Usajili wa nyaraka wizara ya ardhi ni kero. Rushwa imezidi pale.Waziri Lukuvi tusaidie

Bulamba

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
13,193
12,379
Salaam wakuu.

Niende moja kwa moja katika mada.Nilitengenezewa "Power of Attorney" na mwanasheria wangu.Ikabidi niende Wizara ya Ardhi kuisajili.

Nilifika pale nikalipia 53,000 kama gharama ya usajili na nikaambiwa nije baada ya wiki mbili.Sasa hivi imeshapita miezi miwili na nimeshaenda pale mara saba bila mafanikio.Kila siku wanasema bado.Lakini utakuta watu wengine wanakuja na kupata usajili papo kwa hapo.Je tunatapeliwa pale?

Nasikia wafanyakazi wa pale kwa makusudi kabisa huweka nyaraka pembeni mpaka utoe pesa.Inauma sana mtu kupoteza pesa za kulipia usajili na usajili hupati na pia kupoteza muda kila siku wa kufatilia nyaraka.Mh. LUKUVI tupia jicho hiki kitengo.Kimejaa rushwa na ubabaifu.Fukuza watu wa pale waje wapya.

Asante # CCM MPYA
 
Salaam wakuu.

Niende moja kwa moja katika mada.Nilitengenezewa "Power of Attorney" na mwanasheria wangu.Ikabidi niende Wizara ya Ardhi kuisajili.Nilifika pale nikalipia 53,000 kama gharama ya usajili na nikaambiwa nije baada ya wiki mbili.Sasa hivi imeshapita miezi miwili na nimeshaenda pale mara saba bila mafanikio.Kila siku wanasema bado.Lakini utakuta watu wengine wanakuja na kupata usajili papo kwa hapo.Je tunatapeliwa pale?Nasikia wafanyakazi wa pale kwa makusudi kabisa huweka nyaraka pembeni mpaka utoe pesa.Inauma sana mtu kupoteza pesa za kulipia usajili na usajili hupati na pia kupoteza muda kila siku wa kufatilia nyaraka.Mh. LUKUVI tupia jicho hiki kitengo.Kimejaa rushwa na ubabaifu.Fukuza watu wa pale waje wapya.

Asante # CCM MPYA
 
Inakuwaje kichwa cha mada unaandika wizara ya kazi wakati hoja yako inahusu wizara ya ardhi?
 
Ukiwa na kero kwenye wizara zinazoongozwa na mawaziri wajanja walio ndani ya JF. jaribu kutaja maafisa waliokukera ili kesho yake upate huduma nzuri.
Mawaziri wajanja unawajua, yaani hawa mayanki wale walio archives kina mahasira achana nao
 
Salaam wakuu.

Niende moja kwa moja katika mada.Nilitengenezewa "Power of Attorney" na mwanasheria wangu.Ikabidi niende Wizara ya Ardhi kuisajili.Nilifika pale nikalipia 53,000 kama gharama ya usajili na nikaambiwa nije baada ya wiki mbili.Sasa hivi imeshapita miezi miwili na nimeshaenda pale mara saba bila mafanikio.Kila siku wanasema bado.Lakini utakuta watu wengine wanakuja na kupata usajili papo kwa hapo.Je tunatapeliwa pale?Nasikia wafanyakazi wa pale kwa makusudi kabisa huweka nyaraka pembeni mpaka utoe pesa.Inauma sana mtu kupoteza pesa za kulipia usajili na usajili hupati na pia kupoteza muda kila siku wa kufatilia nyaraka.Mh. LUKUVI tupia jicho hiki kitengo.Kimejaa rushwa na ubabaifu.Fukuza watu wa pale waje wapya.

Asante # CCM MPYA
mimi ilinikuta hiyo mpaka nikaachana na hilo suala,mara signature zinarofautia na copy iliyopo kwetu mara leta kiapo kiapo kikaja mara hakijaswii, ni wapuuzi mno,mpaka nikaachana na hiyo kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kulalamika chukua Hatua.
Kila ofisi ina bosi. Waone mabosi wao.

Hata Hivyo hakuna ofisi isiyo na Rushwa na usumbufu. Haipo Afrika.
Afrika tumetengeneza maisha magumu wenyewe kwa kuwakumbatia wanasiasa na watawala wale wale waliotuwekea sheria ngumu na zenye usumbufu.

Watu hao hao walioondoa taa na kuleta giza ndio wanageuka kuwa watoa nuru.

Jiulize ni kwa nini wasiweke Ramani za mipango yao Kila Ofisi za Vijiji na mitaa nchi nzima ili kila MTU aone na ajue ardhi anayomiliki ni halali na haina mgigoro.? Baada ya hapo Kila kitu kianzie Kijijini ,au kwenye mtaa na iishie Wilayani na Hati itolewe ya Kielekroniki kama ilivyo Risiti za Kielekroniki na zilivyo Hati ya Namba ya Mlipa Kodi na Kadi ya Gari.
Kwa mfano tu Huwezi kutoa kadi ya Gari Mara Mbili bila kujua kuwa lina mmiliki Mwingine.

Kwa nini TRA wana machine Karibu nchi Nzima za kutoa Hati za Kielekroniki za Magari na Namba za mlipa kodi ,lakini Wizara ya Ardhi yenye umuhimu kwa kila mwananchi Hati za kumiliki Ardhi zinakua nalolongo mrefu na hazipo Kielekroniki na bado Waziri anazunguka zunguka kuwa mahakama. Kuna tatizo sana.
Wenye viwanja vingi,mashamba makubwa Mengi ni hao hao waliopo Wizarani na ndugu zao na wafanyakazi hao hao.

Tatizo ni kwamba watendaji wamegeuka kuwa wanasiasa na wafia vyama . Hakuna Mwanasiasa anayesimama kwa miguu ya Chama Chochote mwenye nia njema kwa Taifa lake. Hayupo duniani labda itakapotokea Mgombea Binafsi kwenye Katiba ya Waroba endapo atatokea Kiongozi Mzalendo wa kweli na anayejua kuwa Mungu alipomuweka kila binadam hapa duniani alimuweka kwenye ardhi hii hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom