Usaili Umoja wa Ulaya!!

Usaili Umoja wa Ulaya!!

Mangungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
2,405
Reaction score
3,061
Wadau naomba msaada tutani,niliomba nafasi ya Mhasibu Msaidizi,Umoja wa Ulaya!!!!

Leo wameniita kwenye usaili ijumaa saa 4:30, makao makuu ya umoja wao dsm mtaa wa mirambo!!

Wameniambia niende na kikokotozi (calcurator)

Naombeni msaada wenu kama ulishawahi piga nao usaili wa kazi yoyote!!

Asanteni sana.
 
Jenga confidence kwanza. Kama umeambiwa uende na kikokotozi, basi jiandae kukokotoa na usisahau kujiandaa na maswali mengine ya Jumuia na Kazi yenyewe Kwa ujumla. Kila la kheri.
 
Jenga confidence kwanza. Kama umeambiwa uende na kikokotozi, basi jiandae kukokotoa na usisahau kujiandaa na maswali mengine ya Jumuia na Kazi yenyewe Kwa ujumla. Kila la kheri.

Asante sana mkuu wangu!!!
 
Asante sana mkuu wangu!!!

Niliwahi kufanya interview ya project officer hapo, mara nyingi mnaanza written interview ya masaa ma2, wanaofanya vizuri wanaitwa kwajili ya oral ya saa1, mara nyingi maswali yao yanajengwa na misingi ya scenarios, na sio direct questions, kwahiyo, wanaandaaga maswali yenye changamoto katika scenarios fulan. All the best.
 
Thankx mkuu wangu... ngoja nikapigane!!
Yanakua maswali kama mangapi hv??
Maana hadi kubeba calculator hapo ni mtindo wa kushusha Cash flow Kama sio income statement
 
Wameniambia niende na kikokotozi (calcurator)

Duh!!! hadi kwenye umombo bado tu mnachanganya matumizi ya 'r' na 'l'...hatari sana!!!

Naombeni msaada wenu kama ulishawahi piga nao usaili wa kazi yoyote!!
Hata hivyo soma vizuri job description itakupa mwangaza wa namna ya mtu atafutwaye kwa nafasi hiyo...

Uzuri wa ofisi kama hizo huwa hazina watu wengi wanaoitwa kufanyiwa interview, hili husaidia kuondoa mchecheto kwa wasaka kazi...

Mambo mengine ya kuzingatia ni kuwa nadhifu, kama ni oral interview basi jitahidi ujibu kwa kifupi lakini kwa kueleweka...

Kama umeulizwa swali na hujalielewa una haki ya kuomba ufafanuzi zaidi...

Kila la kheri!!!
 
usisahau kuomba inasaidia na uwe couragious jiamini bu t usi over jiamini Mungu akutangulie mkuu
 
Duh!!! hadi kwenye umombo bado mnatumia tu mnachanganya matumizi ya 'r' na 'l'...hatari sana!!!

Hata hivyo soma vizuri job description itakupa mwangaza wa namna ya mtu atafutwaye kwa nafasi hiyo...

Uzuri wa ofisi kama hizo huwa hazina watu wengi wanaoitwa kufanyiwa interview, hili huondoa mchecheto kwa waska kazi...

Mambo mengine ya kuzingatia ni kuwa nadhifu, kama ni oral interview basi jitahidi ujibu kwa kifupi lakini kwa kueleweka...

Kama umeulizwa swali na hujalielewa una haki ya kuomba ufafanuzi zaidi...

Kila la kheri!!!

Watu 8 asante sana kamanda wangu....

Kuchanganya "r" na "l" inategemea na kabila wahaya hawana "ng" wana "ngi" kwenye r and l ni ugonjwa wa taifa!!

Nashukuru tena kwa ufafanuzi wako!!
 
all the best,,ila usisahau kupitia inflation rates,bids and ask,,
 
Back
Top Bottom