SI KWELI USAID wanagawa pesa

SI KWELI USAID wanagawa pesa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
USAID Funds July 10, 25.jpg

USAID Mpesa Text.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwa na ujumbe unaosambazwa katika makundi sogozi ya WhatsApp ikiwaeleza watu kuwa kuna mfuko ujulikanao kama USAID FUNDS FOUNDATION PROGRAM ambao unatoa fedha kwa watu. Ujumbe huo unawataka watu watume pesa kupitia namba iliyotajwa na ili waweze kupata.

Uhalisia wa jambo hilo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo ina lengo la kulaghai na kufanya utapeli.

Aidha kundi la WhatsApp hilo lijulikanalo kama USAID FUNDS FOUNDATION PROGRAM limeanzishwa kwa namba binafsi yenye usajili wa Tanzania (+255) ikiwa ni namba ya mtu binafsi na si ya taasisi.

Ufuatiliaji pia umebaini mfuko huo unaoitwa USAID FUNDS haipo katika mitandao ya kijamii na iliyopo kwa upande wa Instagram ina jina ina maudhui tofauti.

Hata hivyo shirika la misaada kutoka kwa watu wa Marekani limefutwa rasmi Julai 1, 2025 na baadhi ya shughuli zilizobaki zimehamishiwa kwenye wizara ya mambo ya nje.

Ujumbe unaoonekana kuwa ni wa mtu aliyepata fedha kutoka kwenye mfuko huo ni za kughushi kwani zina makosa kadhaa mathalani kiwango cha fedha cha makato kwa muamala.

Ujumbe huo umeonesha kuwa kiwango cha fedha kilichotumwa ni Tsh. 10,000 lakini makato ni Tsh. 1,000. Kwa mujibu wa viwango vya gharama za kutuma pesa kutoka M-pesa kwenda M-pesa ya mwaka 2023 kuanzia Tsh. 10,000 hadi 14, 999 ni Tsh. 350.

Similar Discussions

Back
Top Bottom