Usajili wa CHADEMA online umeanza rasmi

lutayega

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
1,288
552
Kuwa MwanaCHADEMA Leo!
CHADEMA ndicho chama pekee kikubwa cha upinzani ambacho kimekua na kinaendelea kukua kisiasa. Aidha CHADEMA ndicho chama cha upinzani chenye nguvu kuliko vyote Tanzania bara. Ingawa CHADEMA ni chama cha upinzani lakini pia ni chama tawala wilaya za Karatu na Kigoma Ujiji. Wengi wanaamini CHADEMA ndicho chama mbadala kinachotegemewa kukiondoa CCM madarakani. Hivyo basi uamuzi wako wa kujiunga na chama ni uamuzi wa kina, sahihi na wenye busara.
Kama wewe ni Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, mwenye akili timamu na uliyesoma na kukubaliana na Sera, Falsafa, Itikadi na Katiba yetu basi unazo sifa zote za kuwa mwanaCHADEMA. Aidha hutatakiwa kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa unapojiunga nasi.
Ada ya kujiunga na chama ni shilingi mia tano na ya Uanachama kwa mwaka ni shilingi elfu moja. Hata hivyo mnakaribishwa na mnahimizwa kuchangia zaidi ya hicho kiwango kama uwezo unao. Tutawasiliana nawe kwa barua-pepe kukueleza utaratibu wa kulipia ada.
Fuata maelekezo yafuatayo hapo chini ili nawe uweze kujivunia kuwa mwanaCHADEMA leo!
kwa maelekezo na fom ya uanachama Bonyezi hapa kujisajiri.

 
Kwa wale ambao walikuwa wamejiandikisha kwaajili ya usajili kipindi kile mnaombwa kujaza fom hiyo ili kukamilisha usajili
 
MKUU MBONA HIYO LINK YA USAJILI INATOA HII MSG:-

Reported Attack Page!







This web page at USAILI WA UANACHAMA WA TAWI LA CHADEMA ONLINE has been reported as an attack page and has been blocked based on your security preferences.





Attack pages try to install programs that steal private information, use your computer to attack others, or damage your system.Some attack pages intentionally distribute harmful software, but many are compromised without the knowledge or permission of their owners.
 
My PC inaniambia hiyo link ina virus!!!! Kwa nini unataka kuitumia CHADEMA kutuletea virus kwenye computer zetu wewe jamaa Ltayega?

Tiba
 
inafunguka safi tu kwa sasa, japokuwa kuna mtu aliitolea report kama hiyo ni attack site ndio maana mkawa mnakutana na message hiyo. chademaonline.gif
 
PC yangu inanambia hivyo hivyo pia, naomba mjipange then ndo mje hapa mkiwa kamili
 
Mkuu hiyo link unayoweka hapo haya ndiyo majibu yanayotoka Reported Attack Page!
 
Anayetaka taarifa zake za kwenye computer yake, taarifa binafsi, taarifa za kwenye harddisk yake, password na documents tuzimwage LIVE kwenye mitandao na AJISAJILI.
 
1. Waambieni watu wenu wa TEKNOHAMA warekebishe usalama wa link yenu ili wanaotaka kujisajili wasie na hofu ya usalama wa PC na data zao.
2. Ondoeni suala la "kuwa na akili timamu" au wekeni kithibitisho cha kuwa mtu na akili timamu.
 
Hiyo link ya chadema ni infected! Kompyuta yangu imekataa kuifungua na antivirus yangu (avast) imeniambia kwamba kuna virus kwenye link. Link ya chademaonline.org imeshambuliwa na trojan aitwaye vbsAgent -Kztrojan. Safisheni hii link na kuwazuia hao cyber hackers kutekeleza uinga wao! controler
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom