaendelea kuongea akajikuta anaduaa kumuona Tony akiingia huku akihema sana, Martha akajikuta anashindwa kuendelea kusema alichokusudia kusema,

“Lakini huu uzembe…lakini…..lakini….!” akajikuta anarudia maneno huku macho yake yakishindwa kutoka alipo Tony.
Tony aliposikia mwanadada yule anashindwa kumalizia sentensi zake akanyanyua kichwa na kutazama ili afahamu japo kwa kinaga ubaga nini tatizo, daah naye akashikwa na bumbuazi kukuta ni Mtu ambaye anamfahamu, mapigo ya moyo yakaenda mbio zaidi, akageuka kwa jirani yake na kumuuliza,
“Huyu msichana ana cheo gani?”
“Huyu ndie mkurugenzi wa kampuni uliyoingia nayo ubia”

Fikra zikaenda mbali zaidi, kila mmoja akawa anashangaa juu ya tukio lile, Tony akawa anapiga piga meza kuonesha mfadhaiko.Martha akakohoa na kikao kikaendelea, Tony akaomba radhi kwa kuchelewa, wadau wakaelewa na wakafikia makubaliano namna ya kuanza kazi. Kikao kilifungwa na wakapena mikono ishara ya umoja lakini ilipofika zamu ya Tony kupeana mkono na Martha, Tony akakwepa na kuanza kuondoka lakini kabla hajatoka akasikia anaitwa,
“Mr. Tony nakuomba mara moja,” ilikuwa ni sauti ya mmoja ya wadau wa ile kampuni ya kikorea akihitaji kuzungumza machache.
Tony akasogea alipo yule mdau ili kusikiliza nini alichoitiwa,
“Mimi ni msaidizi wa bibie hapa, hivyo natumai utatupa ushirikiano wa kutosha katika kila jambo,” alisema yule mdau.
“Shaka ondoa” Tony akajibu.
“Kwa kuwa wakurugenzi wote mpo mimi nafikiri mngepata muda wa kukaa na kuona jambo gani lianze kufanyiwa kazi”
“Ni kweli ukizingatia muda unazidi kwenda na upinzani wa kibiashara ni mkubwa,” Martha akaongezea.
“Lolote mtakaloamua nipo tayari ila kwa sasa kuna mahali nawahi tutaonana wakati mwingine” akasema Tony na kuanza kuondoka.

Ukweli Tony hakufuraishwa kabisa kufanya kazi na mrembo yule alitamani hata avunje mkataba ila kila alivyofikiria kuhusu mafanikio atakayoyapata kutokana na ubia ule ikabidi avumulie.
Akaangalia simu yake na kukuta ujumbe mfupi uliomuelekeza mahali Fulani ambapo alitakiwa afike, bila kuchelewa akaanza safari na ndani ya dakika 45 akawa amefika. Ilikuwa ni gereji moja kubwa na ya kisasa iliyopo maeneo ya sinza iliyotambulika kwa jina la Mdidi Auto Garage. Alipoangaza huku na kule akakutana na sura ya mwanadada yule ambaye asubuhi alikuwa na ugomvi nae, akasogea hadi alipo na kumwambia,
“Nimerudi kulipa deni langu”
“Kaka naomba uniletee hiyo lisiti ya malipo” akasema yule msichana na ndani ya dakika lisiti ikaletwa Tony akashtuka alipoisoma, akakuta anatakiwa kulipa laki saba na nusu pesa za kitanzania (Tsh. 750,000).
“Mbona pesa nyingi kiasi hiki, na nikiangalia gari lilivyoumia haviendani” Tony akasema.
“Usitake nikuabishe lipa pesa kama huna sema,”
“Sawa nitalipa nipe dakika 15”
“Poa kila la kheri”

Tony hakuwa na pesa hizo mfukoni ikabidi aombe msaada kwa rafiki zake ambao jana yake tuu walikorofishana ila haikusumbua kitu kwani waliweza kumsaidia kwa kutumia mitandao ya simu. Tony akasogea hadi zilipo huduma za kutolea pesa kwa njia ya mtandao na akafanikisha hilo. Akarudi na kukabidhi zile pesa kisha akasogea kwa yule msichana na kumwambia,

“Samahani sana kwa usumbufu ila ulichonifanyia leo usikisahau”
“Una maana gani”
“Ya kawaida tuu, naomba unikabidhi kinachonistahili”
Msichana akapekua pochi yake kuangalia kitambulisho alichokabidhiwa na Tony kama dhamana ya uaminifu lakini hakukiona, akatoa kila kitu pembeni na kupekua kila mahala lakini hakufanikiwa kukipata. Akakaa chini na kuanza kutafakari wapi alipokiacha kitambulisho kile, akakumbuka kuwa amekiacha nyumbani kwao, ugumu ukaja ataanza vipi kumwambia Tony kuwa amesahau kitambulisho,
“Vipi ujakiona kitambulisho! Nina mambo mengi ya kufanya, nimeshalipa deni lako nikabidhi istahiki yangu niende,” akasema Tony.
“Samahani kaka yangu nimekisahau kitambulisho chako nyumbani”
Tony akamtazama sana msichana yule akajikuta hajui amfanye nini,
“Ila kama hutojali nitakuletea popote ulipo jioni hii” aliendelea kuongea mwanadada yule huku hofu kidogo ikimtawala.
Tony akatabasamu na kuanza kuondoka bila kutoa jibu lolote, wakati anaondoka akafikiri vingi sana na akajikuta akiongea kimoyo moyo,
“Kwa kuwa umenianza, hakika sitokuacha, unawezaje kunidhalilisha kiasi kile”.

Jioni ya siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwa Tony akajikuta akizama katika dimbwi la mawazo akiyafikilia zaidi matukio ya siku hiyo kuanzia yule mrembo ambaye hakulifahamu jina lake na yule mkurugenzi mwenza aliyemfahamu kwa jina la Martha. Kila alivyofikiri kuhusu kuwa karibu na Martha ndivyo moyo wake ukajikuta ukijawa na hasira hasa baada ya kukumbuka miaka kadhaa iliyopita.

“Martha kwanini umekuja katika katika maisha yangu, japo si rahisi ila natamani uende mbali nami, kwa muda mrefu hakutokea mwanamke ambaye angeusimamisha moyo wangu walau kwa dakika na kunifanya nimfikirie yeye tuu, lakini wewe umeweza hilo, nakuchukia na lazima ulipie hili,” alisema Tony huku akinywa mvinyo wake taratibu.
“Nitayafanya maisha yako kuwa magumu kuliko kawaida, niko radhi kufanya lolote, liwe la kielevu au la kipumbavu, nitahakikisha unashuka na kuwa mtu wa chini.”
Wakati akiendelea kufikiri hayo simu yake ikaita kuangalia ilikuwa namba ngeni ikabidi aipokee,
“Hallo”
“Hallo! Naongea na Tony”
“Ndio! Nani mwenzangu?”
“Mimi ni Jamilah”
“Jamilah wa wapi?”
“Ooh! Tony unamaswali mengi nipo maeneo ya Bunju kwa sasa, niambie nikuone wapi ili nikukabidhi kitambulisho chako”
“Njoo Mapinga”
“Sawa dakika 15 nitakuwa huko”

Simu ikakatwa na mawazo juu ya Martha yakakata ghafla, Tony akajiandaa haraka huku akinuia kuwa lazima mrembo yule alipie ule uzalilishaji alioufanya juu yake, akapanga kufanya kila aliwezalo amnase mwanamke yule kimapenzi.
Baada ya dakika 15 Jamilah akawa ameshafika maeneo ya Mapinga na kabla hajampigia simu kujua alipo, Tony nae akawa ameshafika maeneo hayo. Tony alitumia takribani dakika moja kuuangalia uzuri wa msichana yule hakika alikubali kweli Jamilah ameumbwa akaumbika. Mrembo yule naye akabaki ameduwaa kwani alimuona Tony tofauti na alivyokuwa asubuhi na kadri alivyozidi kusogelewa na Tony ndivyo alivyozidi kuchanganyikiwa kwa utanashati wake, akajikuta anababaika kuongea asijue aseme nini,

“Siwezi kukupa kitambulisho chako hapa, tutafute sehemu iliyotulia tukae walau tuzungumze kidogo,” alisema Jamilah.
“Sawa twende ukapaki gari yako pale alafu tutaenda huko”
Jamilah akaenda kupaki gari yake sehemu aliyoelekezwa na Tony kisha wakasogea katika mgahawa uliyo karibu akaagiza kinywaji lakini tony akakataa na kusema kuwa alishakunywa alipotoka ivyo hajisikii kunywa chochote, jibu hilo lilimfanya Jamilah nae kughairi kuagiza kinywaji,
“Tony samahani sana kwa kile kilichotokea leo”
“Huna haja ya kuomba msamaha ila mimi ndio natakiwa kuomba radhi”
“Hapana Tony ukweli kila nikifikiria niliyokufanyia leo, moyo wangu unauma sana na sikujua kuwa wewe ni mtu mwema na mkarimu kiasi hiki, nilijisikia aibu pale niliposahau kitambulisho chako nyumbani na nilitegemea utanifanyia kama niliyokufanyia ila uko tofauti mno”
“Yameisha hayo mimi nishasahau”.
Tony alijibu japo moyoni alikuwa na hasira sana juu ya huyo msichana ila akaamua kuigiza mwema hili atomize lile analolitaka.
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 5
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Jamilah akaenda kupaki gari yake sehemu aliyoelekezwa na Tony kisha wakasogea katika mgahawa uliyo karibu akaagiza kinywaji lakini tony akakataa na kusema kuwa alishakunywa alipotoka ivyo hajisikii kunywa chochote, jibu hilo lilimfanya Jamilah nae kughairi kuagiza kinywaji,
“Tony samahani sana kwa kile kilichotokea leo”
“Huna haja ya kuomba msamaha ila mimi ndio natakiwa kuomba radhi”
“Hapana Tony ukweli kila nikifikiria niliyokufanyia leo, moyo wangu unauma sana na sikujua kuwa wewe ni mtu mwema na mkarimu kiasi hiki, nilijisikia aibu pale niliposahau kitambulisho chako nyumbani na nilitegemea utanifanyia kama niliyokufanyia ila uko tofauti mno”
“Yameisha hayo mimi nishasahau”.
Tony alijibu japo moyoni alikuwa na hasira sana juu ya huyo msichana ila akaamua kuigiza mwema hili atomize lile analolitaka.

Tuendelee…………

Jamilah akatoa kitambulisho na kumkabidhi Tony, nae akakipokea na kushukuru, wakaongea mengi na taratibu mazoea yakaanza, usiku ukaingia na wakaagana huku wakiahidiana kuonana tena siku zijazo. Uchangamfu na vituko vya Tony vilitosha kumloga Jamilah na kujikuta kutamani kuwa karibu na mkaka huyo tena na tena.

BAADA YA MIEZI MITATU

Ushirika wa kampuni mbili ukawa mkubwa na maarufu katika macho na masikio ya watanzania wengi, umaarufu huu haukuishia Tanzania tuu ulivuka mipaka na kuenea katika nchi nyingi za Asia hasa zilizo karibu na Korea. Tony alijitahidi kutengeneza Makala mbalimbali zilizoonesha mitindo yenye utamaduni wa kiafrika na kiasia, Kama utafatilia vizuri mpenzi msomaji Afrika na Asia tamaduni zao zinafanana kwa kiasi kikubwa tofauti na zile tamaduni za Ulaya na Amerika. Kila mmoja alifurahia mafanikio hayo na kukaandaliwa na sherehe maalumu kwa ajili ya kupongezana. Sherehe hiyo ikapangwa kufanyika katika moja ya hoteli za kitalii zilizopo katika fukwe za bahari ya Hindi katika mji mdogo wa Bagamoyo. Wafanyakazi wote wakataalifiwa hivyo kila mmoja akawa akiisubiri siku hiyo kwa hamu zote.

Siku ya siku ikafika Tony akiambata na maswahiba zake Darmy na Yassir ambapo kila mmoja alikuwa katika suti moja matata sana, Siku hiyo iliwafanya waonekane wa tofauti sana,
“Tangulieni ndani kuna mtu namsubili,” akasema Tony.
“Duuh! Kama kawaida yako,” Yassir akadakia.
“Haya nani huyo anayekuja leo, Vanessa au Tedy?” Darmy akauliza.
“Si Tedy wala si Van, ila ni…..acha iwe surprise mtamuona akifika”
Darmy na Yassir wakatazamana kisha wakaingia ndani bila kuongeza neno, Tony akaendelea kusubili na ndani ya muda mfupi mwanadada mwenye urembo wa asili akawasili. Tony alitumia dakika moja kuthibitisha kuwa yule ni binadamu au malaika,
“Hakika mwanamke ni sawa na waridi lenye kuvutia na kunukia vizuri, kama ilivyo kazi ya waridi kupendezesha nyumba ndivyo ilivyo kazi ya mtu mke kumburudisha na kumstarehesha mtu mume,” Tony akasema hayo maneno moyoni, akaachia tabasamu zito na akuweza kuzuia mikono yake kumkumbatia mwanadada yule pindi alipomkaribia.

Kwa pamoja wakaongozana ndani wakaangaza huku na huko wakakuta kuna meza tupu, wakajongea na kukaa hapo, Uzuri wa binti yule ulizua gumzo kubwa kwa wageni wote waliolikwa kwenye sherehe hiyo. Darmian na Yassir wakashindwa kuvumilia kule walipokaa,
“Ebhana eenh! Umeona kule,” Darmy akasema.
“Wapi tena?” Yassir akauliza.
“Kule kwenye meza ile”
“Wee! Yule mtoto mzuri vile Tony kamtolea wapi”
“Mhmh! Kwani wewe ndio umemfahamu leo?”
“Daah! Yule jamaa sijui anauchawi gani, yeye tuu kila siku anaibua wapya”
“Ila usifikirie sana labda anaweza kuwa rafiki tuu”
“Aah! Kama ni rafiki yake tuu, nitaomba aniachie mie yule mtoto”
“Wewe mjinga si umeoa acha tamaa nitakusemea mie”
“Daah! Vunga jamaa yangu ila twende palepale walipo”
Wakati wakiinuka kuelekea alipo Tony, Mshehereshaji akashika kipaza sauti na kuomba wageni waalikwa wote wasogee katika viti vya mbele hili sherehe iweze kuanza. Darmy na Yassir wakafika alipo Tony wakatabasamu na kukaa, ikabidi utambulisho mfupi ufanyike hili kuwafanya wawe huru zaidi katika maongezi yao,
“Jamilah hawa ni rafiki zangu wa karibu sana, huyu ni Darmian na huyu ni Yassir,” akawageukia rafiki zake na kuendelea utambulisho.
“Oyah ni shemeji yenu”
“Eenh! Shemeji!” Yassir akajikuta akiuliza kwa mshangao zaidi.
“Kwani ujasikia au ndio mbwembwe,” akasema Darmy.
“Nafurahi kuwafahamu,” Jamilah akasema huku akiwapa mikono wale maswaiba wa Tony.

Sherehe ikaanza kwa watu mbalimbali kuongea na kuonesha wazi kufurahishwa na juhudi za kampuni hiyo katika kukuza utamaduni wa Nchi, ikafika zamu ya mgeni rasmi ambaye pia ni naibu waziri wa Utamaduni, Habari na Michezo. Waziri alifuraishwa sana na hatua ya kampuni ya Korea kuja kuwekeza nchini kwetu, na hii imesaidia sana kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengi aidha Waziri alishukuru pia kwa kuutangaza utamaduni wa nchi yetu.

