Bila kutliza akili yako, na kwa jinsi mjadala unavyokanganya lazima utakuja na haya. Mimi nilivyomuelewa Lusinde na mimi mwenyewe ninavyoamini, fedha za escro zote si za itpl bali ndani ya fedha za escro kunaq sehemu ya fedha za umma, upo hapo sangarar????????????????usipotoshe watu
Ukinionyesha upotoshaji wa maelezo yangu, nitaulekebisha.
Upotoshaji wako uko hapa: Muuzaji ndiye anayelipa vat pale tra na wala sio mmununzi
CAG mwenyewe hana uhakika kama kuna pesa za umma humo.Bila kutliza akili yako, na kwa jinsi mjadala unavyokanganya lazima utakuja na haya. Mimi nilivyomuelewa Lusinde na mimi mwenyewe ninavyoamini, fedha za escro zote si za itpl bali ndani ya fedha za escro kunaq sehemu ya fedha za umma, upo hapo sangarar????????????????usipotoshe watu
It seems you have a point. Conclusion yako imechanganya mambo, umesema fedha za escro si za umma na kwamba kamati ya zitto imepotosha wakati huohuo unasema tena umeeleweka vizuri kwamba anayestahili kulipa vat tra ni muuzaji na umesema iptl alikuwa anamuuzia tanesco umeme na tanesco anamlipa iptl sasa iweje fedha za escro zisiitwe ndani yake kuna fedha za umma????? fafanua kidogo, maana tunapokea maswali mengi kutoka vijijini tunakozaliwa ilituwape maelezo yanayojitoshereza
SAGHANKA... HEBU TUAMBIE Tanesco ni kampuni inayomilikiwa na akina nani kama sio shirika la umma? Na hela inayopatikana kutoka na biashara inayofanywa na kampuni ya umma (Mfano Bandari, TTCL, POSTA etc) hizo hela ni za uma au la... hizo kampuni ikiwemo Tanesco inapofanya malipo ya aina yeyote kwa wateja wake akiwemo IPTL inafanya malipo hayo kwa niaba ya nani kama sio Umma? Baada ya hapo kumbuka kwamba hata Lusinde naye alishangaa hivi ni nani aliyempa AG uwezo wa kusamehe kodi... Jambo la tatu ni kwamba tunachopigania humu ni uadilifu wa wale tuliowachagua kutuongoza.. sasa unapoambia Muhongo aliomba Rusha kwa kiambatanish cha barua ya singasinga kwa PAC , sijui wewe unalizungumziaje hilo.... muomba, mtoaji na mpokeaji wa rushwa wote huwa ni wahujumu uchumi na huwa wanaadhibiwa.. sasa ni kwa nini wao akina muhingo wanaona vigumu kuachia ngazi kwa hilo tu la kuomba rushwa ili wawe madarali ? kitu kingine I kwamba ndani ya miaka 9 tu, serikali imeteteleka kwa mambo haya haya ya ufisadi .. sasa mtu wa kujipima sio Pinda, Lowasa wala muhongo, ni yeye mwenyewe kikwete ajondoe na arudishe madaraka kwa wananchi wawake viongozi wengine.. hata yeye mweyenye alisema anataka kuchunga Ngombe na sijui ni nani aliyemwambia kuchunga ngombe ni kazi rahisi.. najua unakumbuka pale Kenyamonta jinsi hiyo kazi ya kuchunga ngombe ilivyokuwa ngumu halafu leo hii anasema amechoka anataka kuchunga ngombe , ni kudhalau kazi za watu.. kama amechoka inabidi astaafu hata kwa manufaa ya umma kuliko kila siku kututeulia watu wanaotuletea ufisadi kila kona...na hili la IPTL ameliteta yeye, kwa nini asiwajibike tangu akiwa waziri wa nishani.. ni msanii tupu... ameweka history kwamba amepinduliwa na wabunge kuliko Rais yeyote Tanzania na sasa aondoke tu kuliko kuwalazimisha wenzake wastaafu au kujiudhuru...Ndugu watanzania wote (in the voice of profesa Muhongo)
Tuache Jaziba, tuache kulazimisha mapenzi yetu kutimia,tuwe na subra, tujipe nafasi ya kutafakari na kupima mambo haya, tujiweke katika nafasi ya kuwatendea maadui zetu vile ambavyo sisi tungependa kutendewa.
