Usajili wa Mrisho Ngasa

Usajili wa Mrisho Ngasa

Hivi mtu akisema leo si Nanenane, kuna haja ya kukanusha? Ngassa hakuwa na haja ya kukanusha kwa sababu hakukuwa na haja ya kukanusha jambo lililo uongo wa dhahiri.Sheria gani ya FIFA, CAF,CECAFA au TFF inayoruhusu kupandishia mkataba wa aina hiyo? Kwanza timu yoyote haipaswi kuongea na mchezaji mwenye mkataba mpaka ibakie miezi sita ya kuumaliza. Simba wamekopeshwa Ngassa kukiwa na zaidi ya mwaka kabla ya (mkataba) kuisha. Watakiukaje sheria kumsaini hivyo? Inaonesha Simba wanakosea tafsiri ya neno 'loan" kwenye mwaswala ya wachezaji. Tafsiri sahihi ya 'loan' si mkopo. Ni kuazimwa. Ndio maana mchezaji wa aina hiyo huwa anaendelea kulipwa na klabu yenye mkataba naye. Labda Rage alidhani wamekopeshwa kama yeye anavyokopa pesa benki, anaweza kuzifanya apendavyo, madhali atazilipa. Kwani Simba ilitakiwa kuilipa Azam baadaye kwa kumchkua Ngassa? Huo ungekuwa ndio mkopo kwa maana ya Kiswahili ya neno hilo. Simba wasijidanganye, wakawadanganya na Watanzania wenye desturi ya kumwamini kila mtu.
Mkuu hivi ni kawaida mchezaji akipelekwa timu nyingine kwa mkopo timu aliyotoka inapewa hela na yeye pia anapata hela? Kama hiyo haitoshi je ni sahihi mchezaji anayecheza kwa mkopo kulipwa na timu anayoichezea au anaendelea kulipwa na timu inayommiliki?
 
sheria zifatwe, soka la tz sio ngasa au simba na yanga
 
Mkuu hivi ni kawaida mchezaji akipelekwa timu nyingine kwa mkopo timu aliyotoka inapewa hela na yeye pia anapata hela? Kama hiyo haitoshi je ni sahihi mchezaji anayecheza kwa mkopo kulipwa na timu anayoichezea au anaendelea kulipwa na timu inayommiliki?
Nani amlipe mchezaji wa mkopo baina ya timu yenye mkataba naye na iliyoazimwa, ni makubaliano ya timu mbili hizo. Nini timu inayoazimwa mchezaji iilipe timu yenye mchezaji ni makubaliano yao, lakini si fedha ya kumnunua. la sivyo huyo mchezaji asingeambiwa ameenda kwa mkopo. Hili lisitofautishwe na mchezaji kuuzwa (sio kupelekwa) kwa mkopo, ambapo timu inayopokea mchezaji inaweza kuilipa timu inayouza mchezaji kwa awamu. ndivyo inavyotaka Real Madrid kwa Tottenham kuhusu Bale. Nje ya makubaliano hayo, malipo mengine yoyote baina ya timu iliyoazimwa na mchezaji ni makubaliano ya kiungwana, gentlemen's agreement, ambayo hayana mashiko kwenye mustakbali wa timu hiyo na mchezaji mbele ya chama husika cha mpira. Kwa maneno mengine, kunaweza kukawa na kulipana pesa baina ya Ngassa na Simba kwa nia ya kuendelea kuichezea Simba baada ya mkataba wake wa Azam kumalizika. Lakini makubaliano hayo ni kifunga-uchumba tu, si mahari wala sio ndoa. Kisheria ni kama MoU, hati ambayo kisheria haina nguvu za kimkataba. Kwa hivyo TFF si mahala sahihi pa Simba kupeleka malalamiko yao. Wanapaswa kufungua kesi ya madai Mahkamani ambako wakishinda, Ngassa anaweza kutakiwa kurejesha hicho kifunga-uchumba, na hata ziada kutokana na usumbufu alioipa Simba kwa kuipotezea muda na kuinyima fursa ya kupata mchezaji mbadala anayelingana na fedha waliotanguliza au anayelingana na Ngassa mwenyewe. Nje ya hivyo ni ku-boogie step.
 
