Usajili wa Mrisho Ngasa

Usajili wa Mrisho Ngasa

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,297
Reaction score
18,045
Inaelekea msimu huu kutakuwa na vute nikuvute kuhusu usajili wa mchazaji Mrisho Ngasa.

Maadam yeye anasema kasajili Yanga tu, hapa kuna mambo mawili tu. Ama Ngasa kasaini timu zote mbili au viongozi wa Simba wamefoji usajili wake ili kumkomoa.

Safari hii hili suala lisimalizwe eti kwa kutumia busara. Kama kasaini mara mbili apate adhabu yake ya kufungiwa, lakini kama watu wamefoji usajili wake waadhibiwe. Tena bahati nzuri sasa kuna kamati ya maadili. Suala liende huko wahusika wafungiwe kujihusisha na mpira.

Lolote katika hayo, kuna kosa la jinai. Ama utapeli kwa upande wa Ngasa au viongozi waliofoji usajili wake. Pamoja na kamati ya maadili kufanya kazi yake, sheria zichukue mkondo wake ili upumabvu huu usirudiwe tena katika soka la Tanzania.
 
Kama katibu wa tff alisema simba waonyeshe mkataba wa ngassa walioupeleka tff (akimaanisha hakuna mkata wa simba na ngassa tff), sasa simba wamepeleka jina la ngassa kama wamemsajili kwa kigezo kipi?
 
Nadhani mikataba ina wakati wake wa kupeleka. Bila shaka hayo yatazingatiwa wakati wakitoa uamuzi. Lakini safari hii wakomeshe uhuni katika soka.
 
Mi nafikiri mambo kama haya ndio yanayokwamisha maendeleo ya soka hapa bongo,sasa imefika wakati serikali kukosha hawa wahuni walio#TFF na kwenye club wanaochezea sheria na ghushi.
 
Kweli kabisa hao wahuni wapo TFF na kwenye club. Hili ni mambo yaliyomshinda Tenga. Itakuwa nin issue kwa Rais wa TFF ajaye
 
mpira wenu wa masodo , mnashindwa hata kuiga taratibu za usajili kutoka nje ya bara la Afrika, Kuiga tu, Je kubuni mnaweza nyie...
 
Mi nafikiri mambo kama haya ndio yanayokwamisha maendeleo ya soka hapa bongo,sasa imefika wakati serikali kukosha hawa wahuni walio#TFF na kwenye club wanaochezea sheria na ghushi.
Tatizo siyo simba, tatizo ni kale kasomali kanakopenda kutembea na bastola..! Simba naichukia ila haka kasomali nakachukia zaidi..!
 
Inaelekea msimu huu kutakuwa na vute nikuvute kuhusu usajili wa mchazaji Mrisho Ngasa.

Maadam yeye anasema kasajili Yanga tu, hapa kuna mambo mawili tu. Ama Ngasa kasaini timu zote mbili au viongozi wa Simba wamefoji usajili wake ili kumkomoa.

Safari hii hili suala lisimalizwe eti kwa kutumia busara. Kama kasaini mara mbili apate adhabu yake ya kufungiwa, lakini kama watu wamefoji usajili wake waadhibiwe. Tena bahati nzuri sasa kuna kamati ya maadili. Suala liende huko wahusika wafungiwe kujihusisha na mpira.

Lolote katika hayo, kuna kosa la jinai. Ama utapeli kwa upande wa Ngasa au viongozi waliofoji usajili wake. Pamoja na kamati ya maadili kufanya kazi yake, sheria zichukue mkondo wake ili upumabvu huu usirudiwe tena katika soka la Tanzania.

well said maana wamezidi hawa kutuharibia ligi yetu..
 
kweli sibonike kumwanya

uichukie Simba ama umchukie Rage hiyo ni kivyako. Ngassa kama kweli amesaini mikataba ya Timu zote mbili afungiwe kucheza soka kwa mwaka siyo kuangalia ni upande upi umekamilisha document kama alivyonukuliwa akisema Katibu wa TFF vivyohivyo kama viongozi wa Simba kama wamefoji signature ya Ngassa nao wafungiwe.
 
ka Ngasaa kamesajili Yanga ilihali kana mkataba Simba
 
Simba wamefoji mkataba lengo wamkomeshe Ngasa maana bado wanampenda
 
Simba walisahiri kwa ujinga kwani wakati Ngasa anatoka Azam kwa mkopo alikuwa amebakuza mwaka mmoja kumaliza mkataba wake,hivyo basi sheria ya usajiri inasema kuwa huwezi kumsajiri mchezaji kutoka timu nyingine akiwa ndani ya mkataba unaozidi miezi 6.Simba hilo hawakulijuwa?
 