Ikafika hatua ya utoaji Tuzo kwa viongozi wa kampuni zote mbili, TAE XHIANG SUNG GROUP ikawa ya kwanza kuitwa kupokea Tuzo ya heshima. Taa zikazimwa na macho ya wote yakawa katika zulia jekundu ambapo kwa mwendo wa madaha kabisa mwanadada ambaye naweza kusema yeye ni zaidi ya mrembo akawa akitembea kueleka jukwaani, Darmy na Yassir wakashtuka mno wote kwa pamoja wakajikuta wakisema,
“Martha…!”

Jina lile lilivyopenya kwenye masikio ya Tony akajikuta akiangusha glasi aliyoishikiria mkononi mwake, taratibu akanyanyua shingo yake na kutazama kwenye zulia jekundu. Moyo ukamuenda mbio zaidi, Jamilah akabaki kuwashangaa asijue lolote, wakati akiendelea kushangaa Martha akawa ameshafika jukwaani na kupokea Tuzo ile. watu wakampongeza kwa makofi mengi kisha akasogea pembeni, Waziri akaendelea tena kwa kutoa tuzo kwa kampuni zalendo, jina la Tony likaitwa naye bila kuchelewa akamshika mkono Jamilah na kuongozana naye lakini kabla hajaenda Yassir akataka kumzuia kwa sababu aliona hatari ya kufanya vile. Waandishi wa habari walikuwa wengi eneo hilo hivyo kila tukio lilinaswa na kamera zao, Darmy na Yassir walifikiri itakuaje kwa Vanessa na Tedy ambao bila shaka watafatilia habari juu ya tukio hilo. Tony hakujali akaongozana na Jamilah, muonekano wao usiku huo ni kama maharusi, watu walishangilia mno, hali ilikuwa tofauti kwa Martha, alionesha wazi kuchukizwa na tukio hilo nafsi yake ilikaangika mno akapaona pale mbele pachungu. Wakafika jukwaani na Waziri mwenye zamana akatoa Tuzo ile.
Mshehereshaji akampa Martha kipaza sauti walau aongee machache, lakini hakuweza kusema kitu zaidi ya machozi kumtiririka, Tony alipoona vile akafurahi mno na kujisemea moyoni,

“Pole sana Martha, huu ni mwanzo tuu, picha kamili linakuja”
Mshehereshaji alivyoona Martha anashindwa kuongea akaamishia kipaza sauti kwa Tony, naye akakipokea na kuvuta pumzi ndefu kisha akasema,
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwanza, ambaye naamini kwa nguvu zangu nisingeweza kuwa hivi nilivyo leo. Pia shukrani kwa rafiki zangu wa karibu sana, Darmy na Yassir, Shukrani pia kwa wafanyakazi na uongozi mzima wa TAE XHIANG SUNG GROUP na shukrani za kipekee kwa Martha”.
Alipolitaja hilo jina kila mmoja akashangaa, watu wakawa kama wanaangalia picha la kihindi hasa baada ya Tony kugeuza shingo na kumtazama mrembo yule ambaye hatukujua kilio chake ni cha furaha au huzuni, japo alijitahidi kwa kiasi kikubwa kujenga tabasamu usoni mwake.
“Martha, nimejifunza mengi kupitia wewe, tamu na chungu vyote nimevijua asante sana,”
Akarudisha kipaza sauti na kumshika mkono Jamilah tayari kwa kuelekea kwenye nafasi yake.

Sherehe ikaisha na safari ya kurudi majumbani ikaanza Tony akaambata na marafiki zake pamoja na Jamilah, njia nzima kila mmoja akawa kimya hamna aliyejaribu kuuliza kitu. Tony alionekana mwenye mawazo mengi jambo lilimpa wakati mgumu Jamilah kuelewa nini kinazunguka vichwani mwao, wakafika Mapinga Darmy na Yassir wakashuka na Kuelekea makwao, Tony akageuka na kumtazama Jamilah,

“I want to spend this night with you, (nataka kuwa nawe usiku huu)”
“Its ok, am yours (sawa mimi ni wako tuu),” akajibu Jamilah huku akiupapasa mkono wa Tony kuashiria amekubali mualiko ule.
Safari ikaendelea na hatimaye wakafika nyumbani kwa Tony, Jamilah alishangazwa na ukubwa wa nyumba ile,
“Ina maana nyumba yote hii unaishi mwenyewe?”
“Ndio, naishi peke yangu”
“Mhmh! Umewezaje kuishi upweke kiasi hiki?”
“Aah! siwezi kuona upweke wakati wewe upo hapa”
“Wazazi au ndugu zako wako wapi?”
Jamilah akajikuta anauliza maswali mengi ambayo hayakuwa na umuhimu sana kwa wakati ule, Tony alivyoona Maswali yanazidi kuwa mengi akamsogelea Jamilah na kumshika kiuno kisha akamsogelea karibu zaidi na kumtazama usoni,
“Sasa nani…… anaye….ku…..pi….kia,” Jamilah akajikuta akihema kwa kasi mno na kushindwa kumalizia sentensi yake. Tony akamuangushia tabasamu zito na kumwambia,
“Acha nyoyo zetu zizungumze sasa, unachokihisi au ninachofikiri ni vigumu kukielewa, nataka usiku huu uwe wa kihistoria katika maisha yetu,”
“Tony nashindwa kujizuia kusema kuwa nakupenda sana, nifanye niwe wako siku zote”
“Shiiiii! Usiseme kitu”
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 6
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Jamilah akajikuta anauliza maswali mengi ambayo hayakuwa na umuhimu sana kwa wakati ule, Tony alivyoona Maswali yanazidi kuwa mengi akamsogelea Jamilah na kumshika kiuno kisha akamsogelea karibu zaidi na kumtazama usoni,
“Sasa nani…… anaye….ku…..pi….kia,” Jamilah akajikuta akihema kwa kasi mno na kushindwa kumalizia sentensi yake. Tony akamuangushia tabasamu zito na kumwambia,
“Acha nyoyo zetu zizungumze sasa, unachokihisi au ninachofikiri ni vigumu kukielewa, nataka usiku huu uwe wa kihistoria katika maisha yetu,”
“Tony nashindwa kujizuia kusema kuwa nakupenda sana, nifanye niwe wako siku zote”
“Shiiiii! Usiseme kitu”

Tuendelee…………
Tony alizidi kumkoleza mrembo yule kwa maneno yaliyopenya moja kwa moja mtimani, aliugundua udhaifu wa Jamilah mapema sana hivyo akakoleza chumvi na ndani ya muda mfupi mwanadada yule akawa anahisi kama yupo dunia nyingine.
“Samahani sana Jamilah,”
Tony akasema japo kwa hali aliyokuwa nayo Jamilah muda huo akuelewa kitu, Tony akatumia nafasi hiyo kutimiza matakwa ya mwili wake.

****************

Asubuhi na mapema Tony akaamka baada ya kuchangamsha mwili kwa mazoezi mepesi na kuweka mwili safi bafuni akaingia jikoni walau kuandaa kifungua kinywa kwa ajili ya mgeni wake ambaye hadi muda huo alikuwa bado amelala. Wakati Tony yupo jikoni simu yake ikawa inaita na mlio wa simu ukasababisha Jamilah aamke, akaiangalia ile simu akakuta Jina ni Tedy, akaiacha hadi ikakata, baada ya muda mfupi ukaingia ujumbe mfupi,
“Hello mpenzi! Bado umelala tuu”.

Ujumbe ule ukamshtua sana Jamilah, uvumilivu ukamshinda akaamua apekue zaidi simu ya Tony ili kujua zaidi habari za huyo Tedy, wakati akiendelea kupekua ukaingia ujumbe mwingine mfupi toka kwa Vanessa,
“Jamani bae, toka jana umenichunia shida nini, alafu mwenzio nimekumiss sana nataka nije kwako leo”

Jamilah akahisi kama anaota vile hakuamini yale aliyoyashuhudia, ikabidi ajifinye ili aone kama alikuwa ndotoni au la, japo hiyo haikubadili ukweli juu ya aliyoyashuhudia, akajikuta akitokwa na machozi kama mtoto mdogo,
“Siamini kama penzi langu la kwanza laweza kuwa chungu kiasi hiki, kwanini nimekuwa mpumbavu kumuamini mtu kirahisi hivi, kumbe hivi ndivyo maumivu ya mapenzi yalivyo,” aliendelea kusema Jamilah huku akilia, hakika hakuwa na nguvu hata ya kutoka pale kitandani hakutaka kuyakubali yale anayoyashuhudia.

Tony akamaliza kuandaa kifungua kinywa na akaingia chumbani kumuita Jamilah akaribie mezani, alipoingia hakika naye alishikwa na bumbuazi. Alikuta Jamilah akilia mithiri ya mtu aliyepata msiba wa mtu wake wa karibu, akasogea kujua kulikoni lakini Jamilah hakuongea kitu zaidi ya kumpa ile simu. Tony akaishiwa nguvu akajua tayari amesababisha ajali, Jamilah akamkunja Tony na kumpiga piga kifuani,
“Kwanini umenifanyia hivi Tony, katika siku yangu ya kwanza ya kujuana na mwanaume wewe umenifanyia ukatili huu, hakika sitokusamehe,” Jamilah akaongea kwa uchungu mno.
“Kwani nimekufanyia kipi kibaya?” Tony akauliza.
“Kwanini umenilaghai na kunifanya nikupende hadi kufikia hatua ya kulala na wewe wakati una mpenzi mwingine mbaya zaidi sio mmoja wawili Tony”
“Mhmh! Jamilah sasa mimi kuwa na wapenzi inahusiana nini na kilichotokea kati yetu?”
“Kwa iyo unanifanya mimi mtoto kunichanganya na wanawake wengine”
“Binafsi sikumbuki kama ulishawahi kuniuliza kama nina mpenzi au la, pia katika kinywa changu sijawahi kutamka neno nakupenda kwako”
“Tony..!”
Jamilah alijikuta akikosa neno la kuzungumza, hakuamini kama Tony angeweza kucheza na akili yake kiasi kile.
“Twende tukapate kifungua kinywa,” Tony alisema.
Jamilah akamuangalia Tony kwa hasira sana, hakujua nini afanye Zaidi ya machozi kumbubujika, hakuwa na nguvu hata ya kuinuka pale kitandani,
“Tony niambie kuwa niliyoyaona na niliyoyasikia kuwa si kweli”
“Unataka nikuambie nini Jamilah?”
“Niambie kuwa unanipenda na utaachana na hao wapenzi wako”
“Hahahahahahaha! You can’t be seriously! How could I do that? (Unamasihara wewe! Nawezaje kufanya hivyo)”
Jamilah akanyanyuka kitandani bila kusema neno, akaingia bafuni na baada ya kumaliza kuoga akavaa nguo zake na kuondoka lakini kabla hajatoka akageuka na kumtazama Tony kisha akamwambia,
“Usihisahau hii siku ipo siku utailipia, nitayafanya maisha yako kuwa ya shida Zaidi”

Tony alicheka sana aliposikia kauli ile, akamsogelea na kumshika kiuno, Jamilah akasogea nyuma na kumsukuma Tony, lakini jamaa alionekana kuwa imara kwani hakuweza kutikisika. Akamtazama Jamilah machoni na kumwambia,
“Usiwe mjinga wa kusahau ubaya unaoufanya kwa mtu, ile siku uliyonidhalilisha kwa ajali ndogo ya gari lako, niliumia sana na niliapa nitafanya lolote kukupata sasa uko mikononi mwangu huna la kufanya. Nilikwambia kamwe usisahau ile siku ila kwakuwa siku zote wanawake mnaongozwa na hisia kwanza bila kufikiria Zaidi, nikakutega ukategeka kwa hiyo bila bila nenda tu na usifikirie kunitafuta tena”.
Baada ya maneno hayo mazito akamuachia Jamilah ambaye kwa kiasi kikubwa aliduwaa huku machozi tuu yakimtoka, kiburi chake kimemuingiza pabaya.

********************

Baada ya kuwa na mafanikio makubwa kama balozi wa kampuni ya Kikorea Martha akawa ni miongoni mwa wasichana ambao habari zao kila siku zinatangazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Wanaume wengi walitamani kuwa na mwanamke mwenye sifa kama alizonazo Martha, achilia mbali uzuri na urembo wake linapokuja swala la kazi Martha ni mtu anayependa kuwajibika kwa wakati na kuhakikisha kila kitu kimeenda kama kilivyopangwa. Wanaume wachache waliopata bahati ya kuwa karibu na mrembo huyo walishindwa kuzuia hisia zao na kila mmoja akijaribu kutupa karata yake kwa wakati wake. Kati ya wote hao hakuna hata mmoja aliyebahatika kuusimamisha moyo wa msichana yule.

Joseph huyu ni mmoja kati ya vijana wachache waliojaliwa stara na wenye mafanikio makubwa, hakuwahi kuwa katika mausihano ya kimapenzi na alijenga Imani kuwa hamna mapenzi ya kweli duniani, lakini toka amefahamiana na Martha taratibu mawazo yale yakaanza kufutika na akajikuta akivutiwa sana na msichana yule. Kutokana na kufanya kazi katika kitengo kimoja wakajikuta wakiwa karibu Zaidi hasa baada ya kupewa kazi ya kuandaa Makala itakayoonesha utamaduni wa watu wa pwani hasa wale waishio Tanga.

Iliwalazimu kufanya kazi mchana na usiku kuandaa mpango kazi, jinsi ya kuanza hadi utakapoishia, Jospeh alijisikia furaha sana kuwa na mwanadada yule ambaye muda wote aliwaza kazi tuu,
“Martha naweza kukuliza jambo?” alisema Jose.
“Uliza tuu!”
“Umekuwa bize sana na kazi! Nawaza huyo shemeji yangu anapata muda gani nawe?”
“Hahahahahaha! Kwanini umeuliza?”
“Nimeuliza tuu maana inaitaji moyo”
“Kwani wewe mkeo akiwa bize hivi utafanyaje?”
“Binafsi siwezi kusema kitu kwasababu sijawahi kuwa nae”
“Ooh! Real? (Kweli?)”
“Ndio”
“What are you waiting for? (Unasubili nini?)
“Namsubiri yule atakayeufanya moyo wangu kusimama walau kwa dakika na kuacha kufikiria yote na kumuwaza yeye tuu”
“Keep on praying u will find her soon, (endelea kuomba utampata hivi karibuni)”
“Thanks for your advice (akhsante kwa ushauri wako)”
“Your welcome, (karibu)”
“Lakini bado hujanibu swali langu”
“Ooh! Ukweli kwamba sina muda na mapenzi kwa sasa, moyo wangu upo kwenye kazi yangu, hivyo tuu Jose”
“Mhmhmh! Haya”

Jose alijikuta akikatishwa tamaa na jibu alilopewa na Martha aliwaza Zaidi afanye nini walau mrembo yule arudishe hisia za mapenzi japo hakuwa anajua historia yake ya nyuma iko vipi, akajiuliza Zaidi je mrembo yule alishawahi kuwa kwenye mapenzi nini kilimtokea hadi leo kusema kuwa hana muda na mapenzi, kama hakuwai kuwa kwanini aogope kuingia katika ulimwengu huo wa huba.
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 7
+255 713 373731


ILIPOISHIA………
Jose alijikuta akikatishwa tamaa na jibu alilopewa na Martha aliwaza Zaidi afanye nini walau mrembo yule arudishe hisia za mapenzi japo hakuwa anajua historia yake ya nyuma iko vipi, akajiuliza Zaidi je mrembo yule alishawahi kuwa kwenye mapenzi nini kilimtokea hadi leo kusema kuwa hana muda na mapenzi, kama hakuwai kuwa kwanini aogope kuingia katika ulimwengu huo wa huba.

Tuendelee…………

Baada ya mipango yote kukamilika, wafanyakazi wote wakiongozwa na Martha wakaanza safari ya kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya kuandaa Makala itakayoonesha utamaduni wa mkoa huo ambao kwa hakika unasifika kwa mahaba.
“Sasa jamani nani ataongoza upigwaji wa picha maana Tony simuoni!” aliuliza Jose.
“Mimi nitaongoza,” Martha akajibu.
“Hiyo si sawa,” akasema Jose.
“Kwanini?”
“Umekuwa ukifanya kazi nyingi zinazomuhusu Tony, kwa nini azembee kiasi hiki hata kama yeye ni mkurugenzi lazima hawajibike sehemu yake,” aliongea Jose.
“Lakini alichosema Jose ni kweli, yeye ni muongozaji na anajua kila kitu kuhusiana na hii safari sasa kwanini hasiwepo,” alisema mfanyakazi mwengine.
“Jamani tuachane na hayo kila mtu achukulie hii safari kama sehemu ya kutuliza akili mbali na kazi inayotupeleka, tujitahidi kufanya vizuri bila kujali mtu flani hayupo”
Ikabidi wote wakubaliane na Martha japo kishingo upande, maswali mengi yakazuka vichwani, inakuaje mkurugenzi amtete Tony kwenye maswala ya uwajibikaji au kuna mambo yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo wao hawayajui.

**************************

Safari ya kuelekea jijini Tanga ikaanza huku wote wakiamini kuwa Tony anaingiza maswala ya kibinafsi kwenye kazi, sababu mara nyingi walishuhudia wakurugenzi hao wawili wakitofautiana kimitazamo na utendaji pia, japo wote walikuwa na nia moja ya kufanya kampuni kukua na kuingiza faida maradufu.
Safari ilikua nzuri na yenye kuburudisha sana, wengi wao ilikuwa mara ya kwanza kwenda mkoa huo hivyo kwao ilikuwa kama kufanya utalii wa ndani,
“Samahani bosi sijajua tunafikia wapi?” aliuliza Jose.
“Tanga beach resort,” alijibu Martha.
“Aah! Sasa kwani uliwapa taarifa mapema?”
“Hilo ni jukumu la Tony”
“Sasa Tony mwenyewe hakuja tutafanyaje!”
“Usijali! Tutajua tukifika”

***************************

Wakati msafara wa wafanyakazi ukikaribia kabisa kuingia jijini Tanga, Tony alifika mapema sana na akawa ashafanya mipango yote ya hotelini. Tony toka amefika hotelini hapo hakutulia sehemu moja, uwepo wa warembo wengi eneo hilo ulimfanya ajihisi yupo paradiso ndogo,
“Braza eenh! Naona huku mambo sio mabaya,” alisema Tony baada ya kusogea katika kibanda cha mlinzi wa getini ambaye alikuwa zamu kwa wakati huo.
“Kwanini?”
“Braza! Huku kuna warembo kama wameshushwa hivi”
“Hahahahaha! Hii ndio Tanga sasa”
“Daah! Braza wee acha tuu nahisi mtaji wangu wa kuuza matunda nitaufirisi huku”
“Hahahahaha! Angalia utakosa hata nauli ya kurudi Dar”
“Ila broo kwani sehemu nyingine zipi ambazo kuna watoto wakali kama hawa na kumechangamka sana tofauti na hapa?” aliuliza Tony.
“Mhmhmh! Sehemu zilizochangamka ni nyingi kama utaenda Usagara, Chumbageni au kule Raskazone ndio balaa maeneo ya ufukwe nini unaweza kusahau kabisa kurudi kwenu, alafu watoto wakule wanajua mahaba kweli,” alijibu Mlinzi.
“Duuh! Broo uko vizuri kona zote unazijua”
“Hahahahaha! Kawaida tuu”
“Hivi broo umeoa kweli maana daah si mchezo”
“Hahahahahaha! Unafurahisha sana dogo na maswali yako, ukweli mimi nina mke na mtoto mmoja wa kiume, lakini si unajua tena kila siku uwezi kula mboga moja lazima ubadirishe kesho nyama, kesho kutwa maharage japo vyote ni protini” alisema Mlinzi.

Tony alijikuta akijenga Urafiki na Mlinzi yule ndani ya muda mfupi sana, sababu walionekana wote kupenda vitu vinavyofanana. Walizungumza vitu vingi sana, hii ikamsaidia Tony kujua picha nzima ya mkoa huo japo kwa uchache.
Tony akarudi sehemu ya beach na kupunga upepo wa eneo lile, hakuacha kusifia uumbaji wa Mungu kwa hakika alishuhudia warembo walioumbwa wakaumbika, alijisikia furaha sana moyoni mwake.

“Sasa huu si mtihani hata sijui nimsemeshe yupi kati ya hawa, kila mtu ni mzuri na ana kitu cha utofauti ambacho mwenzake hana,” alisema Tony kwa sauti ya chini ambayo haikusikika na yeyote yule.

Baada ya muda mfupi wafanya kazi wenzake wakawa wamefika hotelini Pale, Tony alipigiwa simu baada ya wao kuambiwa kuwa tayari kuna mtu aliyewaandalia sehemu ya kufikia. Tony akawafata na kuwakaribisha kwa tabasamu zito, tabasamu lile likakata hasa baada ya macho yake kukutana na ya Martha. Wawili hao wanasiri nzito sana ambayo kila mtu hataki kuikumbuka na ndio maana mara zote wanazokuwa karibu mmoja wao anajikuta akishindwa kuuficha ule mfukuto wa moyo.
“Daah! Sisi tulijua ndio umetuacha kwenye mataa,” alisema Jose.
“Nadhani unanifahamu vizuri linapokuja swala la kazi masihara uwa naweka pembeni”
“Maana kila tukikutazamia hukutokea kumbe mwenzetu umetuwahi huku au ndio vile nini!”
“Hahahah! Kama kawaida si unajua jiji la mahaba hili,” alisema Tony.
“Kwa hiyo ushachukua namba za wangapi?” Jose aliendelea kuuliza,
“Wengi tuu!”
“Jamani mtaongea mambo yenu mkiwa wenyewe tupo kwa ajili ya kazi, tuambie umechukua vyumba vingapi?” alisema Martha.
“Vyumba 6 tuu”
“Nini! Tunawezaje kulala kwenye vyumba 6 wakati sisi tupo 12?”
“Tutalala wawili wawili”
“No thanks! Siwezi kulala na mtu naomba uongeze vyumba”
Kauli ile ilimfanya Tony ajisikie vibaya mno kwani hakupenda pesa nyingi itumike kwa ajili ya malazi wakati pesa ile inaweza ikagaiwa kwa wafanyakazi kwa ajili ya kuwaongezea pesa za kujikimu kwa kipindi ambacho watakuwepo katika jiji hilo. Akawaangalia wafanyakazi wengine na kuwauliza,
“Na ninyi mnasemaje?”

Wote wakaunga mkono kauli ya Martha, hivyo Tony akapiga simu mapokezi na baada ya muda mfupi mhudumu akafika akiwa na funguo nyingine 6. Martha na Tony wakakosa vyumba upande ule ikabidi waende ghorofa moja Zaidi na huko wakapata vyumba ambavyo milango yao ikawa inatazamana.
“Samahani mhudumu! Siwezi kupata chumba tofauti na hiki?” alisema Tony.
“Hapana kaka yangu vyumba vya hadhi yenu ni hivi tuu na vingine vyote vinawatu si unajua tena msimu wa sikukuu huu,” alisema Mhudumu.
“Sawa akhsante”
“Mkiwa na shida yeyote mtapiga simu mapokezi”

Mhudumu akaondoka na kuwaacha Tony na Martha wakiingia vyumbani mwao kila mmoja. Katika ulimwengu huu wakidigitali mambo mengi hufanyika kwa njia ya mtandao, hii ikampa fursa Martha ya kutoa taarifa ya kikao kitakachofanyika jioni ya siku hiyo. Wafanya kazi wote wakaipata taarifa hiyo sababu kampuni hiyo ilihakikisha wafanyakazi wake wote wanakua na simu zenye uwezo wa internet hii imerahisisha kwa kiasi kikubwa ufikiwaji wa taarifa za dharula kwa wafanya kazi wote.
Tony alipohakikisha kuwa kila mmoja yupo katika chumba chake, hakuwa na kazi tena kwa wakati huo kama kawaida yake ikabidi ashuke kwa swahiba wake wa Muda mfupi ambaye ni mfanyakazi katika hoteli hiyo kama mlinzi.
“Braza nimerudi tena!”
“Aah! Karibu asee tupo tunavuta masaa tuu hapa”
“Sasa broo mi shida yangu unielekeze huko Raskazone maana vya kuadithiwa sitaki nataka nikathibitishe kwa macho yangu”
“Hahaha! Kumbe unamaanisha kweli, ila mbona msafara wenu unawarembo tuu tena kama yule sijui ni meneja sijui nani asee acha tuu”
“Aaah! Wale kila siku nawaona nataka sura mpya”
“Poa basi kuna tax apo nje pia kuna bajaji mbele kidogo, hivyo uamuzi wako juu ya usafiri wa kuutumia ukiwatajia jina la Raskazone hamna hasiyepafahamu”
“Poa broo shukrani”
“Karibu tena!”
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 8
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Tony alipohakikisha kuwa kila mmoja yupo katika chumba chake, hakuwa na kazi tena kwa wakati huo kama kawaida yake ikabidi ashuke kwa swahiba wake wa Muda mfupi ambaye ni mfanyakazi katika hoteli hiyo kama mlinzi.
“Braza nimerudi tena!”
“Aah! Karibu asee tupo tunavuta masaa tuu hapa”
“Sasa broo mi shida yangu unielekeze huko Raskazone maana vya kuadithiwa sitaki nataka nikathibitishe kwa macho yangu”
“Hahaha! Kumbe unamaanisha kweli, ila mbona msafara wenu unawarembo tuu tena kama yule sijui ni meneja sijui nani asee acha tuu”
“Aaah! Wale kila siku nawaona nataka sura mpya”
“Poa basi kuna tax apo nje pia kuna bajaji mbele kidogo, hivyo uamuzi wako juu ya usafiri wa kuutumia ukiwatajia jina la Raskazone hamna hasiyepafahamu”
“Poa broo shukrani”
“Karibu tena!”

Tuendelee…………

Tony akatoka tayari kwa safari ya huko Raskazone, akasogea zilipo Tax na kuanza kumpa dereva maelekezo,
“Huko napafahamu vizuri, usiwe na shaka,” alisema dereva wa tax.
“Sasa inakuwa shilingi ngapi?”
Kabla dereva hajajibu simu ya Tony ikaita, kuangalia akakuta ni namba ngeni ikabidi haipokee,
“Uko wapi kuna vitu tunahitaji kuviweka sawa kabla ya kikao cha jioni,” ilisema sauti ya upande wa pili.
Tony akaisikiliza vizuri na kugundua kuwa ni Sauti ya Martha mwanamke ambaye kiukweli hakupenda kuwa karibu naye hata kidogo.
“Samahani siwezi kuja nimetoka sipo Hotelini,” alijibu Tony.
“Ulisema linapokuja swala la kazi, masihara unaweka pembeni, sasa nini hiki ambacho unaniambia. Mimi nawe tu wakurugenzi na kabla ya kukaa na wenzetu jioni lazima tukutane tuwe na mipango inayoshabihiana,” alisema Martha.

Tony akamsikiliza mrembo yule kwa makini kisha akaamua kuvunja safari yake na kurejea hotelini ambapo akapanga akutane na Martha katika fukwe iliyopo hotelini hapo. Haikuchukua muda wawili hao kukutana tayari wakaka na kuanza kujadili mpango kazi.
“Makala yetu lazima ioneshe utamaduni, vivutio vya asili na sehemu za kihistoria katika mkoa huu, hivyo nafikilia tufanye maojiano na hawa waongozaji wanaokuwa katika sehemu hizi za kihistoria awe anasimulia na sisi tunamrekodi,” alisema Martha.
“Wazo zuri lakini mimi ninafikiri tofauti kidogo” alisema Tony baada ya kumsikiliza Martha kwa makini mno.
“Wewe unataka iweje?”
“Mimi naona tusimrekodi huyo muongozaji badala yako tuchukue clip za sehemu tunazozitaka alafu wengine wafanye kazi ya kuchukua historia ya hizo sehemu kisha, tutaingia studio na kutengeneza audio zenye kuelezea hayo maeneo tutakuja kuzichanganya na hizo picha”.
Martha hakuwa na la kupinga juu ya wazo lile, akamuunga mkono Tony kwa asilimia zote,
“Sawa nadhani tumemaliza tutaonana jioni,” alisema Tony.
Wakati wawili hao wakiongea kwa mbali Jose akawa anaangalia, akaanza kuhisi wivu na kwa kuwa alimjua vyema Tony kuwa huwa afanyi makosa akiachwa karibu na msichana sio yeyote ila mrembo ndio kigezo kikubwa. Jose akahisi kuwa endapo ukaribu huo utazidi basi ni wazi hatoweza kumpata Martha mwanamke ambaye alitokea kumpenda kwa muda mrefu toka alipotua nchini ila akakosa tuu ujasiri wa kuelezea hisia zake.
“Nina nini Mimi? Mbona moyo wangu unaenda kasi kuliko kawaida, je nina hisia zozote juu ya mrembo huyu, ooh! Tony kwa wengine wote sawa ila kwa huyu hapana,” alisema Tony moyoni huku bado akimtazama Martha.

Martha akagundua kuwa Tony anamtazama kwa macho ambayo hayakuwa ya kawaida na yaliyojaa maswali mengi. Wakati akiendelea kutafakari yale Jose akafika na kuingilia maongezi,
“Vipi mabosi mna kikao au!”
Tony akamtazama Jose kisha akachukua tarakishi (laptop) yake na kuinuka,
“Hapana tushamaliza! Karibu upige stori na bosi mimi ngoja niende misele”
“Mhmhmhm! Ushampata nini wa kuzuga naye”
“Bado ndio naenda kumsaka,” alisema Tony na kuondoka.
“Hivi kwa nini mnapenda sana kuongea habari hizo kila mkikutana?” aliuliza Martha.
“Tofauti na kazi ndicho kitu ambacho Tony anakipenda,” alijibu Jose.
Martha akamtazama sana Jose, ambaye alikuja na sura ya tofauti kidogo na siku zote.
“Tony ni mlaghai sana katika mapenzi nimeshuhudia wasichana wengi wakilia kwa sababu yake”
“Kwanini unaniambia haya?” Martha akauliza.
“Sitaki yakukute kama yaliyowakuta wao”
“Jose! Do you think am cheap eenh!, (Jose! unahisi kuwa mimi ni mrahisi hivyo!)”
“Hapana ila ni kama tahadhari tuu”
“Kuna vitu vingi ambavyo wewe huvijui kuhusu Tony, kwa hiyo ni afadhali tukaacha kumzungumzia yeye, Je! Unalingine la kusema nahitaji kwenda kupumzika!”
“Martha kuna kitu naomba tuzungumze kwa kirefu zaidi”
“Ya kiofisi au binafsi?”
“Binafsi tuu”
“Naomba unitafute baada ya kikao sababu akili zangu kwa sasa zipo kwa ajili ya hiko”
“Sawa bosi”

Kadri ya muda ulivyozidi kwenda ndivyo Jose akajenga ujasiri wa kutaka kuelezea hisia zake kwa bosi wake japo ni mkubwa kikazi lakini mapenzi hayaangalii matabaka. Aliweka Imani kuwa ipo siku mrembo yule atamuelewa japo hakujua ni wakati upi hasa. Tony alionekana kuwa tishio kidogo katika harakati zake za kumpata Martha japo hawakugombana ila taratibu akajikuta akijenga chuki moyoni mwake.
Muda wa kikao ukawadia kila mmoja akachukua nafasi yake kusikiliza kile walichoitiwa, Martha akawa wakwanza kuzungumza,
“Jamani leo ni jumatatu, mategemeo yetu kuimaliza hii kazi ijumaa mapema walau mpate nafasi ya kuburudika, safari ya kurudi Dar es salaam itakuwa jumapili na jumatatu ofisini kama kawaida. Kikubwa naomba tushirikiane na kujituma katika hili,” alisema Martha kisha akampa Tony nafasi ya kuongea.
“Tumekuwa marafiki sana lakini hiyo isiwe sababu ya kuweka ulegevu katika kazi, kesho ndio tunaanza rasmi hivyo majukumu ya kila mtu yapo katika faili ambayo muda si mrefu nitatuma kwenye anuani ya barua pepe zenu. Hatutofanya mahojiano kama ilivyokuwa awali ila sasa hivi jitahidi kuandika kila tukio kwa usahihi na mimi nitajitahidi kupata kila picha, baadaye tutaingia studio na kuingiza sauti kisha kazi yetu itakuwa imekamilika,” alisema Tony.

Maongezi yalikuwa ya kirefu Zaidi kila mmoja alikumbushiwa majukumu yake, hari ya kazi ikajaa mioyoni mwao. Mambo yakawa tofauti kidogo kwa Joseph ambaye tayari alisharuhusu hisia za mapenzi zitawale akili yake muda wote alimtazama Martha bila kuzingatia kile kilichokuwa kikizungumzwa,
“Leo lazima nimueleze hisia zangu, siwezi kusubili hata kidogo,” alisema Jose.
Kikao kikafungwa kwa wote kupata chakula cha usiku, wengi walionekana kuufurahia msosi huo kwa kiasi kikubwa.
“Jamani eenh! Mimi ngoja nikacheze buzuki kidogo, kama mjuavyo napenda sana muziki kwa hiyo nyie endeleeni tuu,” alisema Tony na kuanza kuondoka.
“Mhmhmh! Kama kawaida yako wee nenda, tushakuzoea,” alisema Jose.

Tony alijivuta hadi eneo la muziki, akakuta watu wa kila namna wakisakata rhumba, baada ya muda Dj akabadili muziki na kuweka ule wa taratibu, asilimia kubwa ya waliobaki uwanjani walikuwa wawili wawili. Tony akawaza ni namna gani ataucheza mziki ule akakosa jibu, akili ikamtuma atafute mtu wa kucheza naye, akatazama huku na huko kwa mbali akamuona msichana mrembo akiwa amekaa peke yake akinywa mvinyo. Ikabidi atumie dakika kadhaa kuhakikisha kama yule msichana yuko peke yake au yupo na mtu, dakika 5 zikapita bila mtu yeyote kusogea eneo lile. Tony akatumia fursa hiyo bila kupoteza muda,
“Excuse me miss! May I join you? (Samahani! Naweza ungana nawe?),” alisema Tony.
Mrembo yule alitumia sekunde kadhaa kumtazama Tony kabla ya kujibu, alishangazwa na tabasamu zito aliloichia kijana yule. Akajikuta akivutika Zaidi kutaka kujua nini Tony anataka kusema,
“Ofcourse yes! (bila shaka ndio!),” alijibu yule msichana.
Tony akasogeza kiti na kukaa, akamuita mhudumu na kuagiza kinywaji kisha akafungua maongezi na msichana yule,
“Umekuja mwenyewe au uko na mtu?”
“Nimekuja na rafiki yangu, ambaye ni yule aliyevaa blauzi ya pinki,” alisema msichana yule huku akimuonesha Tony sehemu ambayo watu wanacheza muziki.
“Sasa mbona wewe huendi kucheza?”
“Mhmhmh! Sina ujasiri wa kucheza mbele za watu”
“Kwanini?”
“Basi tuu sijazoea”
“Unaonaje ukizoea kuanzia leo”
“What do you mean? (Unamaana gani)”
“May i dance with you? (Naweza kucheza nawe?)”
“No thanks!, (hapana!)
“Usikatae tafadhali! Nahisi upweke kidogo walau twende tukacheze kidogo na nafikiri tutazidi kufahamiana kadri ya muda unavyoenda”
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 9
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Tony akasogeza kiti na kukaa, akamuita mhudumu na kuagiza kinywaji kisha akafungua maongezi na msichana yule,
“Umekuja mwenyewe au uko na mtu?”
“Nimekuja na rafiki yangu, ambaye ni yule aliyevaa blauzi ya pinki,” alisema msichana yule huku akimuonesha Tony sehemu ambayo watu wanacheza muziki.
“Sasa mbona wewe huendi kucheza?”
“Mhmhmh! Sina ujasiri wa kucheza mbele za watu”
“Kwanini?”
“Basi tuu sijazoea”
“Unaonaje ukizoea kuanzia leo”
“What do you mean? (Unamaana gani)”
“May i dance with you? (Naweza kucheza nawe?)”
“No thanks!, (hapana!)
“Usikatae tafadhali! Nahisi upweke kidogo walau twende tukacheze kidogo na nafikiri tutazidi kufahamiana kadri ya muda unavyoenda”

Tuendelee…………

Msichana yule akafikiri kidogo, kisha akaongeza mvinyo wake kwenye bilauri na kunywa kwa haraka, alipomaliza akasimama na kumwambia,
“Twende!”
Tony hakuamini kama ingekuwa rahisi kwa msichana yule kukubali, akajenga Imani kuwa kama amekubali kucheza naye hayo mengine hawezi kuchomoa hata iweje.

**********

“Jamani nyie hivi kazi kweli itafanyika kesho, maana director wetu ni balaa, mwangalieni kule,” alisema mmoja wa wasichana ambao wanafanya kazi katika kampuni ambayo Martha ndiye meneja.
“Aaah! Yule jamaa ni kumbakumba asee, alafu kama mchawi vile yeye ananasa warembo tuu,” alisema Jose kwa sauti kidogo ambayo ilimfanya Martha naye kusikia.
Martha akatazama alipo Tony, akakuta amemshika msichana yule ambaye wote hawakumfahamu, kwa mbwembwe za Dj taratibu walionekana kuufurahia muziki ule.
“Bosi eenh! Muda umeenda sana, na nidhamu ya kazi ni bora Zaidi, kamwambie Tony akapumzike asije tukwamisha kazi kesho,” Jose alisema.
“Mwacheni sie tuondokeni,” alijibu Martha.

Mabadiriko yale yaliwashtua wengi kidogo, wakashangaa kwa nini bosi wao huyo muda mfupi uliopita alikuwa akicheka na kufurahi, sasa amekasirika na kuondoka kama amegombana na mtu.
“Nyie sio bure mjue! Nahisi bosi Martha anampenda Tony”
“Nini! Acha kuongea vitu usivyovielewa wewe,” alisema Jose.
“ila hata mimi nahisi hivyo maana mara nyingi Martha anaonekana kumtetea sana Tony na tukianza kuongelea habari za Tony kuwa na wanawake wengi tunamuona wazi kama anaumia hivi japo hataki kuweka wazi maumivu yake, mfano mdogo ni sasa hivi,” alisema Bosco ambaye naye pia ni mfanyakazi wa kampuni ila yeye yupo katika kitengo cha kuseti mwanga.

“Martha hawezi kumpenda mtu kama yule,” alikazia Jose.
“Mhmhmh! Vipi ndugu mbona kama unatetea sana au nawe tayari ushamzimia bosi,” alisema Bosco.
“Ilo alikuhusu,” alijibu Jose na kuondoka.
“Jamani eenh! Huyo ndiyo Tony asije fanya tukazidi kukosana wenyewe kwa wenyewe, hata hivyo ana uhuru wa kufanya hivyo, nadhani itakuwa busara kama sisi sote tukaenda kupumzika na akili zetu tuziweke kwa ajili ya kazi kesho,” alisema Bosco.
Kila mmoja akakubaliana na shauri la Boso, bila kupoteza muda wakaelekea vyumbani mwao tayari kwa kupumzisha akili na miili yao.

*****************

“Japo tumecheza kwa takribani dakika 20 sasa lakini sijalifahamu jina lako,” alisema Tony kwa sauti ya chini.
“Ooh! Ni kweli nimenogewa na muziki kiasi cha kujisahau, mimi naitwa Leilah”
“Ooh! Leilah sina wasiwasi na jina lako, maana linalandana sawia na uzuri Mungu aliokujalia, mimi naitwa Tony”
“Jamani hata wewe una jina zuri”
Maongezi ya hapa na pale yakaendelea huku wakisindikizwa na muziki wa taratibu ambao kwa hakika uliwafanya wajisahau. Kadri muda ulivyozidi kwenda ndipo hisia za kila mtu zikaanza kubadirika, Leilah akaligundua hilo akaomba kwenda kupumzika. Tony bila hiyana akaridhia,
“Tony I have to go, am out of time, (Tony acha niende muda umekimbia sana)”.
“Owky! Can I have your phone number? (Sawa! Je naweza kupata namba yako?)”.
“No need of it! We shall meet if we destinied to, (haina haja, tutaonana Mungu akipenda)”.

Tony hakutegemea jibu lile toka kwa msichana yule, akafikiri kama atakuwa amekosea mahali lakini hakupata jibu, na kwake ilikuwa mara ya kwanza kujibiwa vile.
“Kweli haina haja! Je naweza kukusindikiza?”
“Haina haja pia rafiki yangu ametangulia na ananisubili”
“Sawa ukikaribia kwa rafiki yako nitakuacha uende”
Leilah hakuongea kitu Zaidi ya kupiga hatua ndefu kuelekea sehemu yalipo magari, kabla hajafika Zaidi akasimama na kumtazama Tony,
“Naomba tuishie hapa! Sihitaji rafiki yangu akuone!”
Tony hakuongea kitu Zaidi ya kumvuta mrembo yule karibu yake, akahakikisha hakuna umbali wowote kati yao,
“Unataka kufanya nini?” aliuliza Leilah.
“Je uwezi kunyamaza na kutulia walau kwa dakika mbili?”
“Hapana! Mwenzangu ananisubili isitoshe muda umeenda sana”
“Stay calm, I promise to let you go after few seconds, (Tulia, nitakuacha uende baada ya sekunde kadhaa),” alisema Tony.

Leilah akafurukuta kutaka kujinasua mikononi mwa mwanaume yule lakini alishindwa akajikuta akikubali kutulia kwa muda huo. Tony hakumfanya lolote msichana yule Zaidi ya kumkumbatia na kumtazama usoni kwa macho yenye uhitaji. Leilah naye akamtazama Tony kwa macho malegevu,
“Sihitaji namba yako wala sitotaka kukuona tena, kama sekunde hizi chache zitaisha hivi hivi,” alisema Tony.
Mapigo ya moyo yakamuenda mbio sana Leilah akajikuta katika wakati mgumu wa kushindana na nafsi yake. Akahisi kuvutiwa Zaidi na kijana yule, machozi ya kushindwa yakaanza kutiririka mashavuni mwake. Akaiunua mikono yake na kulikubali kumbatio lile la Tony, ndani ya dakika mbili tuu hakuna aliyeelewa nini kimetokea Zaidi ya kujikuta wakiwa katika hali nzito ya ndimi zao kuungana. muda waliopanga ukaisha Leilah hakushtuka wala hakutamani kumuachia tena Tony. Tony alifanikiwa Kwa kiasi kikubwa kucheza na akili ya Leilah hadi kuugundua udhaifu wake, wakati wakiendelea kukisi ghafla rafiki yake na Leilah akawakuta katika hali ile. Rafiki yule hakuliamini hilo hata kidogo, ikabidi aangushe chupa ili kuwashtua na hapo ndipo akili ikamrejea Leilah. Akajikuta akilia Zaidi na kukimbia, hakutamani kumtazama Tony usoni. Tony akabaki ameduwaa yule rafiki wa Leilah akamsogelea Tony na kumwambia,

“Leilah ni mke wa mtu, anampenda sana mume wake, hana muda mrefu toka aolewe na hakuwahi kufikilia kumsaliti mumewe hata siku moja, mimi nimebeba dhamana ya kuja huku baada ya mumewe kusafiri kikazi. Kwa hiyo tafadhali naomba ukae mbali naye acha kuuyumbisha msimamo wa Leilah”.
Kauli ile ikawa kama amemwagiwa maji ya baridi, pamoja na kuchezea wasichana ila hakuwahi kufikiri kufanya ukatili huo kwa mke wa mtu, kwa mara ya kwanza Tony akajihsi mkosaji,
“Sawa nimekuelewa dada yangu hili alitotokea tena”.
Tony alijibu na kuondoka eneo lile, huku akili yake bado haikukaa sawa, akashindwa kuamini ukweli wa mambo kuwa Leilah ni mke wa mtu maana ndani ya muda mfupi ule alijihisi kuwa yupo sayari nyingine, akatamani kulipata penzi la Leilah.
Huku nyuma Leilah naye hakuamini kilichotokea muda mfupi uliopita, akawa analitaja jina la mumewe huku akiomba msamaha.

“Usijali rafiki yangu hayo mambo huwa yanatokea, nitakutunzia hii siri,” alisema rafiki yake Leilah.
“Najua wajua kiasi gani mume wangu ananipenda name nampenda ila kilichotokea kwa kweli hata sielewi yaani”
“Basi yameisha hayo kikubwa ni kuwa makini siku nyingine”

*********************

Usiku ukapita na siku nyingine ikaanza, watu wote wakakusanyika tayari kwa kwenda kazini isipokuwa Tony pekee,
“Mmeona kile nilichosema jana, huyu jamaa lazima atatuchelewesha tuu,” alisema Jose.
“Twendeni bhana anajua tunapoanzia,” alisema Bosco.
“Acheni papara muda tuliokubaliana ni saa 2 kamili na sasa ni saa 1.55, bado dakika 5 nzima tuvute subira kidogo,” alisema Martha.
Jose taratibu akaanza kusadiki maneno ya wafanyakazi wenzake kuwa Martha inawezekana akawa kweli anampenda Tony maana kila jambo haachi kumtetea. Kabla ya dakika 5 hazijaisha Tony akawa amefika eneo hilo, alionekana amepooza kidogo.
“Bila shaka kila mtu ni mzima, ni wakati wetu wa kuwajibika sasa akili zetu ziwe kwenye kazi,” alisema Tony.
Wote kwa pamoja wakaingia kwenye gari na safari ya kwenda amboni ikaanza, njiani wakaongea mengi juu ya mipango ya kazi. Lakini Tony hakuonekana kuwa sawa kabisa jambo lile liliwashtua wengi mno. Kila mmoja akatamani kujua nini hasa kinachomsibu.

Akili ya Tony kwa muda huo ilikuwa juu ya mrembo Leilah, mtoto wa kitanga ambaye kwa muda mfupi tuu tayari alishauyumbisha moyo wake. Tony mwanaume ambaye kiukweli hakuweza kumuacha mwanamke mzuri kama Leilah akikatiza mbele yake. Mtihani ni kwamba msichana yule tayari ni mke wa mtu hivyo ni hatari sana kama angelazimisha ukaribu.
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 10
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Wote kwa pamoja wakaingia kwenye gari na safari ya kwenda amboni ikaanza, njiani wakaongea mengi juu ya mipango ya kazi. Lakini Tony hakuonekana kuwa sawa kabisa jambo lile liliwashtua wengi mno. Kila mmoja akatamani kujua nini hasa kinachomsibu.
Akili ya Tony kwa muda huo ilikuwa juu ya mrembo Leilah, mtoto wa kitanga ambaye kwa muda mfupi tuu tayari alishauyumbisha moyo wake. Tony mwanaume ambaye kiukweli hakuweza kumuacha mwanamke mzuri kama Leilah akikatiza mbele yake. Mtihani ni kwamba msichana yule tayari ni mke wa mtu hivyo ni hatari sana kama angelazimisha ukaribu.

Tuendelee…………

Siku zikazidi kuyoyoma hatimaye kazi iliyowapeleka Tanga ikakamilika, ilikuwa ni siku ya ijumaa hivyo ikabidi wafanyakazi wapewe uhuru wa kufanya mambo yao binafsi.
“Jamani leo usiku tutafanya sherehe ya kupongezana kwa kazi nzuri tuliyoifanya hivyo kila mmoja akapumzike na saa 3 usiku tukutane tunapokutanaga siku zote,” alisema Martha.
Kila mmoja akausubili muda huo kwa hamu Zaidi lakini hali ikawa sio shwari kwa Tony, tamaa ya kumpata Leilah ikazidi kumuingia,
“Daah! Kwanini namuwaza sana msichana huyu, nitamuona wapi! Sijui anapokaa wala sina namba zake” alisema Tony kwa sauti ambayo hakuna mtu aliyeweza kuisikia.

*************

Muda uliokuwa ukisubiliwa ukawadia, wafanyakazi wote wakawa sehemu moja, keki maalumu ya kupongezana ikaandaliwa, Tony na Martha wakaikata keki ile na kuwarisha wafanyakazi wao. Hakika ilikuwa siku ya furaha mno, wakafungua shampeni na kila mmoja akamiminiwa baada ya hapo ukafata wasaa wakucheza muziki. Ilikuwa vituko katika uwanja wa muziki maana asilimia kubwa tayari walishalewa hawakufata stepu ila kila mmoja alicheza vile alivyoona inafaa.

Chakushangaza Zaidi Martha naye alikunywa pombe siku hiyo, alionekana akiwa mwenye furaha kuliko siku zote zile. Wakajikuta wote wakiwa chakali hakuna aliyeweza kumsaidia mwenzie, Tony akawa wa kwanza kuondoka eneo lile na kwenda chumbani kwake kupumzika. Alitembea kwa kupepesuka na alipofika moja kwa moja akajitupa kitandani, fikra zikaenda mbali akahisi kama vile yupo karibu na Leilah. Huku nyuma kila mmoja naye akajikokota kuelekea chumbani kwake, hali ilikuwa ngumu kwa Martha ambaye hakuzoea kunywa kilevi, alijitahidi kutembea hadi kufika juu hakuelewa chumba chake kipi, kila chumba alichogusa kilikuwa kigumu, akapapasa na kutoa funguo yake, hakukumbuka hata namba ya chumba chake. Akasogea katika chumba chake ila kila alipojaribu kufungua akashindwa akahisi labda amekosea, akageuka nyuma na kukisogelea chumba cha Tony alipogusa kitasa mlango ukafunguka. Bila kusita akaingia chumbani na kuufunga mlango, kisha naye moja kwa moja akapanda kitandani alipo Tony.

Tony aliendelea kuweweseka na kuhisi tayari Leilah amemkaribia pale kitandani, akajikuta akimkumbatia Martha bila kujua, Martha naye hakuwa anaelewa akajikuta anatoa ushirikiano kwa Tony. Muunganiko wa wawili hao ukafanya hali ya hewa nje kubadilika, radi ikapiga na upepo mkali mithili ya kimbunga ukawa unavuma,
“Hata kama wewe ni mke wa mtu lakini nimetokea kukupenda sana, naomba usiku huu usisahaulike vichwani mwetu,” alisema Tony.
“Nakupenda pia,” Martha alijibu.
Tony alijiona mshindi kwa kiasi kikubwa, kilichofata hakuna anayeelewa. Maana wote wakapitiwa na usingizi mzito.

*****************

Ni Asubuhi nyingine tena, Tony akawa wa kwanza kuamka, kichwa kilikuwa kizito mno kutokana na uchovu wa jana, akataka kutoka kitandani lakini akagundua kuwa hakuwa na nguo, akajaribu kuvuta kumbukumbu lakini alichokumbuka ni kuwa aliingia chumbani kwake na kulala akiwa na nguo zote. Alipotazama pembeni hakuyaamini macho yake alipoona Martha akiwa pale,
“Mungu wangu! Nini tena hii, huyu mwanamke amefata nini chumbani kwangu?”
Tony alijikuta akijiuliza mfululizo bila kupata majibu ya maswali yake, wakati akiendelea kufikilia hayo Martha naye akaamka, alishikwa na bumbuwazi baada ya kuona akiwa amelala na Tony kitanda kimoja. Akakurupuka lakini alishindwa kunyanyuka hasa baada ya kuona nguo zake zote zikiwa chini, alihisi kuchanganyikiwa asijue nini la kumfanya mwanaume yule,
“Tony kwanini umenifanyia haya tena chumbani kwangu bila ridhaa yangu,” alisema Martha.
“Nikuulize wewe Chumbani kwangu umefata nini, na kwanini umenifanyia haya,” Tony alijibu.

Martha alivyotazama vizuri akagundua kweli hakuwa chumbani kwake, nguvu zikamuisha akajikuta akidondosha chozi asijue nini la kufanya. Tony akachukia mno kwani pamoja na kujua kuwachezea wanawake lakini hakufikilia kama hatakuja lala na msichana yule, akaingia bafuni na kumuacha Martha pale kitandani. Martha akaamua atumie muda huo kurudi chumbani kwake ile anatoka mlangoni akakutana na Bosco, alishtuka mno, uso wa aibu ukamjaa. Bosco hakutaka akashikwa na kigugumizi asijue amwambie nini Bosi wake huyo,
“Bosi! Jana uliisahau funguo yako hivyo wamenipa nikuletee na sikujua kama utakuwa umelala kwa Tony,” alisema Bosco.
Martha akafungua mkoba wake na kugundua ile funguo aliyokuwa akiitumia usiku ulopita haikuwa ya hapo. Akaichukua funguo ile aliyopewa na Bosco bila kusema lolote, akaingia chumbani kwake na kujifungia humo. Bosco ikabidi arudi kwa wenzie akiwa anacheka jambo ambalo liliwafanya wawe na shahuku la kutaka kujua kilichojili,
“Hahahahaha! Jamani Tony sio mtu mzuri walah!” alisema Bosco.
“Kwanini wasema hivyo!” Jose akauliza.
“Mhmhm! Mlivyonipa ile funguo nikawa naelekea kwa Tony kumuuliza uenda akawa anafahamu lolote ila nilichokutana nacho nikaishiwa pozi”
“Umekutana na nini wewe”
“Nimemkuta bosi Martha akitoka chumbani kwa Tony na inavyoonesha walilala pamoja”
Kauli ile ikawa kama mwiba mkali kwenye kidonda kibichi ilipotua masikioni mwa Jose akajikuta anainuka na kuondoka bila kuaga.

***************

Tony alipotoka bafuni hakumkuta Martha, hakutaka kujishughulisha kujua alipo msichana yule japo ukweli hakuwa na ujasiri pia wa kuonana naye, akaamua kuama hoteli siku hiyo akapanga vitu vyake na kuondoka bila kumtaarifu yeyote.
Muda wa kukutana ukafika, wote wakakusanyika kasoro Tony pekee, Martha akajiuliza alipo mtu yule ila akashindwa kupata jibu, akatamani ampigie simu lakini hakuwa na ujasiri huo.
“Leo ni siku ya kuwa huru, nendeni popote mpendapo ila kumbukeni kesho asubuhi na mapema tutaanza safari ya kurejea Dar,” alisema Martha.

Kila mtu alifurahi isipokuwa Jose ambaye ni wazi hakuwa na raha hasa baada ya kusikia kuwa mwanamke anayempenda amelala na mwanaume mwingine tena asiyejua thamani ya mapenzi. Martha aliamua kutumia muda wake kukaa ufukweni na kuangalia mawimbi ya bahari, huku akifikiri mambo mengi ambayo yalikwisha tokea katika maisha yake, hakutaka kwenda popote siku hiyo. Jose aliona kuwa hiyo ndiyo nafasi pekee ya kuelezea hisia zake. Akajisogeza hadi alipo Martha,
“Tone moja la maji haliwezi badili ladha ya maji chumvi haya, ingawa kwa uweza wa Mungu yawezekana, ndivyo ilivyo kwa neno langu moja kutoweza kubadili msimamo wako ingawa kwa thamani halisi ya neno lile inawezekana,” alisema Jose.
“Unamaanisha nini kusema hivyo?” aliuliza Martha.
“Naomba hifadhi ndani ya moyo wako, naahidi kuwa mwema na muwazi siku zote”

Martha alishtuka mno kusikia kauli ile ya Jose hakuwahi kufikilia kama itatokea siku ataambiwa maneno yale.
“Martha nakupenda na nahitaji uwe wangu”
“Nadhani nilishakuweka wazi msimamo wangu juu ya mapenzi, tafadhali naomba uelewe siwezi kuwa na mtu kwa sasa”
“Sijali! Hata kama hutonipenda kwa sasa ipo siku utakuja nipenda huko baadae, tafadhali Martha!”
“Am sorry Jose! I can’t give you what you want, (Samahani Jose! Siwezi kukupa utakacho)”
“Why! Is it because of Tony?, (Kwanini! Je ni kwasababu ya Tony),” alisema Jose kwa hasira kidogo na kumfanya Martha ashtuke.
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 11
+255 713 373731

ILIPOISHIA………
Martha alishtuka mno kusikia kauli ile ya Jose hakuwahi kufikilia kama itatokea siku ataambiwa maneno yale.
“Martha nakupenda na nahitaji uwe wangu”
“Nadhani nilishakuweka wazi msimamo wangu juu ya mapenzi, tafadhali naomba uelewe siwezi kuwa na mtu kwa sasa”
“Sijali! Hata kama hutonipenda kwa sasa ipo siku utakuja nipenda huko baadae, tafadhali Martha!”
“Am sorry Jose! I can’t give you what you want, (Samahani Jose! Siwezi kukupa utakacho)”
“Why! Is it because of Tony?, (Kwanini! Je ni kwasababu ya Tony),” alisema Jose kwa hasira kidogo na kumfanya Martha ashtuke.

Tuendelee…………

“Tayari kuna mtu aliyeujaza moyo wangu, hivyo sizani kama nitaweza kumkubali mwingine yeyote”
“Sawa siwezi kuulazimisha moyo wako uniangukie ila ipo siku utagundua ni kiasi gani nakupenda na kwa ushauri tu, kaa mbali na Tony, ni mchezeaji tuu yule,” alisema Jose.
“Nimekuelewa,” Martha akajibu.
“Naomba tuwe hata Marafiki wa karibu”
“Tulishakuwa hivyo toka siku nyingi”
Maongezi yakaendelea baina ya wawili hao, kila mmoja alizungumzia jinsi kazi ilivyokua na kiasi kikubwa walifurahia,
“Hivi siku ya leo tutaimalizia hapa?” Jose akauliza.
“Yeah! Mimi sioni pa kwenda!” Martha akajibu.
“Twende tukatembee Raskazone”
“Aah! Sasa mazingira ya kule si yanafanana na ya huku”
“kule kuna fukwe nyingi na pamechangamka Zaidi, twende huko naamini kila mmoja ukimwambia atafurahi”
Ikabidi wawataarifu wenzao, wote kwa pamoja wakakubaliana na ilo wazo na kwa haraka wakaanza safari ya kuelekea Raskazone.

***********************************

Tony hakutamani kuuona uso wa Martha hasa baada ya kilichotokea usiku uliopita, akaamua atoke na kwenda Raskazone, huko akakodi chumba kwenye Lodge moja iliyo karibu kabisa na ufukwe. Kwa kuwa hakuwa na kazi ikabidi asogee hadi sehemu ya ufukwe, alishuhudia watu wa kila namna, aliduwazwa na uzuri wa wasichana waliyekuepo eneo hilo,

“Mwanamke siku zote yupo kwa ajili ya kumburudisha mwanaume, sio dhambi kama nitamtafuta wa kupumzika naye kwa siku ya leo, nitampata bila shaka,” alisema Tony huku akipiga hatua fupi fupi kuzunguka eneo la ufukweni.

Wakati anaendelea kuzunguka eneo hilo akazidi kuona vitu vilivyomvutia macho yake, watu walikuwa wakicheza na wengine kuogelea. Kilichomvutia Zaidi ni kuona wapenzi wakiwa wanakimbizana na kumwagiana maji,
“Daaah! Mapenzi kama uchizi yaani, kuna wakati unaweza kufanya jambo ambalo ukikaa na kufikili lazima ucheke,” alisema Tony huku akiendelea kuduwaa.

Akaendelea kuwatazama wapenzi wale huku akitembea, kufumba na kufumbua akajikuta akipigana kikumbo na mwanadada ambaye Tony alijikuta akitumia dakika moja nzima kumtazama, hakuwa mwingine ila ni Leilah mwanamke aliyetokea kuunyanyasa moyo wa Tony, jamaa hakuamini aliona ni kama ndoto, Leilah mwenyewe akabaki anashangaa kumuona Tony eneo lile,

“Leilah!”
“Tony!”
“Nafikiri Mungu anampango mzuri kati yetu hadi akaamua kutukutanisha katika hali kama hii na kwa mara nyingine tena,” alisema Tony.
“Mhmhmh! Acha kumshirikisha Mungu katika mambo yasiyofaa,” alijibu Leilah.
“Hahahah! Inaonekana ni muumini mzuri katika maswala ya Imani, hata hivyo siitaji kufahamu Zaidi, je naweza kupata muda wako hili tuzungumze japo kwa ufupi”
“Hakuna la kuzungumza kati yetu Tony, nadhani kila kitu kilikuwa wazi siku ile na sihitaji kurudia makosa”
“Unaonaje tukiongea sehemu ya wazi ambayo kila mtu atatuona”
“Ili iweje?”
“Nahitaji kukuondoa wasiwasi, nakuhaidi sitokugusa ila nipe muda kidogo tu nizungumze nawe”
Leilah akafikiri kidogo kisha akakubali ombi la Tony, wakaelekea sehemu iliyo na watu wengi lakini Leilah hakuipenda sehemu hiyo,
“Nadhani eneo lililo na watu wachache ni salama Zaidi kwangu,” alisema Leilah.
“Na iwe kama ulivyosema”
Tony akaongozana na Mrembo huyo ambaye muda wote tabasamu zito lilijaa kwenye sura yake,
“Mwanaume aliye kuoa wewe ni mwenye bahati sana,” alisema Tony.
“Kwanini?”
“Rangi yako angavu sioni haja ya taa nyakati za usiku, sura yako ya kupendeza sina haja ya kuangalia tv. una mwendo wa madaha Zaidi ya wanaogombania urembo wa nchi hata dunia, mbaya Zaidi uhusiano wangu na wako ni kama wa kiumbe na jua, kadri nitamanivyo kukusogelea ndivyo ninavyozidi kuungua,” alisema Tony baada ya kufika sehemu nzuri na kukaa na mrembo huyo.
“Naomba hifadhi Leilah japo kibarazani maana najua chumbani tayari kuna mtu kakaa”

Tony aliendelea kutoa maneno makali ambayo kiukweli yalizidi kumchanganya Leilah akawa akishindana na nafsi yake, upande unamwambia amkubali upande unamwambia akatae.
“Nalitamani busu lako Zaidi na Zaidi, hakika nashindwa kukutoa kwenye ufahamu wangu. Nakuona kila sehemu niendayo, wakati wakula, wakufanya kazi na hata wakati wa kulala taswila yako hunijia”.
“Tony usinifanyie hivi nashindwa kuvumilia,” alisema Leilah.
Kauli ile ikawa kama ushindi kwa Tony, akazidisha ukaribu kwa binti yule na akasahau kabisa kwamba anacheza na mali ya watu, safari hii aliamua kutumia viganja vyake kumtomasa Leilah hapa na pale. Maskini leilah hakuweza kuimili ushawishi wa mwanaume huyo, akajikuta kwa mara ya pili akimsaliti mumewe kwa kuunganisha ulimi wake na wa Tony.

Upepo wa bahari ukawa mkali Zaidi, mawimbi yakaongezeka ukubwa na kuwafanya watu waliokuwa wakiogelea kutoka sehemu hiyo. Tony baada ya kuhakikisha kuwa amecheza na akili ya Leilah vya kutosha akaamua abadili uwanja wa mapambano, safari ya kueleka chumbani ikaanza huku Leilah akiwa kama kuku wa kizungu asiyeweza kujinasua kwa mwanaume yule. Tony kila alipomuangalia Leilah ndipo alitamani afike kwa haraka chumbani hili aweze kutimiza haja ya moyo wake. Leilah hakuweza sema lolote kwa hakika alipagawishwa mno na Tony, wakafika chumbani bila kupoteza muda wakakumbatia kwa pupa na kuanza kupeana mabusu mazito. Tony taratibu akawa anapunguza nguo za mrembo yule, hapo Leilah akashtuka kidogo na kurudi nyuma,

“No Tony! We can’t do this, (hapana Tony! Hatuwezi fanya hivi),” alisema Leilah.
“Ooh! Come on Leilah! Am so excited to have you, (acha hizo Leilah! Nina hamu sana ya kuwa nawe)”
“This is wrong! Please try to understand, (hii si sawa, jaribu kuelewa tafadhali)”
Tony hakutaka kuongea Zaidi ya kumsogelea Leilah na kumgusa sehemu ambazo kwa kiasi kikubwa ziliamsha upya hisia za Leilah,
“Am somebody wife Tony! You will be in danger if my husband found out, (Mimi ni mke wa mtu Tony, utakuwa matatani mume wangu akigundua)”

Tony alizidisha kumkoleza mrembo huyo, akajikuta anashindwa kutoa sentensi zilizokamilika, na ikawa nafasi ya Tony kuamishia mashambulizi yake kitandani. Leilah hakuwa na kipingamizi chochote kwa Tony alionesha ushirikiano wote.

Baada ya shughuli iyo nzito kila mmoja akapitiwa na usingizi, huku nje Martha pamoja na wengine wakawa katika mazingira hayo wakiendelea kushangaa na kuburudika kila mmoja na namna yake.
***************************
Zay ambaye ni rafiki wa Leilah akaangaika kumtafuta rafiki yake asijue wapi alipoelekea, kila alipopiga simu ilikuwa ikiita bila kupokelewa mbaya Zaidi mume wa Leilah naye akaamua aje eneo hilo baada ya kuona simu ya mkewe haipokelewi. Zay aliogopa mno hakuelewa rafiki yake yupo katika mazingira yapi na alimuogopa Zaidi mume wa Leilah sababu si mtu mwenye utani wala masihara linapokuja swala la mkewe. Alimpenda sana mkewe na akamgharamia kila kitu na kwa kuwa haikuwa kawaida kwa Leilah kutopokea simu akaamua afike eneo hilo la Raskazone ajaribu kumtafuta.

“Samahani kaka yangu, kuna mdada namtafuta, ni mrefu kiasi, mweupe pia anashepu flani hivi,” alisema Zay.
“Mhmhmh! Ni yule mdada aliyevaa jinsi la blue hivi na blauzi flani panapana,” alijibu huyo mkaka ambaye ni muhudumu eneo hilo.
“Yeah! Ndiye yeye nambie alipo”
“Asee! Dada yangu mimi nilimuona akiwa na jamaa flani hivi sijui ndiye mumewe, walikaa muda mrefu hapo na baadae nikawaona wanaelekea ndani”
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 12
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

“Samahani kaka yangu, kuna mdada namtafuta, ni mrefu kiasi, mweupe pia anashepu flani hivi,” alisema Zay.
“Mhmhmh! Ni yule mdada aliyevaa jinsi la blue hivi na blauzi flani panapana,” alijibu huyo mkaka ambaye ni muhudumu eneo hilo.
“Yeah! Ndiye yeye nambie alipo”
“Asee! Dada yangu mimi nilimuona akiwa na jamaa flani hivi sijui ndiye mumewe, walikaa muda mrefu hapo na baadae nikawaona wanaelekea ndani”

Tuendelee…………

“Ndani!” Zay alishtuka sana.
“Ndio dada yangu”
“Unaweza kujua chumba walichopo”
“Aah! Ilo lipo nje ya uwezo wangu maana ni mambo binafsi ya mteja”
“Tafadhali kaka yangu naomba unisaidie huyo mwanaume aliyekuwa naye si mumewe na mumewe hivi tunavyoongea anakaribia hapa. Tukizubaa inaweza kuwa hatari kubwa mno,” aliongea Zay.

*******************

Baada ya saa kadhaa kupita Leilah akaamka, akajikuta akilia kwa kile kilichotokea, hakuamini kama siku hiyo aliweza kumvulia nguo mwanaume mwingine tofauti na mumewe. Wakati akiendelea kulia Tony naye akaamka na kumsogelea mrembo yule,
“Umenipa raha ambaye naweza kusema sijawahi ipata toka nilivyoanza kuingia ulimwengu wa mapenzi”
“Tony do you real love me? (Je unanipenda kweli Tony?)”
“Why? (Kwanini?)”
“I need to know, (naitaji kujua)”
“Mhmhmh! Vipi kama nitakwambia nilikutamani tuu na kwa kuwa shida yangu imeisha unaweza kwenda,” alijibu Tony.
“What…!? You can’t be serious!”
“Am seriously! Sina hata chembe ya utani juu ya hili akshante kwa penzi ulilonipa na uondoke zako”

Leilah akajikuta anaishiwa nguvu, akajiona Kama yupo ndotoni kile ambacho anakisikia, aliamini kuwa kadri ya muda unavyoenda ataamka na kusahau. Alishtushwa na mlio simu yake kuja kuiangalia akachanganyikiwa Zaidi baada ya kukuta missed call 17 za mumewe na 33 na rafiki yake kipenzi Zay, mapigo ya moyo yakaenda mbio Zaidi hasa baada ya kuiona meseji ya zay,
“Shoga umeniweka katika majanga, hapa nipo na mumeo tunakusaka, nimeambiwa na muhudumu kuwa upo chumbani na mwanaume mwingine kwa hiyo utajua mwenyewe namna ya kufanya”
Baada ya kusoma ule ujumbe akamgeukia Tony na kumwambia,
“Nakupenda sana Tony tena kuliko nilivyokuwa nampenda mume wangu japo nimekufahamu kwa kipindi cha muda mfupi, aidha nashukuru kwa kuaribu maisha yangu, mume wangu amejua kuwa nipo hapa na yupo nje ananisaka bila shaka atakuwa na watu wengine. Sina la kulipia ovu hili Zaidi ya kifo, Mume wangu ananipenda sana na wala sijakosa chochote toka kwake, ila umefanikiwa kuuteka moyo huu japo sikufikilia kama mwisho wake utakuwa hivi. Acha hii tabia Tony usitumie uzuri wako kuwachezea watu wasio na hatia, ondoka eneo hili utakuwa salama”

Maneno hayo yalimchoma sana, akajikuta akijutia sana kosa alilofanya. Kwa mara ya kwanza huruma ikamjia akawaza ni kwa namna gani atamsaidia msichana yule, machozi yakamtiririka mfadhaiko mkubwa ukamshika,
“Nifanye nini Leilah kukusaidia!”
“Niambie unanipenda walau mara moja tuu”
“Sasa hiyo ndiyo itasaidia nini?”
“Nitakufa nikiwa nakumbukumbu nzuri”

Kabla hawajaongea Zaidi mlango wa chumba walichomo ukagongwa, Tony akaogopa mno, jamani mke wa mtu ni kama asidi ambayo ukiichezea inakuunguza na kukutokomeza bila kubakisha hata kipande cha nguo yako. Tony alijenga ujasiri na kuufungua mlango akaduwaa Zaidi alipokutana Martha,
“Martha..! Wafata nini hapa?” Tony aliuliza kwa mshangao.
“Hakuna muda wa maswali chukua kilicho chako na tuondoke,” alisema Martha.
“Hapana siwezi kuondoka wewe nenda tuu,” alisema Tony.
“Acha ubishi unadakika 5 tuu za kuwa hapa,” ilikuwa sauti ya msichana mwingine ambayo haikuwa ngeni sana masikioni mwa Tony alipomtazama vizuri akagundua kuwa ni rafiki yake na Leilah.
“Nilikwambia kila kitu siku ile Tony, kweli mtu hawezi acha asili yake umeharibu maisha ya Leilah”
Zay hakutaka kusubili jibu lolote toka kwa Tony akaingia ndani na kumtaka Leilah avae nguo zake haraka kisha wakatoka kupitia mlango wa uani,
“Siwezi kumkimbia mume wangu Zay, nipo radhi kupokea adhabu inayonistahili”
Wakati akiongea hayo mume wa Leilah akafika akiwa amefura kwa hasira sana, hakutaka kuuliza akampiga vibao mfululizo Leilah hadi Zay akaogopa na kuhisi uenda mwanaume huyo atamua mkewe.
“Huu ndio upuuzi unaoufanya siku zote unapoaga kuwa unatoka?” aliongea mwanume huyo kwa hasira sana.
“Zay nilikuwa nakuheshimu kama mdogo wangu na kama shemeji yangu ila siamini kama nawe umeweza kushirikiana na mwanamke huyu kusaliti kiapo ambacho tulikiweka mbele ya sheikh, wazazi ndugu na jamaa”
“Ukweli nimekukosea sana mume wangu, naomba unisamehe japo najua sistahili tena kuitwa mkeo,” alisema Leilah huku akilia kwa kwikwi.
“Na huyu mpuuzi uliyekuwa naye yuko wapi?”

Mume wake Leilah aliuliza kwa ghazabu Zaidi kutaka kujua alipo Tony mwanaume aliyesababisha usaliti kwa mkewe. Wakati hali ikiwa hivyo upande wa pili ilikuwa aibu nzito kwa Tony kwani wafanyakazi waliomueshimu kama bosi wao leo wameshuhudia ujinga alioufanya, aliumia Zaidi alipomtazama Martha ambaye mbali na usiku uliopita kulala naye alihimili aibu ile ya kumfumania Tony na kumuokoa kwenye balaa ambalo angeweza kulipata kama wasingekuepo.
“Sikilizeni! Ratiba imebadilika tunaondoka usiku huu hatuwezi kusubili hadi kesho,” alisema Marthaa.
Jose alimchukia Zaidi Tony hadi kufika hatua ya kuomba bora angepigwa hadi afe kwenye fumanizi lile, Martha alijitahidi kuwa karibu na Tony na kumsihii atulize akili yake,
“Martha kwanini unanifanyia haya mimi kwa sasa sidhani kama nastahili,” alisema Tony.
“Mpumbavu wewe! Usifikiri kama nimefurahishwa na nimeridhishwa na uchafu ulioufanya, ila wewe una kazi ya mamilion kama ikipotea ni wazi kampuni zetu zitafirisika ndio maana nilikwambia nahitaji uwe hai,” alisema Martha.

*******************

Ilikuwa majira ya saa 2 usiku Leilah na mumewe wakiwa nyumbani. Mume wa Leilah alijaribu kumdodosa maswali kadhaa mkewe lakini hakuna hata moja alilojibu Zaidi ya kulia na kuomba msamaha huku akisisitiza kuwa yupo tayari kupokea adhabu yeyote ile.
“Nakupenda sana mke wangu siwezi kufanya jambo lolote la kukudhuru ila huyo mwanaume uliyekuwa naye hatoweza kutoka nje ya Tanga hii akiwa salama”
Kauli hiyo ilimtisha Zaidi Leilah akatamani amtetee Tony lakini kufanya hivyo kungesababisha mambo kuwa magumu Zaidi upande wake.
“Kitakachomkuta hatokaa akisahau katika maisha yake,” alizidi kuongea mume wa Leilah.
“Mimi ni mzigua hawezi kucheza na mke wangu nikabaki namtazama japo simfahamu ila ipo siku kama si yeye au ndugu zake watanitafuta kuniomba radhi”

************************

Safari ya kurejea Dar ikaanza usiku huo huku kila mmoja akiwa na hofu nyingi juu ya safari hiyo, kila mtu alianza kuomba kwa Mungu wake waweze kusafiri bila shida yeyote. Dereva alikuwa makini sana hakutaka kwenda mwendo wa kasi ila alichojali ni usalama wa watu aliowapakia. Mungu akawasaidia wakapita Tanga na viunga vyake salama ila mauzauza yakaanza pale tuu walipolikaribia daraja la Mto wami. Wakaona kundi kubwa la viumbe vya ajabu vyenye umbo mithili ya nusu binadamu nusu sokwe likiwa juu ya maji ya mto wami. Chakushangaza Zaidi ni pale walipoona moto ukiwa umekolezwa juu ya maji na ukiwaka bila shida yeyote.

“Mungu wangu nini kile!” alisema Martha kwa hofu kuu.
“Mungu tusaidie tuvuke salama eneo hili” Jose akasema
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 13
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Safari ya kurejea Dar ikaanza usiku huo huku kila mmoja akiwa na hofu nyingi juu ya safari hiyo, kila mtu alianza kuomba kwa Mungu wake waweze kusafiri bila shida yeyote. Dereva alikuwa makini sana hakutaka kwenda mwendo wa kasi ila alichojali ni usalama wa watu aliowapakia. Mungu akawasaidia wakapita Tanga na viunga vyake salama ila mauzauza yakaanza pale tuu walipolikaribia daraja la Mto wami. Wakaona kundi kubwa la viumbe vya ajabu vyenye umbo mithili ya nusu binadamu nusu sokwe likiwa juu ya maji ya mto wami. Chakushangaza Zaidi ni pale walipoona moto ukiwa umekolezwa juu ya maji na ukiwaka bila shida yeyote.
“Mungu wangu nini kile!” alisema Martha kwa hofu kuu.
“Mungu tusaidie tuvuke salama eneo hili” Jose akasema

Tuendelee…………

Wakati huo wote Tony alijua kuwa yeye ndiye mtu anayewindwa kutokana na uovu alioufanya, roho ilimuuma Zaidi hasa baada ya kuona hatari ambayo ingeweza kusababisha wengine kupata madhara,
“Hapa itabidi nitembee mwendo wa taratibu sana, msiangalie nje tutapita salama,” alisema dereva.
Mungu mkubwa wakavuka daraja lile bila shida yeyote, safari ikaendelea lakini kabla hawajafika mbali Zaidi gari ikazima ghafla, ikabidi Tony, dereva na wanaume wengine washuke ndani ya gari kuangalia tatizo ni nini. Mazingira waliyokuepo yalikuwa yakuogofya sana kwani hakukuwa na dalili za makazi ya watu jirani na hapo, ulikuwa ni msitu huku sauti za ndege na wanyama mbalimbali zikisikika.

Baada ya kuangalia vizuri gari hawakuona tatizo lolote, dereva ikabidi aingie ndani na kujaribu kuliwasha likawa linawaka na kuzima ila baadae likakubali. Wote wakaanza kuingia ndani ili kuendelea na safari, huku nyuma Tony akaanza kusikia kitu kama kinatembea kwenye kichaka, ikabidi ageuke kutazama hakuweza kuona chochote. Akasogea ulipo mlango wa gari na kuanza kupiga hatua kuingia ndani na kabla hajamalizia mguu mwingine akatokea nyoka mmoja mweusi na mrefu sana akamgonga, Tony alitoa yowe la mshtuko lilochanganyika na maumivu, ikabidi Bosco na Jose watazame kilichomkuta Tony. Wote walijaa na uoga hasa baada ya kumshuhudia nyoka mkubwa vile na mwenye kung’aa akiwa karibu na Tony, nyoka yule alivyoona watu wanashuka akaingia kwenye vichaka na kutokomea. Wakasaidia kumuingiza Tony kwenye gari na kumfanyia huduma ya kwanza huku dereva akiongeza mwendo walau kufikia eneo lenye huduma za afya.

Hali ya Tony ilibadirika ndani ya muda mfupi, wote walishuhudia mguu wa Tony ukianza kubadirika rangi na kuwa mweusi kama mkaa. Tony hakutaka kulalamika kwa Mungu sababu alijua kuwa ni wazi yanayomkuta sasa ni malipo ya dhambi zake,
“Msihuzunike juu yangu, kuweni na Amani tuu haya yamenistahili,” alisema Tony.

Martha alishindwa kujizuia akajikuta akidondosha chozi, hali ilikuwa tofauti kidogo kwa wengine kwani waliona hata adhabu hiyo ni ndogo. Dereva alitembea kwa kasi sana bila kupata shida yeyote na wote waliamini kwa kuwa walishampata mtu wao hivyo kusingekuwa na madhara mengine kwenye safari hiyo. Saa mbili baadaye wakawa wamefika wilayani Bagamoyo ikiwa ni karibu kabisa na nyumbani kwa Tony. Martha ikabidi awapigie Yassir na Darmy ambao ni marafiki wa karibu sana wa Tony. Wakafika na kumkimbiza Tony hospitali,
“Amekutwa na nini?” Yassir aliuliza baada ya safari ya Hospitali kuanza.
“Ameumwa na nyoka usiku huu”
“Inaonekana nyoka huyu ana sumu kali sana, ila mmefanya vizuri kumfanyia huduma hii ya kwanza,” alisema Darmy.

*******************

Ni katika maeneo ya Sahare mkoani Tanga ambapo Leilah na mumewe wanaishi, Asubuhi hiyo mume wa Leilah alionekana kuwa na furaha sana,
“Mke wangu kazi iliyokuwa ikiniumiza kichwa nimeimaliza na hapa nasubili siku 9 ili nimalize kila kitu,” alisema mumewe Leilah.
“Kazi gani tena mume wangu?” akauliza Leilah.
“Yule mpuuzi aliyesababisha usaliti wa agano letu, maisha yake yapo matatani kwa sasa na hata akinusurika kwa hili basi atakuwa mtu wa kitandani na hatoweza kunyanyuka hadi umauti”.
Kauli ile ilimtisha sana Leilah, akajikuta akiangusha chozi kwa kumuhurumia Tony,
“Mume wangu haya utayafanya mpaka lini? Kila siku ukiendelea kukumbushia ilo jambo mimi nakosa Amani na najiona mkosaji nisiyefaa kusimama mbele yako”.
“Ingawa nimekusamehe lakini yule mpuuzi atalipa kwa aliyoyafanya na ndio ameanza sasa, zikifika siku 9, nitafikiria kama kummaliza kabisa au kumuacha hivyo hivyo,’ alisema mume wa Leilah.

**************************

Baada ya vipimo kufanyika, Daktari akatoa majibu ambayo yanashtua na kuhuzunisha nyoyo za wengi huku kwa baadhi ikiwa ni furaha na sherehe yenye kufana,
“Nasikitika kuwaambia kuwa sumu imemuathiri sana Tony na hatuna namna ya kufanya zaidi ya kuukata mguu huu ili kuzuia sehemu nyingine ya mwili kudhurika aidha upande wake mmoja umepooza hatoweza kuinuka wala kufanya lolote kila kitu atakifanya akiwa kitandani,” alisema daktari.
Taarifa ile ilikuwa ni Zaidi ya msiba kwa Yassir na Darmy, hawakujua maisha yatakuaje bila rafiki yao huyo ambaye walishirikiana naye katika mambo mengi,
“Msijali jamaa zangu hii ni mitihani ya dunia,” alisema Tony.
Walishindwa kumwambia chochote maana mara nyingi walijitahidi kumshauri atulie hakuwaelewa, taarifa ya fumanizi liliwaumiza mno.
“Naomba mnipeleke kwangu sitaki kuwa mzigo kwenu ila kikubwa naomba muiangalie sana kampuni naiacha mikononi mwenu maana lolote laweza kutokea”

***********

Wakamchukua Tony na kurudi nae nyumbani, siku zikaenda na hakuna yeyote aliyejitokeza kuja kumtazama wengi waliamini kuwa Tony ni muovu na amestahili adhabu ile. Shughuli za kampuni ya Studio 7 Media Ltd. Zikaendelea kama kawaida japo hakuwa na uwezo wa kushika chochote aliwapa maelekezo rafiki zake ambao waliacha shughuli zao na kuamua kujikita katika kampuni ya swahiba wao kipenzi.

“Project iliyofanyika Tanga lazima tuihariri na iwe nzuri mimi sina uwezo wa kushika chochote lakini akili yangu bado inafanya kazi hivyo nendeni ofisini kachukueni data na sauti ambazo zimesharekodiwa”
Yassir ikabidi aende ofisini na kuonana na Martha ambaye hata hivyo alikataa kata kata kutoa data zikafanyiwe kazi,
“Tony hawezi kwa sasa acheni kazi tutaifanya hapa,” alisema Martha.
“Mie nafata maelekezo ya Tony tuu, hii kazi ni ya mamilioni ya pesa, hata kama mwili wake haufanyi kazi lakini bado akili yake ni nzima, naomba tafadhali,” alilisisitiza Yassir.
“Nenda bhana! Wewe umeona wapi maiti ikafanya kazi,” Jose akaingilia kati maongezi yale.
Yassir alijisikia vibaya sana kwa kauli aliyoitoa Jose akabaki anamtazama Martha asikie atamwambiaje lakini hakuambiwa lolote,
“Martha kumbuka wewe ndiye sababu ya haya yote, Tony hadi kuwa vile wewe ndiyo chanzo ila tumekuvumilia tuu na hata yeye hakutaka lolote lifanyike juu yako, leo hii bado anaendelea kupokea adhabu kutokana na kosa ulilolifanya wewe,” Yassir aliongea kwa hasira mno.

Jambo lile likazua maswali mengi kichwani mwa Jose ambaye ni wazi hakuwa anaelewa vitu vingi kuhusu wawili hao,
“Sitaki kusikia lolote juu ya Tony, na sina kosa la kujutia juu yake, mwambie mkataba hautovunjwa japo hatofaidika na chochote kutokana na yeye kuharibu kazi,” aliongea Martha.
“Sawa zimemfikia,” alijibu Yassir na kuondoka eneo hilo.

**************

Taarifa za kuugua kwa Tony zilifika masikioni mwa wengi sana, kila mmoja akajaribu kuchimba ila kujua kiini cha tatizo. Wengi walitofautiana na majibu wapo waliosema amelogwa na wapo walioamini ni ajali tuu ambaye inaweza kumtokea yeyote. Habari ya ugonjwa wa Tony ikatua masikioni mwa mjomba wake kipenzi na kumtaka apelekwe nyumbani kwake haraka iwezekanavyo.
Baada ya mipango kukamilika Tony akapelekwa kwa mjomba yake ambaye anaishi Mkoani Mbeya wilaya ya Tukuyu, Mjomba wake huyo alioa mke wa kinyakyusa hivyo akabahatika kumiliki mashamba kadhaa ya mpunga pamoja na mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kuku na nguruwe. Mbali na kuwa na mali hizo hakutamani kabisa kuishi katika jiji la Dar es Salaam. Tony alifikishwa Tukuyu akiwa bado na hali mbaya sana, mguu ulizidi kuwa mweusi na kufanya hata sehemu nyingine za mwili kuanza kuwa nyeusi,
“Huyu si nyoka wa kawaida,” alisema Mjomba.
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 14
+255 713 373731


ILIPOISHIA………

Baada ya mipango kukamilika Tony akapelekwa kwa mjomba yake ambaye anaishi Mkoani Mbeya wilaya ya Tukuyu, Mjomba wake huyo alioa mke wa kinyakyusa hivyo akabahatika kumiliki mashamba kadhaa ya mpunga pamoja na mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kuku na nguruwe. Mbali na kuwa na mali hizo hakutamani kabisa kuishi katika jiji la Dar es Salaam. Tony alifikishwa Tukuyu akiwa bado na hali mbaya sana, mguu ulizidi kuwa mweusi na kufanya hata sehemu nyingine za mwili kuanza kuwa nyeusi,
“Huyu si nyoka wa kawaida,” alisema Mjomba.

Tuendelee…………

“Wengi walisema hivyo, na tumejaribu kuhangaika katika mahospitali na kauli yao ya mwisho ni kwamba Tony akatwe mguu jambo ambalo yeye mwenyewe hakuridhia,” alisema Darmy.
“Sawa! Kwanza niwashukuru sana kwa moyo wenu wa upendo hadi hapa mlipofikia naomba niwasaidie kumuuguza huyu mpwa wangu hili ninyi shughuli zenu zisilale, tutajitahidi kadri Mungu atakavyotujalia naamini kwa uweza wake atapona,” alisema Mjomba.

**************

Ndani ya kipindi hiko kifupi habari zikasambaa mtandaoni juu ya kuugua kwa Tony, mume wake Leilah akawa mmoja kati ya watu aliyeona habari ile, kwa haraka Zaidi akamuita mkewe na kumuonesha kuwa yule ndiye au la. Maskini Leilah alishindwa kuvumilia akajikuta akitoa machozi mbele ya mumewe.
“Mume wangu basi yatosha muache kijana wa watu, mimi sitorudia kosa naamini hata yeye hatorudia kosa hilo”
“Hahahahaha! Mimi nimemalizana naye kuna dawa ilikuwa nimmalize na mbele yako leo naichoma moto, ataishi hivyo alivyo sababu hakuna dawa ya kumtibu Zaidi ya kumuangamiza,” alisema mume wa Leilah kwa dharau mno.

BAADA YA MIEZI 4

Afya ya Tony iliziidi kudhoofika kwa kiasi kikubwa, matumaini ya kuishi yakadidimia mno, mjomba wake hakukata tamaa Zaidi ya kuangaika na dawa za mitishamba, aliwafata wazee wa kila aina na kila mmoja akawa na maoni tofauti. Swala la kupiga lamli likawa likiongelewa na wengi ila mjomba huyo hakuwa kabisa na Imani hizo, alimuamini Mungu wake na kama amepanga mpwa wake aendelee kuishi basi hakuna litakalopangua.

***********************

Kutokana na Tony kushindwa masharti ya mkataba waliowekeana kati ya kampuni yake na kampuni ya Tae Xhiang Sung Group ambayo inaongozwa na Martha kama balozi akiwakilisha Makao makuu ambayo yapo nchini Korea ya Kusini. Maamuzi yakafikiwa kuwa mkataba lazima uvunjwe na Tony anapaswa kulipa hasara yote ambayo imejitokeza,

“Hapana hii sio haki! Tony hawezi kuwapa chochote ninyi, hapa tunapoongea anapigania uhai wake, msimfanyie hivyo tafadhali,” aliongea Yassir kutetea hoja.
“Ni kweli Tony lazima alipe hasara iliyopatikana, hana pesa lakini ana nyumba nzuri ambayo ikiuzwa tunaweza kufidia hasara hii,” aliongea Bosco.
“Tatizo bosi unaingiza maswala binafsi katika kazi, mtu Malaya kama yule, wewe bado unataka kumtetea hili iweje!” Jose akasema kwa ghadhabu.
Darmy na Yassir wakajikuta wakisimama kwa hamaki, wote walishindwa kusema neno. Martha akasimama na kuwataka wakae chini na kisha akasema,
“Hasara yote hii nitailipa mimi, na mkataba kati ya Studio 7 Media LTD. Na Tae Xhiang Sung Group utaendelea kama kawaida”.

Watu wote walishangaa sana, wengi wakapinga swala lile. Hata hivyo Martha akabaki na msimamo huo huo,
“Sijaona kampuni ya ajabu kama hii, mimi nakuwa wakwanza kuacha kazi,” alisema Jose.
“Mimi pia naacha,” Bosco akadakia.
Martha akawatazama wengine hili kujua kuwa nao msimamo wao uko vipi. Nusu ya wafanyakazi wakaungana kuachana na kampuni hiyo kama mkataba utabaki vilevile.
“Hatufanyi kwa ajili ya pesa tuu, ila tuna mapenzi ya kile tunachofanya, hatuwezi kuvumilia upuuzi wa mtu mmoja ukiharibu kazi”.

Kabla ya Martha kujibu akataokea mzee mmoja wa makamo ambaye yeye alipewa nafasi ya kufanya kazi kama mshauri katika kampuni hiyo, akasogea hadi mbele na kuwaomba wote wakae na kumsikiliza kile ambacho anataka kuwaambia. Wote wakatii na mzee akaanza kuongea,
“Mnajua nini kuhusu Tony ninyi! Bosi wenu yupo sahihi katika maamuzi haya, mnafikiri Tony alikuwa na tabia hii?”
Watu wote wakakaa kimya, minong’ono ya hapa na pale ikaendelea ila kwa busara za mzee wote wakaona haya na kuamua kumsikiliza.
“Badala ya kujadili ni namna gani tunaweza kumsaidia mwenzetu ninyi mnajadili namna ya kumdidimiza na kutaka kumyang’anya hata kile alichokuwa nacho”
Mzee akavuta kiti na kukaa na kuwataka wamsikilize kwa makini kisha baada ya simulizi atakayowapa, wana uhuru wa kufanya lile watakaloona ni sawa. Mzee akaanza simulizi yake kama ifuatavyo..

*********************

Miaka 5 iliyopita Tony hakuwa na ndoto za kuwa director kitu pekee alichokipenda katika maisha yake muziki alijua kuimba hata kutunga pia, alikuwa ni mtu mwenye nidhamu na heshima kwa kila mwanadamu, hakujua kutumia kilevi wala hakujua starehe ya wanawake. Kutokana na kipaji kikubwa alichokuwa nacho wengi wakamshauri ashiriki mashindano ambayo hufanyika kila mwaka kumsaka mtu mwenye kipaji cha uimbaji. Alifata ushauri wa wengi na kuingia katika mashindano hayo.
“Mabibi na mabwana ule wakati tuliokuwa tukiusubiria sasa umewadia, ivyo kwa heshima na tahadhima namkaribishaa…”
Kabla ya mc hajamalizia tayari mashabiki wakawa wanataja jina la kijana ambaye ameteka hisia za wengi toka shindano lenye kusaka watanzania wenye vipaji mbali mbali kuanza “Tanzania Got Talent”.

“Tony! Tony..! Tony..!”
“Kijana huyu ni tishio kwa ushindi wangu,” akaongea mshiriki mwenza wa shindano ilo katika kipengele cha uimbaji.
“Jinsi anavyoimba, sauti na mpangilio wake wa mashairi hakika hamna kitachomnyima ushindi”.

Kila mmoja aliongea lake kumuhusu kijana huyo, tupia mbali kipaji chake, muonekano tuu ulizidi kuwavuruga wengi, kwa hakika Tony ni miongoni mwa vijana watanashati tena asiopitwa na wakati, mwenye kujiamini na ubunifu wa hali ya juu katika kila anachokifanya. Uwezo wake wa kuona mbali ndio ulimfanya aonekane mpya na wakipekee kila apandapo jukwaani.
“Yalinikuta kama yako rafiki, aliuteka moyo wangu nikajiweka usoni pake kabla ya macho yangu. Akaukataili moyo huu na kuniacha kilema, kwani ukumbuki tulivyokutana na akanikiss, sasa kwanini aniache bila kuangalia nyuma, ila rafiki nimeamua kutompenda yeyote tena”.

Yalikua baadhi ya maneno yaliyokuwa kwenye nyimbo ambayo Tony alikuwa akiimba, ukumbi mzima ulizizima kwa nderemo na vifijo baada ya kuona Tony ameingia katika 10 bora za shindano ilo.
“Mhm! Hongera jamaa yangu leo umekamua kichizi”
“Hahaha! Kwani siku zote hujui shughuli yangu iko vipi?”
“Ila jamaa ulivyoimba kama umetendwa kweli yale mahisia nini daah! Nikaona watu wanalia huku”
“Duuh! Kumbe walilia eenh!”
“Sana tuu yaani”
“Basi kikubwa ngoja nijipange maana shindano limefika patamu” yalikua maongezi kati ya maswahiba wawili, Darmian akimpa pongezi zake Tony.
Kisha kwa pamoja wakawa wanatoka ukumbini tayari kwa kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwao, wakafika nje na kusimama kidogo,
“Hivi Yassir yukwapi si alikuja leo?” Tony akauliza
“Daah! Bora ulivyonikumbusha tungemwacha”
“Yupo wapi kwani”
“Twende hivi tukamcheki”
“Sawa”.
Tony akakubaliana na Darmy taratibu wakawa wanaelekea alipo lakini kabla hawajafika mbali, wakasikia mtu akiita
“Tony! Darmy!”

Walipogeuka wakakuta Yassir akiwa na msichana ambaye kwa hakika alikuwa mrembo Zaidi, mwanga hafifu wa mbalamwezi haukuweza kuuficha ung’aavu wa sura yake. Hakuwa na umbile kubwa la kutisha, umbo lake la wastani lilifanya Darmy na Tony kutumia dakika kadhaa kumtazama mrembo yule, hakuna aliyeweza kuuzuia moyo wake usiende mbio hasa msichana yule alivyotoa tabasamu. Vishimo vidogo vilivyojitokeza mashavuni mwake vilizidi kumpa sifa ya kuwa mwanamke ambaye kila mwanaume anaweza kuota kuwa naye.
“Tony, Darmy huyu anaitwa Martha ni rafiki yangu,” Yassir akatoa utambulisho mfupi ambao vichwani mwa jamaa zake ukawa bado umeacha maswali mengi.
 
USALITI WA KIAPO
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 15
+255 713 373731


ILIPOISHIA………
Walipogeuka wakakuta Yassir akiwa na msichana ambaye kwa hakika alikuwa mrembo Zaidi, mwanga hafifu wa mbalamwezi haukuweza kuuficha ung’aavu wa sura yake. Hakuwa na umbile kubwa la kutisha, umbo lake la wastani lilifanya Darmy na Tony kutumia dakika kadhaa kumtazama mrembo yule, hakuna aliyeweza kuuzuia moyo wake usiende mbio hasa msichana yule alivyotoa tabasamu. Vishimo vidogo vilivyojitokeza mashavuni mwake vilizidi kumpa sifa ya kuwa mwanamke ambaye kila mwanaume anaweza kuota kuwa naye.
“Tony, Darmy huyu anaitwa Martha ni rafiki yangu,” Yassir akatoa utambulisho mfupi ambao vichwani mwa jamaa zake ukawa bado umeacha maswali mengi.

Tuendelee…………

“Martha huyu bila shaka unamfahamu na huyu ni rafiki yangu pia anaitwa Darmian au Darmy kwa kifupi”
“Sawa nafurahi kuwafahamu,” alisema Martha huku akiwapa mkono.
“Sasa jamani mimi natoka ila narudi muda si mrefu,” alisema Yassir.
“Wee unaenda wapi saa hizi, mida hii” Tony akasema.
“Vunga kidogo, pigeni stori na mrembo huyo nakuja”.
“Tony mimi ni shabiki yako sana, ukweli napenda jinsi unavyoimba natamani nami ningejua kuimba lakini ndio hivyo si kipaji changu,” alisema Martha huku akitabasamu.
“Nashukuru sikuwahi kufikiria kama naweza kuwa na shabiki kama wewe,” Tony akajibu.
“Daah! Usanii raha kweli ushanizidi kete jamaa” Darmy akasema, Tony akajikuta akicheka japo Martha hakuwa ameisikia vizuri kauli ya Darmy.
Baada ya dakika 10 Yassir akawa amerudi akiongozana na msichana mwingine na mwenye mvuto wa kipekee.
“Mhm! Huyu mjinga hawa warembo anawatolea wapi?” Darmy akamuuliza Tony kwa sauti ya chini.
“Hata mimi sifahamu”
“Jamani eenh! Huyu ndio shemeji yenu anaitwa Grace na nimefahamiana na Martha kupitia yeye sababu wao ni marafiki” Yassir akawatumbalisha.
Baada ya hapo wakaagana na wale wasichana na kuingia kwenye Bajaji ambayo iliwapeleka moja kwa moja hadi mtaani kwao. Njiani mazungumzo yakaendelea,
“Hivi wale wasichana umefahamiana nao vipi?” Darmy akauliza.
“Wale wasichana nilikutana nao ukumbini, nilianza kumuona Grace ikabidi nianze kulia shida ila akawa anielewi, Mungu fundi Tony ukapanda jukwaani, kabla hujaanza kuimba ikabidi nianze kusema yale mashairi (yalinikuta kama yako rafiki, aliuteka moyo wangu nikajiweka usoni pake kabla ya macho yangu, akauktaili moyo huu na kuniacha kilema…). Taratibu nikaona mtoto aniangalia kisha akauliza, Unamaana gani? Mimi nikamjibu kuwa nampenda Zaidi ya neno kupenda. Nikaona anaanza kunielewa hivi, apo apo nawe ndio ukaanza kuimba tena maneno yale yale, nikajifanya kama kumpotezea akaanza kuniuliza, “kwani Tony unafahamiana naye?”, aah hapo ndio nikaona ngoja nimmalize kabisaa, nikamwambia mimi ndiye mwalimu wake yaani mashairi na nyimbo anazoimba mimi ndio nazitunga”.
Kufika hapo wote wakajikuta wakiangua kicheko hadi dereva wa bajaji naye akacheka bado kidogo apoteze umakini na kuingia mtaroni.
“Duuh sasa siku ukigundulika kama hujui kuimba wala kutunga hamna atakayekutetea!” Darmy akasema.
“Mhm! Acha kunitia mkosi hadi aje kugundua itakua baadae sana labda muamue kuuza gazeti”.
Muda wote Tony alikuwa anacheka tuu kwa ule mchezo ambao Yassir ameucheza hakika haukuwa wa kitoto.
“Tony kuna mzigo wako Martha ameniambia nikupe”.

Yassir akatoa kikadi kidogo chenye mawasiliano na kumkabidhi Tony. Wakati huo wakawa washafika mtaani kwao, wakamlipa dereva wa bajaji na kila mmoja akashika njia yake.
Tony anaishi na dada ake wa pekee ambao kiukweli ndugu hao wanapendana sana, wanashauriana na kusaidiana kwa kila hali, Wazazi wao walifariki miaka kadhaa iliyopita. Maisha yao yalikuwa yakawaida, hayakuwa ya juu sana wala ya chini sana, Biashara ndogo ndogo zilizoachwa na wazazi wao ziliwasaidia katika kupata ridhiki ya kila siku.
“Hongera mdogo wangu, japo sikuwa ukumbini ila nilikuwa nakufatilia kwenye luninga, ukweli najivunia kuwa na ndugu kama wewe”
“Hongera nawe dada, kwani bila msaada na ushauri wako nisingalifika hapa nilipo sasa”
“Nakupenda sana mdogo wangu”
“Nakupenda pia dada”. Yalikuwa maongezi mafupi kati ya Tony na dada yake kabla ya kuingia chumbani kwake na kulala.

************************

Siku zikazidi kusonga hatimaye mchujo ukapita na Tony akafanikiwa kuingia fainali ambapo washiriki watano watashindana kumpata mshindi mmoja. Tarehe ikatangazwa na wasanii maarufu ndani na nje ya nchi wakaalikwa kushuhudia ni nani atakayeibuka kuwa mwenye kipaji Zaidi ya wengine. Kila mshiriki akawa anajiandaa kwa anavyoweza kuhakikisha anaibuka mshindi, Kwa upande wa Tony hakuwa na wasiwasi kwani alijua wazi hakuna anayeweza kumshinda.
“Wewe ndiye jaji mkuu, hakikisha Tony hapati ushindi badala yake mtangazeni Daniel kuwa mshindi wa huo mchuano”.
“Ilo haliwezekani, watanzania wanamkubali sana Tony na hata ukiangalia Daniel uwezo wake ni mdogo ukilinganisha na Tony”
“Sawa nitajua mimi cha kufanya, Daniel lazima awe mshindi”.
Yalikuwa maongezi kati ya jaji mkuu na mzee mmoja mwenye uwezo wa kipesa, anaushawishi mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao kutokana na pesa alizonazo lolote atakalotaka liwe linakuwa. Na uamini kuwa palipo na pesa hamna litakaloshindikana, jina lake maarufu ni Pedeshee Mkwanja.
“Unafikiria kufanya nini?” jaji akauliza
“Daniel ananifaa sana katika shughuli zangu na nimemuahidi ushindi kama zawadi yangu ya kwanza katika kukubali kuungana nami”.
Mzee akaingia mfukoni na kutoa kibunda cha pesa na kumkabidhi jaji, kisha akatazama huku na huko na kumwambia,
“Hii ni zawadi yako, hakikisha ufungui kinywa chako na kumwambia yeyote juu ya haya tuliyoyaongea”
“Sawa kuwa na Amani”
Pesa inashawishi sana,jaji yule hakuweza kuikataa, akapokea kitita kile cha pesa na kukisunda mfukoni tayari kwa kumnyima haki Tony.

***********************

Kadri siku ya fainali ilivyokuwa inakaribia ndivyo umaarufu wa Tony ulizidi kuongezeka katika vyombo mbali mbali vya habari na hata katika mitandao ya kijamii, wengi walikua na uhakika kuwa kijana huyo ndiye anafaa kutwaa taji la “Tanzania Got Talent”.
“Tony hivi karibuni vyombo vya habari, mitandao ya kijamii havitakuwa na la kuandika juu yako badala yake mimi nitatawala,” alisema Daniel baada ya kuona taarifa za Tony.

Hakuna aliyejua mipango ya siri inayofanyika kumuangusha Tony, kila mmoja akawa anaisubiri siku ya fainali kwa hamu zote. Baada ya mazoezi mazito Tony akakaa na rafiki zake wakipeana ushauri juu ya iyo siku ya fainali,
“Usiwaze sana ndugu yangu, huna mpinzani kaka” Darmy akaongea na Yassir akadakia
“Daah! Mimi hapa nafikiria nitokeje siku hiyo, alafu ukipewa tuzo lazima nije na mimi walau niuze jukwaani”
“Wewe unataka kuuza si kwa sababu ya Grace!”
“Aah! Umejuaje asee, yaani siku hiyo acha, kwanza swaga zinaongezeka yaani mtoto akinicheki aone kama majaji wamekosea kutoa tuzo”
“Unamaana gani?” Darmy akauliza
“Mimi ndiye ningepewa badala ya Tony”.
Muda wote huo Tony hakuongea neno akabaki kuwasikiliza na kufurahi,
“Ukweli najisikia furaha sana kuwa na marafiki ambao ni kama ndugu kwangu, ninyi mmekuwa sehemu ya muhimu sana katika maisha yangu, sitowasahau kamwe”.
“Aah! Kawaida tuu usijali, tupo pamoja katika kila hali”.
“Asanteni sana”.
“Tony eenh! Baadae hivi kuna sehemu nataka unisindikize,” Yassir akasema.
“Wapi tena..?”
“Wee kubali kwanza kisha nitakwambia tutakapoelekea”.
“Sawa tutaenda”.
“Nawe Darmy vipi?”
“Aah! Mimi siendi popote leo!”
“Acha hizo bhana, twenzetu sio ishu kila siku kukaa kitaa”
“Poa tutaenda,” Darmy akajibu.
“Tukajiandae basi saa moja jioni tunaenda,” alisema Yassir.
“Sawa, ila hujasema tunaenda wapi?”
“Mtajua huko huko”
“Mhmh haya bhana”.

*********************

Muda waliopanga kukutana kwa ajili ya safari ukawadia, kama ilivyokuwa kawaida usafiri wao mkubwa ni bajaji hivyo wakamuita dereva wao wasikuzote, bila kupoteza muda akaja na kuianza safari.
“Oya suka ongeza mwendo tumechelewa sana,” alisema Yassir.
“Sawa bosi usijali! Si umesema ni tabata Chang’ombe?”
“Yeah pale Chikoho hotel”
“Poa dakika chache tutakuwa tumefika!”
“Fanya kweli suka”.
Tony na Darmy hawakujua wanapoelekea hadi waliposikia toka kwa dereva, wakamgeukia Yassir na kumuuliza,
“Mhmh! Wewe jamaa Chikoho hotel tunaenda akufanya nini?”
Kabla hajawajibu, simu ya Yassir ikaita na kwa haraka Zaidi akaipokea,
 
Back
Top Bottom