Na zaidi, tufuate ushauri alioutoa Mheshimwa Lusinde jana jioni bungeni, kwamba, "TUSEME KWELI ILI TUFANYE MAAMUZI YA HAKI"
KUHUSU PESA ZA ESCROW KUWA NI ZA UMA ETI KWA SABABU KULIKUWA NA KODI YA VAT NDANI YAKE
Ndugu watanzania wote.
Huu ni upotoshaji, ni uongo na uzushi ambao tunapaswa kuukataa, jambo lolote linalofanywa kwa uovu mwisho wake huwa sio mwema.
Report iliyowasilishwa na PAC katika bunge letu, japo ilitegemewa kuwa msingi wa kulipatia haki Taifa letu, imekuwa ni chanzo cha aibu kwa Taifa zima, hutuwezi kupigania maslahi ya Taifa letu kwa kusema uongo, kuficha ukweli kwa wingi wa meneno yaliyopindishwa pindishwa na kupambwa kwa lugha za ghirba.
UKWELI NI HUU
Kama ambavyo mahusiano ya IPTL na TANESCO yanajurikana, hawa walikuwa na bado wanaendelea kufanya biashara pamoja, IPTL akiwa muuzaji na TANESCO Mnunuzi.
Bila kuzingatia namna wanavyofikia bei ya bidhaa husika, ni wazi IPTL imekuwa ikiipatia INVOICES Tanesco, Ili Tanesco Iilipe IPTL.
Sheria yetu ya kodi ya VAT ya mwaka 1997, imetoa maelekezo yanayowapa wafanyabishara FURSA ya kukusanya kodi ya VAT kutoka kwa wanunuzi wa bidhaa zao, kwa niaba ya TRA.
Kutokana na vigezo vilivyowekwa katika sheria husika, IPTL nao ni wakara wa TRA katika kukusanya kodi ya VAT kutoka Tanesco.
Kutokana na mahusiano ya kibishara kati ya TANESCO NA IPTL, TANESCO Haina mamlaka mpaka leo ya kuchukua maamuzi ya kutoilipa IPTL VAT eti ipeleke VAT hiyo TRA yenyewe.
Hivyo basi, hata katika PESA zilizokuwa kwenye ACCOUNT YA ESCROW, TANESCO walitekeleza wajibu wao wa kisheria na kibiasha kuziweka hela hizo kwenye account hiyo zote za IPTL pamoja na VAT (Ambazo kimsingi zote ni za IPTL), Na wakati malipo yanafanyika kutoka account hiyo, YALIFANYIKA KWA USAHIHI KABISA Kwa PESA zote KULIPWA kwa IPTL. Kwa sababu ni wajibu wa IPTL kukusanya VAT kutoka Tanesco.
TRA walipaswa kuidai IPTL pesa hiyo ndani ya mwezi mmoja baada ya IPTL kuipatia INVOICES Tanesco, bila kujali kama IPTL wanaubishani na Tanesco juu ya usahihi wa INVOICE AMOUNTS au la?.
Huu ndio utaratibu, sio mpya, na wote tunaufahamu, jana nimetoa mfano ambao haukueleweka, ukienda dukani kununua bidhaa, unaambiwa bei ya bidhaa ambayo ndani yake kuna VAT, ukifanya maamuzi ya kununua unamlipa muuzaji pesa zote, NA KUANZIA HAPO ZINAKUWA ZAKE na wewe bidhaa inakuwa yako rasmi.
Swala la wafanyabishara kutopeleka makusanyo ya VAT TRA ni tatizo lingine.
HIVYO BASI
Kama sababu ya msingi ya kudai kwamba zile pesa ni za UMA ni sababu ya VAT COMPONENT KWA ZILE HELA, HUO NI UONGO NI UPOTOSHAJI.
Nawasilisha.
Ukinionyesha upotoshaji wa maelezo yangu, nitaulekebisha.
Juzi nilienda kununua mifuko ya cement. Kwenye stakabadhi ya malipo niliyopewa, kuna item ya VAT. Muuzaji wa cement hakunitaka niende kulipa hiyo VAT TRA bali yeye kama muuzaji ndiye aliyekuwa na dhamana ya kukusanya VAT kutoka kwangu na kuiwasilisha TRA