Tanzania ni matapeli tu kamchezaji Kakiwa na jina kidogo tu Basi inakuwa vurugu katika swala la usajili mbona huko majuu hakuna huo ujinga na majina makubwa yapo. Hapa ni utapeli. Vilabu utapeli na Tff utapeli na wizara ya michezo utapeli mtupu
 
Kwani mkataba baina ya timu na mchezaji ni siri? Mbona kila Simba inaposaini mkataba na mchezaji huwa ni tukio linalohudhuriwa na wanahabari ambao hawasiti kulifanya tukio hilo kuwa ndio habari kwa wiki kadhaa baadaye? Licha ya hafla ya kupokelewa kwa mkopo, ni lini chombo chochote cha habari kiliripoti Simba kumsainisha Ngassa mkataba? Lini mkataba ulipelekwa TFF? Walichowahi kueleza Simba ni kichekesho kwamba wamenunua haki zote za Azam kwa mchezaji huyo, kwa maana kwamba baada ya kumaliza muda wa mkopo, Ngassa angeendelea na Simba kama ni mchezaji wa Azam. Jamani kuna hakimiliki (copyright arrangement) kwenye mikataba ya wachezaji? Hata kama iko, ina maana mchezaji mwenyewe huwa hahusishwi? Kama ni hivyo, hiyo si biashara ya binaadamu (human trafficking). Ndio Simba inakotaka kuipeleka Tanzania huko? Swala la Yondani halikutosha kuwa funzo? Bila kujali ushabiki wa upande mmojawapo unaohusika, uhalifu wa aina hii unapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.
 
Nakumbuka vizuri ile siku ngassa anatambulishwa simba....kiongozi wa simba aliongelea hili...alisema tumemchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja na tumemwongezea mwaka mmoja mwingine,ngasa hakuwahi kulipinga hili licha ya kusikia...lakini hata mm nilikuwa napata wakati mgumu sana kuelewa pale mechanism gani imetumika mpaka umetokea mkataba wa miaka miwili,nadhani ngassa aliuona huu udhaifu na akautumia....viongozi wa simba timu yangu si watu makini kabisa mwache aende tu jamaa kawazidi akili viongozi
 
ka Ngasaa kamesajili Yanga ilihali kana mkataba Simba

Kalienda Simba kwa mkopo toka Azam, huo mkataba umeisha mwishoni mwa msimu uliopita kakaenda Yanga baada ya mechi ya watani, Simba walikasainisha lini? Huenda walikachomekea huo mkataba bila kenyewe kujua, kisheria huo ni mkataba batili kwa vile kuna hila ndani yake. Tuwaachie TFF waamue.
 
Tanzania ni matapeli tu kamchezaji Kakiwa na jina kidogo tu Basi inakuwa vurugu katika swala la usajili mbona huko majuu hakuna huo ujinga na majina makubwa yapo. Hapa ni utapeli. Vilabu utapeli na Tff utapeli na wizara ya michezo utapeli mtupu

Arsenal v Liverpool (Suarez) na Chelsea v Man United (Rooney); hizi issues unazionaje Mkuu?
 
Nakumbuka vizuri ile siku ngassa anatambulishwa simba....kiongozi wa simba aliongelea hili...alisema tumemchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja na tumemwongezea mwaka mmoja mwingine,ngasa hakuwahi kulipinga hili licha ya kusikia...lakini hata mm nilikuwa napata wakati mgumu sana kuelewa pale mechanism gani imetumika mpaka umetokea mkataba wa miaka miwili,nadhani ngassa aliuona huu udhaifu na akautumia....viongozi wa simba timu yangu si watu makini kabisa mwache aende tu jamaa kawazidi akili viongozi

Hivi mtu akisema leo si Nanenane, kuna haja ya kukanusha? Ngassa hakuwa na haja ya kukanusha kwa sababu hakukuwa na haja ya kukanusha jambo lililo uongo wa dhahiri.Sheria gani ya FIFA, CAF,CECAFA au TFF inayoruhusu kupandishia mkataba wa aina hiyo? Kwanza timu yoyote haipaswi kuongea na mchezaji mwenye mkataba mpaka ibakie miezi sita ya kuumaliza. Simba wamekopeshwa Ngassa kukiwa na zaidi ya mwaka kabla ya (mkataba) kuisha. Watakiukaje sheria kumsaini hivyo? Inaonesha Simba wanakosea tafsiri ya neno 'loan" kwenye mwaswala ya wachezaji. Tafsiri sahihi ya 'loan' si mkopo. Ni kuazimwa. Ndio maana mchezaji wa aina hiyo huwa anaendelea kulipwa na klabu yenye mkataba naye. Labda Rage alidhani wamekopeshwa kama yeye anavyokopa pesa benki, anaweza kuzifanya apendavyo, madhali atazilipa. Kwani Simba ilitakiwa kuilipa Azam baadaye kwa kumchkua Ngassa? Huo ungekuwa ndio mkopo kwa maana ya Kiswahili ya neno hilo. Simba wasijidanganye, wakawadanganya na Watanzania wenye desturi ya kumwamini kila mtu.
 
Back
Top Bottom