Usalama wa Taifa Someni hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usalama wa Taifa Someni hapa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAZETI, Nov 21, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Sijui kama ni watu mnaoshaurika, ingawa nafahamu wazi kuwa tunakuwa pamoja katika majukwaa mbalimbali.

  Ndani ya nchi yetu kuna tishio la Al- Shababb.

  Ninachokiona hapa ni kuwa tishio litakuwa kubwa zaidi iwapo mpango wa Odinga kuomba msaada wa Kijeshi kwa Israel utafanikiwa. Kuingia kwa Waisrael ndani ya Somalia eti kwa Lengo la kuwasaidia wakenya kitakuwa kivutio kwa maadui mbalimbali wa Israel ambao ni wengi sana na ni suala linalofahamika. Hiyo itakuwa ni moja ya sababu za kuiingiza nchi yetu kwenye machafuko hayo ambayo tusipokuwa makini yatasambaa A.Mashariki.

  Tunachotakiwa kufanya ni kutokubali kabisa kujiingiza kwenye mzozo huo ambao tusipozingatia utatuingiza kwenye machafuko ambayo yatazidi kuharibu uchumi
  wetu ambao tayari yamekwishaharibika pia ule wimbo wa Nchi yenye AMANI hautaimbwa tena.

  WASIWASI WANGU
  Kuna uwezekano mkubwa Mataifa ya Magharibi (Hususani Marekani) au Israel, wakalipua moja katika maeneo ya nchi yetu na kuwasingizia AL Shabab ili wapate kisingizio cha kuiingiza Tanzania kwenye mgogoro huo wa aina yake

  USHAURI WANGU
  Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwa Idara kuunda kitengo maalum ambacho kitakuwa na kazi maalum ya kutafakari kwa kina jambo lolote linalotokea namna ya kuliendea n.k Kitengo hicho kiwe na watu wenye uwezo nzuri wa kufikiri na kushauri juu ya masuala nyeti ya nchi na si kuwaachia wanasiasa waamue wanavyotaka.

  Mwambieni ndugu A.C aunde special department ya watu wenye akili ambao wataweza kutushauri pale Wamarekani na mataifa mengine korofi wanapotaka kuturubuni kwa jambo lolote.

  GAZETI (P.I)
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja!

  Niemeona vitu viwili hapa ... Ulinzi ni zaidi ya AKILI (Ulinzi wa Taifa Kiakili) na Ulinzi ni UTU na HEKIMA pia! (Ulinzi wa Taifa Ki Utu na Ki hekima)
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri sana. Lakini kama hujagundua tatizo la taifa letu ni kutofuata ushauri wa kitaalam. Itaundwa tume, na kuja na mawazo mazuri tu. Mwisho wa siku wahusika watajifanyia madudu yao!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa!marekani wanaenda uganda na israel wanaenda kenya hao wote wauaji wakubwa tena wanaua kwa ndege zisizo na rubani.tanzania tunahitaji busara sana ktk kukabiliana nao
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tumejihusisha uswaiba na Amerika,tuwe tayar kwa vyandarua vyao na Fitna zao
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  alshababu na maharamia wengine ni maadui na magaidi na wanapaswa kudhibitiwa at any cost.kama tulipeleka majeshi msumbiji kumsaidia rafiki sioni kwanini tusiwasaidie wana EAC wenzetu.maharamia hawa wanateka meli zenye madawa huwezi ukasema tuwaache eti kwa kuogopa mashambulizi ya mabomu.majangili wa kisomali waliwahi kutusumbua huko ngorongoro na jeshi letu liliweza kuwadhibiti tupunguze uwoga.
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Nafikiri wewe ndio umegoma kuushirikisha ubongo wako, hatuhitaji kitengo maalum kwa hili kwani misikiti yote ambayo ni maficho ya Al shabaab inajulikani na tumeshairipoti na tumeweka thread hapa kuitaja wazi wazi misikiti hiyo kwa majina, kwahiyo sahau hilo unalopendekeza, usidhani Usalama wa Taifa hawafanyi kazi, wanafanya kazi sana hila tatizo pale magogoni hawashauriki.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kama ni sisi wenyewe tutajilinda sawa lakini si usa au israel watusaidie
   
 9. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kutoshaurika kwa magogoni hilo liko wazi kabisa.
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  sawa kabisa mkuu na wao walishasema wewe ni rafiki yetu na pia ni adui yetu vile vile..
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  umeona mbali gazeti, lakini kama hatujaweza kutatua migogoro inayofukuta ndani ya nchiyetu kwa sababu ya katiba, sidhani kama hili la kwako litawezekana iwapo watu/mataifa mabaya yataamua kutufanyia kitu kibaya.

  Kama viongozi wetu wanashindwa kuanzisha mchakoto huru ndani ya nchi, je nje ya nchi wataanzia wapi?
   
 12. Qulfayaqul

  Qulfayaqul JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 471
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tumekwisha kwa jinsi walivyokuwa na usongo na sisi hasa baada ya kukataa sera za kimagharibi sijui kama kutakuwa na usalama.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Hujui ulisemalo, ni sera gani tulizozikataa? hujui kwamba Uranium yetu tayari ni ya Wamaekani tumebadilishana nao kwa vyandaruwa? na unajifanya hujui kwamba Barrick ni kampuni ya nchi za Magharibi? hujui kinachoendelea kigamboni? na hujui gesi ya songosongo ananufaika nayo nani? na haujui kwamba Richmond sasa ndio inaitwa symbion power na inakula pesa zetu kama kawa?
   
 14. k

  king11 JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nadhani imefika wakati Tanzania ikachagua upande wa kuwa nao mshirika kati ya pande za magharibi au upande wa mashariki ambao unaongozwa na china na mataifa mengine ya Asia . kuendelea kuwa katika kundi lisilofungamana ni kitu cha kupoteza muda tu
   
 15. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  :A S 13::A S 13::A S 13:....................................Napita tu,
   
 16. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  "Sera za Magharibi", maana yake "David Cameron"?:puke:.... Mungu na aepushe mbali..!!!
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu GAZETI. Kwa mtu makini anaposoma hoja yako anagundua wewe siyo kwamba unaipenda sana Tanzania na haupendi ishambuliwe na magaidi wa Al shabab bali wewe una chuki dhidi ya Marekani na Israel.
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  king11 katika dunia hii mataifa karibia yote hayana urafiki wa kudumu. Tena haya makubwa yakiwemo hayo ya mashariki wanaangalia maslahi ya kiuchumi,biashara na wakati fulani ulinzi(kijeshi)
   
 19. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  There are currently 84 users browsing this thread (23 members and 61 guests)
   
 20. n

  ngokowalwa Senior Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamhuri ya watu wa Kenya tofauti na JMT (URT) ina uhusiano na mataifa hayo miaka nenda rudi, hivyo tuwaache wafanye kile wanachoona kitanufauisha taifa lao. Nasi tuendeleeni na sera zetu bila kusahau kulinda mipaka yetu kuzuia wahalifu majangili wa kupora maliasili zetu ( kama wanyama pori ) maeneo ambayo tumeonyesha udhaifu mkubwa kama hatuna uwezo wa kudhibiti vitu kama hivi basi ni vyema tukaomba moja ya nchi marafiki zetu yenye uwezo katika hizo nyanja na isiyo na maadui wengi duniani ije itusaidie .
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...