Usalama UDART uangaliwe upya

Usalama UDART uangaliwe upya

kabwigwa

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
933
Reaction score
1,543
Wakuu habari,najaribu kuthink out loud kuhusu suala la usalama katika Mabasi ya mwendokasi (UDART)kuanzia vituoni mpaka ndani ya mabasi.

Kama mnavyojua suala la ugaidi hutarget zaidi maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama kwenye Mall au kwenye masoko na vituo vya mabasi.

UDART mbali ya kuchemka kuuendesha mradi suala la ulinzi wamefeli kabisa.Tangu mradi umeanza hakukuwa na jitihada zozote za kuimarisha ulinzi.

Hakuna Security door scanner,wala hand held metal detactors(kama zipo basi wale walinzi wenu wa China Tanzania Security wanakaanazo tu kama mapambo),ingawa kwa wingi ule wa watu security door scanner ndizo zinazofaa.Tunaamini Tanzania ipo shwari but Waswahili husema ‘tahadhari kabla ya hatari’.

Kwa hali ilivyo sasa hata kama abiria ana bomu au silaha yoyote ile anapita nayo bila kugundulika.

Ninakuomba waziri Kangi Lugora tusaidie kwa hili,ukisema litafanyiwa kazi.

Alamsiki
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Ni kweli Mkuu maana ulinzi wetu bado sana hatujachukua tahadhari ya kutosha
 
Hatujafikia huko bado... Tanzania ni nchi ya amani na utulivu... ingawa kuna wachache wanataka kuitia doa...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom