Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
.
USAHIHI WA RAIS MAGUFULI UPO WAPI?
Nimeshindwa kueleweka, lakini nitaeleweka tu..!
Rais Magufuli kitendo cha kumuachia huru Mwana Hiphop Ney wa Mitego, kinaweza kusesabiwa kuwa ni kitendo cha uungwana miongoni mwa wengi, na kikafurahiwa, lakini haimaanishi kwamba wote tutaamini hivyo na kupongeza, kwani kama maamuzi yanaweza kufanywa bila utaratibu Kwa kusudio jema na tukaona ni sawa kwasababu tu imekuwa Neema kwetu, basi tuwe radhi kushuhudia maamuzi ya kifanywa bila kufuata utaratibu hata Kwa Yale yanayotuumiza pia, kinyume na hapo tuzibadili sheria zetu, kanuni na taratibu mbalimbali tulizojiwekea wenyewe.
Msimamo wangu ni kwamba sheria zifuatwe, ifahamike kwamba tuna sheria mbovu na kandamizi au tuna sheria nzuri isipokuwa utekelezaji wa sheria na uwajibikaji ndiyo unaokosekana.
Jeshi la polisi pamoja na kuwa limekuwa likilalamikiwa kuwaonea wananchi, kuwabambikia kesi na kuwachelewesha mahabusu kwenda mahakamani Kwa kisingizio cha upelelezi haujakamilika, lakini jeshi la polisi bado huona zipo sababu za msingi za kumkamata mtuhumiwa aidha Kwa makosa ya madai, au makosa ya jinai. Na hata lilipomkamata mwana hip hop Ney wa Mitego, jeshi la Polisi lilikuwa na sababu aidha Kwa taaluma na uzoefu wao, utashi wao, sheria za nchi, au taratibu na tamaduni za watanzania ambazo ziliwapelekea kumkamata Ney wa Mitego. Na kilichokuwa kinafuata ni utaratibu wa kimahakama, kumfikisha msanii huyo mahakamani ndani ya SAA 24, kusomewa mashitaka, naye kujibu na kutetewa na mawakili wake, ambao tayari walikwisha kujitokeza kumtetea akiwepo wakili msomi Peter Kibatala.
Alichokifanya Rais Magufuli ni kuingilia kati wakati ambao msanii Ney wa Mitego alikuwa anaelekea mahakamani. Na wananchi wengi tulikuwa tayari kufahamu ukweli wa makosa ya msanii Ney wa Mitego wakati kesi yake ikiendeshwa. Nina hakika Polisi wetu waliudhika labda kuona mtu Fulani akidhalilishwa Kwa kuitwa BASHITE ambapo wao wanamfahamu Bashite kama kiongozi wa serikali, au yawezekana Polisi walifahamu kwamba kweli kuna Kichaa kapewa Rungu, hivyo kumuimba hadharani ni makosa, haya na mengine mengi tungeyafahamu huko mahakamani.
Lakini Rais Magufuli kitendo cha kuingilia kati Kwa kigezo cha kufurahishwa na wimbo huo na kwamba msanii Huyo aachiwe huru na aendelee kuimba nyimbo kama hizo, ni mwendelezo wa kumkumbatia Mkuu wa mkoa wa DSM ambaye amekuwa akitajwa na wananchi wengi kuwa ndiye BASHITE, hivyo pamoja na yote yaliyokuwa yamejiri Siku chache zilizotangulia, ni wazi pale mahakamani huenda majina halisi ya mkuu Huyo wa mkoa wa DSM yangefahamika, na hoja ya kufoji vyeti ingefunguka, na mkuu Huyo wa mkoa wa DSM angejikuta matatani, kwahiyo alichokifanya Rais Magufuli ni kitendo kinaitwa 'Diversion' kukwepesha mjadala na kumuokoa BASHITE, pamoja na kumficha Yule anayesemekana hataki kupokea ushauri wala kukosolewa.
Leo msanii Ney wa Mitego yupo huru, Je: polisi walifanya makosa kumkamata? Kama walifanya makosa, kwanini hawajaambiwa hadharani kwamba hilo sio kosa na msirudie tena kuwakamata wasanii wanaoikosoa serikali? Faida ya mahakama ni kwamba, kama msanii Ney wa Mitego angeshinda kesi, maamuzi ya Jaji yangewalinda wasanii wengine ambao Siku zausoni wataimba kama alivyoimba Ney wa Mitego, Je, maamuzi haya aliyoyafanya Rais Magufuli yatawalinda wasanii wengine watakaoimba namna hiyo??
Kulinda Uhuru wa taasisi simamizi nchini, likiwepo jeshi la polisi, IGP alipaswa kwenda mahakamani kuipinga kauli ya Waziri/Rais ambayo imeingilia utekelezaji wa majukumu yake, pamoja na kwamba Rais ndiye amiri jeshi mkuu, lakini Kwa ushahidi wa makosa aliyokuwa amekosea mtuhumiwa, ilipaswa jeshi la polisi kumfikisha mahakamani, kinyume na hapo, IGP angejiuzulu, maana amedhihirisha uongozi wake kwenye jeshi la polisi sio wa haki na hauzingatii sheria.