Usajili wa Majwega Simba S.C: Wathibitisha Undugu wake na Azam F.C

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Baada ya Figisu Figisu za mda mrefu hatimae jana, yule kiungo machachari kabisa kutoka nchini Uganda, Brian Majwega.. Katua Simba S.C.
Hii haijatokea kama ajali bali ni kutokana na Undugu wa mda mrefu wa hizi timu mbili.
Nawashushia usajili baina ya Azam F.C na Simba S.C ambao japo kulikua na Figisu Figisu nyingi.. Ila Undugu uliopo ulisababisha usajili ukakamilika;

WACHEZAJI WALIOTOKA AZAM NA KUTUA SIMBA
1. MRISHO NGASSA a.k.a Ankoo
Alisajiliwa Azam F.C kutoka Yanga kwa dau kubwa tu, lakini haikuchukua muda akaanza kama kutoaminika anapocheza dhidi ya timu yake ya zamani.
Azam F.C wakaona isiwe tabu.. wakangalia kushoto kulia.. Wakamuona Ndugu yake Simba S.C kuna kitu kinamisi katika katika 1st eleven yake.. Hivyo wakaamua kutupatia Ngasa.

2. RAMADHANI CHOMBO a.k.a Redondo
Huyu alisajiliwa Azam F.C akitokea Simba SC kwa dau kubwa tu mwanzoni mwa msimu wa 2011/12... Baada ya mda mfupi, Redondo alitorokea Msumbiji kabla ya kukwama ITC, na kurejea Azam ambako alicheza hadi mwisho wa msimu.
Katika msimu wa 2012/13.. Redondo alijitoa Azam na kuja kusaini Simba kimya kimya.. Azam ilileta tafrani kidogo, lakini baadaye ikaamua kumalizana na Simba ili Redondo arejee timu yake ya zamani.. Haya yote yalifanikiwa kutokana na Undugu uliopo baina ya hizi timu mbili.

3. JOSEPH OWINO a.k.a Gela
Alisajiliwa Azam akiwa majeruhi toka Simba S.C, ambapo walimgharamia matibabu na wakamvumilia kukaa nje ya Uwanja kwa msimu mzima.
Alipopoma akakuta kuna Defence imara ishajengwa hivyo kupenya ikawa ngumu.. Kipindi hicho Msimbazi kulikua na tatizo la beki wa kati.. Azam wakaona isiwe shida, wakatupatia Gela, ambapo alikuja kuwa nguzo imara sana katika defence line yetu.

WACHEZAJI WALIOTUMIA TIMU NYINGINE KAMA DARAJA
1. DEO MUNISHI a.k.a Dida
Huyu mlinda mlango alitua Azama F.C akitokea Mtibwa Sugar. Ikumbukwe kabla ya kutua kwa Wakata Miwa, Deo alikua akiitumikia Simba SC.

2. SHOMARI KAPOMBE
Daraja lake la kuelekea Azam F.C lilikua ni timu ya Nice toka nchini Ufaransa.. Japo ilikua ngumu sana kwa Kapombe kutua Azam baada ya kutoka nchini Ufaransa.. Ndugu wawili tulikaa tukamalizana, na sasa jamaa anakipiga Azam.

3. SAID MOURAD
Alisajiliwa Azam F.C akitokea Kagera Sugar, baada ya awali kuitumikia Simba SC.. Said alikwenda kua nguzo muhimu sana kwa timu ya Azam F.C.

WACHEZAJI WALIOTOKA SIMBA NA KUTUA AZAM
1. AMRI KIEMBA a.k.a Rasta.
Awali Azam FC ilitaka ipewe kiungo huyo kwa mkopo, lakini Simba ikakataa huku ikatangaza dau la dola 15,000.
Lakini Ndugu wawili wakutanapo hakuna kinachoharibika.. Hatimae mambo yakaenda safi kabisa na Kiemba aksajiliwa kwa mkopo na Azam kwa muda wa miezi sita.

2. RAMADHAN SINGANO a.k.a Messi
Dili la Messi kutua Azam akitokea Simba S.C lilitaka kuvunja Undugu wetu wa Miaka mingi.
Baada ya Azam kuona wanapata hasara kubwa [Na hii ni baada ya mashabiki wa Simba S.C duniani kususia bidhaa zote za Azam, ili kupinga usajili wa Messi ~ just joking].. walitufuata Ndugu zao tukakaa chini tukamalizana.. Na katika moja ya makubaliano yetu ni kutuongezea nguvu katika timu yetu.. Hapo ndipo wakatupatia Joseph Kimwaga aje atutumikie kwa Mkopo.

NOTE: 12/12/2015 Undugu tunauweka kando.. Ndugu zetu Azam F.C mtatusamehe.. Lazima Tushinde.
 
...hivi ukisema undugu huoni kama unaweza kutafsiriwa tofauti?! mimi nakushangaa sana, kule juu umeandika undugu nikadhani umeishia hapo, kumbe tena unakuja kuanzisha uzi kuzungumzia 'undugu'?!
Sidhani kama kweli wewe ni msemaji 'official' wa simba kwenye mitandao.
 
Sasa hivi klabu ya simba ni kama timu ya mchangani.....hata usajili ni wa kuokoteza......viongozi wanachopigania ni timu kubaki ligi kuu.....lakini si kuirudisha heshima ya klabu.........
kitu pekee tunachojivunia SIMBA ni kuifunga YANGA tu.......
 
Mimi si msemaji wa Simba S.C.. Ni mwanachama pia mshabiki wa Mnyama.
Na kuhusu Undugu baina ya timu 2 ni jambo la kawaida duniani..
Mfano..
1. Anderlecht na Arsenal
2. Man United na Club Guadarajala ya Mexico
Hivyo mtu anaposhangaa undugu wa Simba na Azam, lazima nimshangae.
 
ok; kama unalinganisha ulaya na bongo halafu unajiona uko sawa!!
 
Sasa hivi klabu ya simba ni kama timu ya mchangani.....hata usajili ni wa kuokoteza......viongozi wanachopigania ni timu kubaki ligi kuu.....lakini si kuirudisha heshima ya klabu.........
kitu pekee tunachojivunia SIMBA ni kuifunga YANGA tu.......

...hii ya kumfunga Yanga nayo inaanza kuondoka taratibu, tutabaki tunajivunia rangi nyekundu na nyeupe!
 
Mimi si msemaji wa Simba S.C.. Ni mwanachama pia mshabiki wa Mnyama.
Na kuhusu Undugu baina ya timu 2 ni jambo la kawaida duniani..
Mfano..
1. Anderlecht na Arsenal
2. Man United na Club Guadarajala ya Mexico
Hivyo mtu anaposhangaa undugu wa Simba na Azam, lazima nimshangae.

Mifano uliotoa ni ya timu 2 za nchi 2 tofauti, lakini simba na azam zote za bongo.
 
Mifano uliotoa ni ya timu 2 za nchi 2 tofauti, lakini simba na azam zote za bongo.

sasa kwa kuwa ni nchi moja si ndiyo inadhihirisha one faza one maza? ole wemu mniite mafuru kisa nimechanganya language..
 
Back
Top Bottom