Usajili wasogezwa mbele kwa siku mbili

Usajili wasogezwa mbele kwa siku mbili

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
Wakati TFF ilikuwa ifunge usajili wa Ligi Kuu Bara usiku huu, taarifa inasema siku mbili zimeongezwa.

Kuna taarifa Shirikisho hilo limeamua kuongeza siku mbili za usajili sasa utafungwa tena Ijumaa saa 6 usiku.

"Kuna taarifa kwamba usajili umesogezwa mbele, tumepata taarifa kupitia simu," alieleza kiongozi mmoja wa klabu usiku huu.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa tayari Yanga na Simba zilishawasilisha majina ya wachezaji wao watano wa kigeni.

Yanga iliwasilisha majina ya Wanyarwanda wawili (Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima), Wabrazil wawili (Jaja&Coutinho) na Hamis Kiiza huku ikiwa imemtema Okwi.

Wakati Simba iliwasilisha majina ya Wakenya wawili (Modo Kiongera&Donald Musoti), Warundi wawili (Amissi Tambwe&Peirre Kwizera) na Mganda, Joseph Owino.

Bado haijajulikana sababu hasa za TFF kuamua kusogeza mbele kwa siku mbili usajili huo.
 
Wamesema sababu zipi zilizofanya waongeze na nani katoa taarifa hizo
 
Hii itakuwa sinema ya Okwi tu ndo imesabishwa yote hayo.
 
Pamoja na hayo usajili wa kimataifa bado unendelea lakini wa ndani ndo ulitakiwa umalizike hiyo jana saa 6 usiku lakini pia habari nyingine ni kwamba wamefanya hivyo ili timu moja kubwa sio yanga wala simba imchukue mchezaji mmoja ambae anakisiwa kuwa ameachwa na Timu moja wapo.
 
Musoti huyo, Azam wamesaidia hela ya kulipwa Okwi Simba
 
Back
Top Bottom