Inaelekea jibu la sakata la Ngasa linaanza kupata majibu. Kufuatana na habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Citizen, Simba wamepeleka mkataba pekee wakati Yanga wamepeleka mkataba pamoja na fomu yenye taarifa za mchezaji ambayo Ngasa aweka sahihi yake. Kwa maana hiyo, makabrasha ya Simba hayajakamilika kama sheria na taratibu za TFF zinavyotaka.

Angalia link hii:

Simba
 
Hapa simba tumeliwa. Maana tumebaki na jina na wao Yanga wamebaki na mchezaji.
 
Nani amlipe mchezaji wa mkopo baina ya timu yenye mkataba naye na iliyoazimwa, ni makubaliano ya timu mbili hizo. Nini timu inayoazimwa mchezaji iilipe timu yenye mchezaji ni makubaliano yao, lakini si fedha ya kumnunua. la sivyo huyo mchezaji asingeambiwa ameenda kwa mkopo. Hili lisitofautishwe na mchezaji kuuzwa (sio kupelekwa) kwa mkopo, ambapo timu inayopokea mchezaji inaweza kuilipa timu inayouza mchezaji kwa awamu. ndivyo inavyotaka Real Madrid kwa Tottenham kuhusu Bale. Nje ya makubaliano hayo, malipo mengine yoyote baina ya timu iliyoazimwa na mchezaji ni makubaliano ya kiungwana, gentlemen's agreement, ambayo hayana mashiko kwenye mustakbali wa timu hiyo na mchezaji mbele ya chama husika cha mpira. Kwa maneno mengine, kunaweza kukawa na kulipana pesa baina ya Ngassa na Simba kwa nia ya kuendelea kuichezea Simba baada ya mkataba wake wa Azam kumalizika. Lakini makubaliano hayo ni kifunga-uchumba tu, si mahari wala sio ndoa. Kisheria ni kama MoU, hati ambayo kisheria haina nguvu za kimkataba. Kwa hivyo TFF si mahala sahihi pa Simba kupeleka malalamiko yao. Wanapaswa kufungua kesi ya madai Mahkamani ambako wakishinda, Ngassa anaweza kutakiwa kurejesha hicho kifunga-uchumba, na hata ziada kutokana na usumbufu alioipa Simba kwa kuipotezea muda na kuinyima fursa ya kupata mchezaji mbadala anayelingana na fedha waliotanguliza au anayelingana na Ngassa mwenyewe. Nje ya hivyo ni ku-boogie step.
Mkuu mimi sio mfuatiliaji sana wa usajili hasa wa nje hasa ulaya, je scenario kama hii ulishawahi kuisikia popote zaidi ya Ngasa na Azam na Simba? Kama kweli makubaliano ya awali hayana nguvu kwa mujibu wa kanuni za TFF na kwa maelezo ya katibu mkuu wa TFF (nimesikia leo star tv) kwamba kama karatasi hazijakamilika basi usajili huo ni batili (hapa inaonekana kama ni mkataba tu na hakuna fomu mama) je wachezaji hawawezi kutumia hiyo loop hole na kujinufaisha, anasaini mkataba timu nyingine, halafu ataenda timu nyingine tena anasaini mkataba na kusaini fomu mama hivyo timu ya kwanza inakuwa imeliwa? Na je ile kanuni ya kwamba mchezaji akisajili timu mbili anafungiwa mwaka mmoja ni wakati gani hutumika, anaposaini tu mkataba kwa timu mbili tofauti au hadi amalizie na zile fomu mama kwa timu mbili tofauti? Au hadi usajili wake uidhinishwe na TFF kwa timu mbili tofauti? Au niulize hivi ni wakati gani mchezaji atahesabika kwamba amesaini timu mbili tofauti?
 
Kwa ligi ya kulipwa ambapo mchezaji huingia mkataba na timu, usajili hukamilika baada ya mkataba uliokamilika kuwasilishwa chama husika cha mpira. Kinachotokea Tanzania ni kwamba usajili hufanyika kila mwaka hata kwa mchezaji mwenye mkataba wa miaka mingi na timu, jambo ambalo halifanyiki Ulaya. Huko hufanyika usajili pale tu mchezaji anapoingia mkataba mpya na timu, au timu zinapobadilishana mchezaji kwa mkopo. Kwa namna hiyo, junakosekana uwezekano wa mchezaji kusajili zaidi ya timu moja, kwa kuwa mkataba huwasilishwa chama cha mpira wakati wowote unapokamilika. Uwazi katika kusajili (unasikia harakati za usajili Ulaya) nao huondoa usiri kama huu wa Simba na Ngassa.
kwa ufupi, mkataba hukamilika pale unapotiwa saini na pande mbili na kisha kubarikiwa na chama cha mpira cha nchi husika.
 
gazet la leo la mwananch limelipot kuwa tm ya simba imeolodhesha jna la ngasa kama mchezaj watakae m2mia mcm ujao.je ngasa n mchezaj wa tm gan kwel bongo no
 
Kwa ligi ya kulipwa ambapo mchezaji huingia mkataba na timu, usajili hukamilika baada ya mkataba uliokamilika kuwasilishwa chama husika cha mpira. Kinachotokea Tanzania ni kwamba usajili hufanyika kila mwaka hata kwa mchezaji mwenye mkataba wa miaka mingi na timu, jambo ambalo halifanyiki Ulaya. Huko hufanyika usajili pale tu mchezaji anapoingia mkataba mpya na timu, au timu zinapobadilishana mchezaji kwa mkopo. Kwa namna hiyo, junakosekana uwezekano wa mchezaji kusajili zaidi ya timu moja, kwa kuwa mkataba huwasilishwa chama cha mpira wakati wowote unapokamilika. Uwazi katika kusajili (unasikia harakati za usajili Ulaya) nao huondoa usiri kama huu wa Simba na Ngassa.
kwa ufupi, mkataba hukamilika pale unapotiwa saini na pande mbili na kisha kubarikiwa na chama cha mpira cha nchi husika.
Asante kwa ufafanuzi, lakini swali lako la mwisho halijapata ufafanuzi, ni kitu gani kitakachowaonyesha TFF kwamba mchezaji fulani amesajili timu A na pia amesajili timu B, ili kanuni yao ya kumfungia mchezaji kama huyo kwa muda wa mwaka mmoja iweze kutumika?
 
Iwapo mkataba wa mchezaji A na timu AA utawasilishwa chama cha mpira cha nchi husikamara tu baada ya kusainiwa baina yao, na iwapo utakuwa umekamilika, chama husika cha mpira hakitakuwa na sababu ya kutoubariki mkataba huo hapohapo. Ukishasajiliwa hivyo, na baadaye mkataba baina ya mchezaji huyohuyo A na timu BB ukawasilishwa kwa chama cha mpira cha nchi hiyo, utakataliwa kwa sababu tayari ilikwishamsajili mchezaji huyo na Timu AA (hata kama tarehe ya makubaliano na Timu BB yataonekana kwenye mkataba wao kuwa ulisainiwa mwanzo na timu BB Unaotambuliwa ni mkataba uliokamilika unaowasilishwa mwanzo kwenye chama cha mpira). Lakini hili ni nadra kutokea huko Ulaya kwa sababu wachezaji wa huko hawako na akili za ki-ngassa na viongozi wa vilabu hawana utoto wa ki-rage. Tatizo la TFF ni kusajili kila mwaka hata kama mchezaji ana mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja. Labda ni kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kiteknohama ambayo ndiyo inayofuatilia mikataba ya wachezaji mbalimbali waliosajiliwa tarehe tofauti kwenye chama cha mpira cha nchi husika.
 
Kama TFF kutaendelea kuwa na viongozi aina ya katibu mkuu wa sasa basi hii kanuni inatakiwa kufutwa kwa sababu haionyeshi uwezekano wa kuvunjwa, kama mkataba uliosainiwa na pande mbili wakiwepo na mashahidi lakini hauwezi kuwa valid mpaka uthibitishwe na TFF na TFF nao wanathibitisha mikataba na kuidhinisha na mapenzi yao kumbe basi hiyo kanuni ina maana gani.
 
