usalama wa majaji na mahakimu wetu shakani

usalama wa majaji na mahakimu wetu shakani

Dogo1

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,356
Reaction score
580
Ndugu wana JF siku moja niliitikia wito wa mahakama kwenda kutoa ushahidi mbele ya mheshimiwa hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi.

Miongoni mwa tuliokua kwenye chumba cha mheshimiwa nilimuoana jamaa mmoja ambae alikua amebeba silaha ndogo (bastola) kiunoni. Nilipata mshangao hasa kwa kuzingatia usalama wa hakimu mwenywe na watu wengine ndani ya mahakama. Yule jamaa alikuwa amefika mahakamani pale kutoa taarifa kwamba mtuhumiwa hakuweza kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa.

Nimelileta hili ili tulitafakari kwa kuzingatia kwamba dunia imebadilika so hata utaratibu wa ulinzi na usalama unatakiwa uendane na mabadiliko ya dunia.
 
we ulijuaje kama ile bastola ilikuwa kwa ajili ya hakimu au nawewe ulihusika kwenye huo mpango.
 
we ulijuaje kama ile bastola ilikuwa kwa ajili ya hakimu au nawewe ulihusika kwenye huo mpango.

ndugu Billie, nadhani hukunielewa. Concern yangu ni kwamba kuingia na silaha ya aina yeyote kwenye chumba cha mahakama kunahatarisha usalama ndani ya mahakama. Yule jamaa aliingia na bastola, inawezekana hakua na nia mbaya but kusipokua na udhibiti kuingia na vitu aina hiyo si salama kwa mtazamo wangu.
 
Kama alikuja kutoa taarifa ya mtuhumiwa kushindwa kufika mahakamani pengine ni Askari kanzu kutoka magereza. Lakini unaangalia suala zima la watu kuingia mahamani na silaha, Askari wanaruhusiwa kuingia nazo, lakini na wenyewe Siku hizi mbona wamekupa fyatu, lolote linaweza kutokea
 
Hata mimi mtoa mada sijamwelewa, kwa sababu huyo aliyekuwa na silaha hujafanya kautafiti kidogo kujua alikuwa askari au mtu baki, halafu analeta hofu hapa barazani. Nijuavyo mimi kati ya vitu vinavyotakiwa kuwepo mahakamani ili kesi ziendeshwe ni ulinzi. Na siku zote polisi na wale wa magereza wanakuwepo. Nakushauri mtoa mada uwe unaleta vitu vya uhakika si kukurupuka tu maadamu eti umeona silaha. Silaha kuonekana mahakamani si hoja, hoja ni silaha hiyo ina nani.
 
kama wanatoa hukumu ya haki hakuna hatakayewagusa
 
Hata mimi mtoa mada sijamwelewa, kwa sababu huyo aliyekuwa na silaha hujafanya kautafiti kidogo kujua alikuwa askari au mtu baki, halafu analeta hofu hapa barazani. Nijuavyo mimi kati ya vitu vinavyotakiwa kuwepo mahakamani ili kesi ziendeshwe ni ulinzi. Na siku zote polisi na wale wa magereza wanakuwepo. Nakushauri mtoa mada uwe unaleta vitu vya uhakika si kukurupuka tu maadamu eti umeona silaha. Silaha kuonekana mahakamani si hoja, hoja ni silaha hiyo ina nani.

Sijakurupuka ndg, nadhani wewe una tatizo kwenye ubongo wako! Kwanza kabla ya kutoa mawazo yako ulikua na haki ya kuuliza zaidi upate kuelewa.

Mazingira ya mahakama nayaelewa coz nimeshafika so many times. Niliyemuona na silaha kiunoni hakua askari. Ninaelewa ninachokiongelea hapa. Changia hoja kama huna cha kuchangia si lazima.
 
Kufika mara nyingi si hoja, unaweza kufika na usielewe. Wadau wanachochangia ni kile ulichokiandika na ndo maana tunakwambia umekurupuka otherwise ungeeleza yote watu wakuelewe.

Back
Top Bottom