Usajili wa Mrisho Ngasa

Usajili wa Mrisho Ngasa

Unachosema ni sawa lakini kama kuna viongozi ambao uamuzi wao hauongozwi na kanuni zilizopo hata kama wangekopi taratibu za ulaya mambo kama haya yataendelea tu kuwepo.
!

Unalosema pia ni sawa, lakini linatupeleka kwenye mjadala mwengine mpya: tutawapataje viongozi wanaotoa maamuzi yao kwa mujibu wa kanuni, ikizingatiwa kwamba wadau wote wa mpira nchini (wakiwemo wa Azam) ni wadau wa Yanga ama Simba? Wenzetu walioendelea hawana tatizo hilo kwa sababu timu zao hazina wanachama. Zina washabiki tu, nazo zimeegemea kwenye miji ziliko. Hata majina yao yanaashiria hivyo: Dynamo Zagreb, Manchester City/United, Inter/FC Milan, Bayern Munich, Real (kwa maana ya Royal kwa Kispaniola)/Atletico Madrid, Liverpool, Arsenal (yote ni mitaa ya London ambayo kwa ukubwa wake ni vigumu timu moja kujinasibisha na London nzima) n.k. Kwa hivyo timu za huko zimegawana wapenzi kwa mujibu wa wakaazi wa miji zilioko. Isipokuwa kwa wahamiaji kutoka Madrid, ni nadra kuwakuta watu wa Barcelona wakishabikia Real Madrid, wa Arsenal hawashabikii Manchester United, Bayern haishabikiwi Hamburg, n.k. Kwa hivyo siasa za mpira wa Uingereza hazitawaliwi na Arsenal wala Man U, za Ujerumani hazitawaliwi na Bayern, za italia hazitawaliwi na Juve (ingawa ina historia ya upendeleo kidogo kwa sababu conservative Italians wanaamini ukoo wa Angeli unaomiliki timu hiyo ni Warumi hasa ambao jumla yao Italia nzima haipindukii laki moja). Huku kwetu wakaazi wa Mwanza wanapenda Yanga au Simba kwanza kabla ya Toto au Pamba, wa Moro pia wanapenda kwanza Simba/Yanga kuliko Mtibwa, n.k.
tatizo jengine ni kanuni ya msingi ya FIFA ya kuepuka mgongano wa kimaslahi katika uendeshaji shughuli za mpira. Yeyote mwenye maslahi na swala fulani anapaswa kulitangaza hilo kwanza kabla ya kikao kinachojadili jambo lenye maslaha hayo. Kwa hivyo Wambura, Rage na Kaduguda walipaswa kujitoa kwenye vikao vyote vilivyoijadili Simba wakiwa makatibu wakuu wa FAT, Tenga ajitoe yanapojadiliwa maswala ya Yanga na Pan. Lakini katika ushindani wa timu hizo kuhakikisha kila moja inaingiza wadau wake wengi kuliko mwenzake kwenye Kamati Tendaji ya TFF, akidi (qorum) itapatikana iwapo kila M-Yanga ajitoe inapojadiliwa Yanga, na M-Simba ajitoe inapojadiliwa Simba? Nionavyo, hilo ndio tatizo la msingi.
 
Kama Ngasa hakuruhusiwa kusaini mkataba na Simba lakini hali akijua hivyo akaingia mkataba na Simba na akachukua pesa bado ana kosa la kujibu ambalo ni kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Hapo umesema. Simba wakiri kuwa walifanya makosa kumsajili Ngassa kinyume cha kanuni. Aidha Ngassa hakujipatia fedha kwa udanganyifu kwani yeye hakuomba/haku-solicit bali Simba walimrubuni na sasa wanavuna walichopanda. Sheria ukiijua ina raha yake. Hivi Simba haina Wanasheria wa kuwashauri?
 
Arsenal v Liverpool (Suarez) na Chelsea v Man United (Rooney); hizi issues unazionaje Mkuu?

Swala la Suarez na Rooney Sio sawa na swala la Mrisho Ngasa! Ngasa amesajiliwa na timu2. Suarez ni mchezaji halali wa Liverpool na Rooney ni mchezaji halali wa Man Utd na wote hao hawajasajili katika vilabu viwili Kama Ngasa!
 
Back
Top Bottom