Ngasa upeo mdogo angepambana awafuate Samatta na Ulimwengu sio kukaa kula chipsi chafu tmk.ovyoooo
 
uichukie Simba ama umchukie Rage hiyo ni kivyako. Ngassa kama kweli amesaini mikataba ya Timu zote mbili afungiwe kucheza soka kwa mwaka siyo kuangalia ni upande upi umekamilisha document kama alivyonukuliwa akisema Katibu wa TFF vivyohivyo kama viongozi wa Simba kama wamefoji signature ya Ngassa nao wafungiwe.
Mbona una hasira? Unataka wote tuipende simba?
 
Kama TFF kutaendelea kuwa na viongozi aina ya katibu mkuu wa sasa basi hii kanuni inatakiwa kufutwa kwa sababu haionyeshi uwezekano wa kuvunjwa, kama mkataba uliosainiwa na pande mbili wakiwepo na mashahidi lakini hauwezi kuwa valid mpaka uthibitishwe na TFF na TFF nao wanathibitisha mikataba na kuidhinisha na mapenzi yao kumbe basi hiyo kanuni ina maana gani.

mbona ni rahisi tu? Timu na mchezaji zifikie mkataba. Mkataba uwasilishwe chama cha mpira. Chama cha mpira kiuorodheshe mkataba huo na kuufuatilia muda wake wa kumalizika. Mchezaji aliyekwishawasilisha mkataba uliokamilika na kuorodheshwa hapaswi na hataweza kuwasilisha kwenye chama cha mpira mkataba na timu nyingine mpaka uliopo umalizike. Kwa utratibu huo, hata mimi na wewe tutaweza kusimamia, hakuna upenyo wa double registration.
 
Mbona una hasira? Unataka wote tuipende simba?
ahaa sina hasira bwana; ila nashangaa kuona wachezaji, wapenzi na viongozi wa soka la kibongo wanakua na ufinyu wa mawazo. Taratibu zipo wazi na ndo maana Sheria zimewekwa, mtu asiyetaka kuzifuata aadhibiwe. sakata la Ngassa ni ukiukwaji wa Sheria hivyo sioni kwanini tuanze kuumiza vichwa wakati adhabu zimeisha ainishwa kisheria. Anayesaini timu zaidi ya moja na ikabainika basi afungiwe kucheza mpira kwa mwaka mmoja. Na huo ndo UTAWALA WA SHERIA.
 
kweli kabisa lakini kwa TFF hii ninawasiwasi Simba imekula kwao labda waende mahakamani..
 
mbona ni rahisi tu? Timu na mchezaji zifikie mkataba. Mkataba uwasilishwe chama cha mpira. Chama cha mpira kiuorodheshe mkataba huo na kuufuatilia muda wake wa kumalizika. Mchezaji aliyekwishawasilisha mkataba uliokamilika na kuorodheshwa hapaswi na hataweza kuwasilisha kwenye chama cha mpira mkataba na timu nyingine mpaka uliopo umalizike. Kwa utratibu huo, hata mimi na wewe tutaweza kusimamia, hakuna upenyo wa double registration.
Unachosema ni sawa lakini kama kuna viongozi ambao uamuzi wao hauongozwi na kanuni zilizopo hata kama wangekopi taratibu za ulaya mambo kama haya yataendelea tu kuwepo.
 
Kama Ngasa hakuruhusiwa kusaini mkataba na Simba lakini hali akijua hivyo akaingia mkataba na Simba na akachukua pesa bado ana kosa la kujibu ambalo ni kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Simba walisahiri kwa ujinga kwani wakati Ngasa anatoka Azam kwa mkopo alikuwa amebakuza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake,hivyo basi sheria ya usajiri inasema kuwa huwezi kumsajiri mchezaji kutoka timu nyingine akiwa ndani ya mkataba unaozidi miezi 6.Simba hilo hawakulijuwa?
 
Back
Top Bottom