Usaliti! Usaliti! Usaliti! Tafakuri ndani ya Mwezi mchanga, au katikati ya ndoto

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Wadau salaam,

Sisi wazalendo tumekuwa katika hali ya kuipigania nchi wakati wote! si mnaona tunavyopambana na mafisadi? Sasa tunasema hivi, mafisadi watatukoma safari hii. Tunasema ni lazima mkaguzi wa serikali akague mahesabu yao na aone ufisadi ulioko humo. Sisi siku zote tumekuwa ni mfano, na hakuna haja ya kukaguliwa! na hawa wanaojifanya eti wazalendo wanajidai eti na sisi tukaguliwe,oh! mara tutoe taarifa ya mapato na matumizi mara ooh! sijui nini na nini, ni wasaliti hao! achaneni nao kabisa wasaliti hao wachumia tumbo! sisi tunapambana na mafisadi wanatuletea mambo ya ajabu!Au inamaana wao hawawaoni hao mafisadi hao? au usaliti tu umewajaa! ni wakuwapuuzza hawa!!!

Tunasema hivi! huu ni wakati wa kumng'oa mkoloni mweusi tuu na si vinginevyo!, kwa hiyo tuwaache wana mapinduzi wafanye kazi zao hadi wakamilishe mapinduzi, sijui tunaelewana!.Suala la watu kutaka mara sijui chaguzi huru, wazi, za haki na ushindani katika chaguzi za ndani , mara sijui nini na nini, mara kubana bana pua, huo ni usaliti na kurudisha nyuma mapambano yetu.Ndio! huo ni usaliti unaofanywa na wanafiki wachumia tumbo! Kwanza wameshapewa hela hao, mamluki wasaliti wakuu!

Wakati wote tumekuwa na tuna maamuzi na fikra za kadiri kwa kuwa sisi ndio wazalendo wa kweli, busara zetu zimekuwa za kadriii, hekma zetu za kaadri, na uzoefu wetu wa kadri vile vile. Ni lazima tuwashungulikie haswa ila sasa kuna viwasaliti fulani hivi vinajaribu kujifanya eti vinatukosoa! unatukosoa sisi! Msaliti wewe! nasema wewe ni msaliti mkubwa! period!Kwanza sijui hata kwa nini nimezungumza na wewe msaliti wewe!

Unapojiunga na sisi umejiunga na wazalendo, na unapoamua kujitenga nasi au kujiunga na wengine (bila kujali ni kwa nini umeamua kufanya hivyo!) huo ni usaliti! wala hatutaki kusikia na kupima hoja zako, una hoja gani msaliti wewe! toka lini msaliti akawa na hoja? wewe umemua kuwasaliti wazalendo, peleka unafiki wako kule msaliti mkubwa wewe!

Unapoamua kutusifu au kututetea tutee wakati wote, ukimtetea au kumsifu mtu mwingine, kimsingi wewe ni msaliti tena nafiki tu wewe! kama hujanunuliwa mbona umebadilika! eti unajifanya una vijihoja na unaleta viji-thread vyako hapa, msaliti mkubwa wewe! na unatumika tu wewe na wala hatuna haja ya kuzijua hoja zako maana umekwamisha harakati za ukombozi khaa! hebu kafie mbali huko!.

Tunasema hatuwezi kuwavumilia wasaliti wachumia tumbo hawa wanaotuletea ujinga ujinga! na waende zao huko maana wanakwamisha mapambano! Alaah!

Ni mawili: Ama mwezi mchanga kwa mleta mada, Au 'hoja ya ndoto' ya Descartes. Kama ni mwezi mchanga, Tutakuwa tuko salama kwani utapita tu muda si mrefu ila kama ni hoja ya ndoto ambapo Descartes anajaribu kutafakari kwamba 'ikiwa wakati unaota ndoto unakuwa haujui kwamba unaota hadi utakapozinduka usingizini, na wakati fulani unaweza ukawa unahisi kwamba uko katika ulimwengu halisia kumbe unaota, je ni kwa vipi unapofanya kitu unaweza kuwa na uhakika kwamba hauko ndotoni?'. Kwa sababu hiyo basi, ikiwa ni ndoto, sina uhakika kama tuko salama vya kutosha!, ni suala la wewe tu, kujiridhisha kama uko dhahiri na unachokiona, unachokisoma, unachosimuliwa, unachokisikia sikia na sio ndoto ambayo itaisha tu utakapoamka!.
 
Unaweza kukirudia vizuri ulichoandika? Ama ndio una mwezi mchanga?

ACT inakupoteza kijana...
 
betlehem

Si unaona yanayomkuta mwenzio Deogratius Kisandu?
Hauwezi kisaliti Mageuzi matakatifu ya Mungu na ukabaki Salama.
Ni kama ya Yuda Eskariote.
Wasaliti wotr lazima mtalipiziwa hapa hapa Duniani.
 
Last edited by a moderator:

Vp ACT mnaendeleaje? Katiba yenu itakuwa tayari lini?
 
betlehem
Hauwezi kisaliti Mageuzi matakatifu ya Mungu na ukabaki Salama.
Ni kama ya Yuda Eskariote.
Wasaliti wotr lazima mtalipiziwa hapa hapa Duniani.
Ni kweli kabisa ndugu yangu na ndicho ninachokizungumzia Mkuu, yaani unakuta mtu anasaliti kabisa mageuzi ya Mungu mwenyewe!? au anahoji hoji? yaani unajiuliza mtu huyo anapata wapi mamlaka ya kuhoji mambo yanayotokana na mungu, unashindwa kuelewa kabisa
 
Aisee umeandika nini? Hata sijaelewa...

Too much yaan nilishika concept ya kwanza ikapotelea njiani.nnalokumbumbuka kama pia nyie wasafi ruhusuni kukaguliwa nimeona ukitetea wasaf wasaf watu wataproove vip kuw waz naona una mtizamo mzuri ila shida ni mpangilie wa mawazo
 
Na wewe naona hujaelewa kama mimi tu
 
maandiko yako siku hizi yanadharaulika,jiulize kwanini!!!!
kama ulikuwa unaniheshimu kwa kuwa niliwakosoa wale usiowapenda, na sasa umeamua kunidharau kwa kuwa nimekukosoa na wewe vile vile, na kwa kuwa sikumkosoa niliyemkosoa kwa kuwa simpendi au wewe humpendi, na kwa kuwa sikukosoi kwa kuwa sikupendi bali yote ninayafanya kwa kuzingatia 'Facts' je! ungeshauri nifanye nini ili uniheshimu? je haufikiri kwa kufanya hilo unalotaka wewe ili uniheshimu , kutawafanya wengine nao wanidharau? je! hilo ambalo unataka nilifanye ili niheshimike, wewe ushalifanya tayari? kama ushalifanya, umeheshimika kwa kiasi gani?

Tafakari.
 
ACT lazima mtasalitiana tu! Kisandu alisaliti CDM akaenda NCCR akasaliti yuko njiani kwenda ACT mwisho atatua CCM.
 
Mkuu! usaliti ni nini? maana sasa naanza kujiridhisha kwamba kuna maneno ambayo watu wanayaimba humu huku wakiwa hawajui maana yake. By the way sasa kwa mchango uliotoa hapa umesaidia nini na kwa nani?

Usikae ukafikiri kwamba wewe huna wajibu kwako mwenyewe, kwa jamii yako na kwa nchi yako bali kuna mtu fulani yuko mahali; yeye ndio ana wajibu juu yake mwenyewe, kwako wewe, kwa jamii yake na kwa taifa kwa ujumla.Fikra hizo si sahihi na kinyume chake ndio sahihi.Ni bora kubadilika ukiona inafaa kufanya hivyo.
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu na ndicho ninachokizungumzia Mkuu, yaani unakuta mtu anasaliti kabisa mageuzi ya Mungu mwenyewe!? au anahoji hoji? yaani unajiuliza mtu huyo anapata wapi mamlaka ya kuhoji mambo yanayotokana na mungu, unashindwa kuelewa kabisa
Unaandika kwa kejeli...lakini angalia kwa umakini tu utatambau...usaliti unaozungumziwa na watu hapa kwenye jukwaa ni wa kuwauza watu..watu mnapanga mikakati mtu anaenda kuiuza kwa kuahiiwa kitu...wewe unataka kuwaaaminisha watu wanaokosoa ndo wanaonekana wasaliti la hasha... jiongeze zaidi
 
Mfano zitto kasaliti nini? Haya twende kwa hoja objective na vielelezo, yale majibu ya nasikia, sijui iko wazi, sijui watu wote wanajua, majibu ya namna hiyo ndio yanatuletea sida wakati wote.
 
Back
Top Bottom