Usahihi: VAT kwenye escrow

Usahihi: VAT kwenye escrow

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Ndugu watanzania wote (in the voice of profesa Muhongo)

Tuache Jaziba, tuache kulazimisha mapenzi yetu kutimia,tuwe na subra, tujipe nafasi ya kutafakari na kupima mambo haya, tujiweke katika nafasi ya kuwatendea maadui zetu vile ambavyo sisi tungependa kutendewa.

Na zaidi, tufuate ushauri alioutoa Mheshimwa Lusinde jana jioni bungeni, kwamba, "TUSEME KWELI ILI TUFANYE MAAMUZI YA HAKI"

KUHUSU PESA ZA ESCROW KUWA NI ZA UMA ETI KWA SABABU KULIKUWA NA KODI YA VAT NDANI YAKE
Ndugu watanzania wote.

Huu ni upotoshaji, ni uongo na uzushi ambao tunapaswa kuukataa, jambo lolote linalofanywa kwa uovu mwisho wake huwa sio mwema.

Report iliyowasilishwa na PAC katika bunge letu, japo ilitegemewa kuwa msingi wa kulipatia haki Taifa letu, imekuwa ni chanzo cha aibu kwa Taifa zima, hutuwezi kupigania maslahi ya Taifa letu kwa kusema uongo, kuficha ukweli kwa wingi wa meneno yaliyopindishwa pindishwa na kupambwa kwa lugha za ghirba.

UKWELI NI HUU
Kama ambavyo mahusiano ya IPTL na TANESCO yanajurikana, hawa walikuwa na bado wanaendelea kufanya biashara pamoja, IPTL akiwa muuzaji na TANESCO Mnunuzi.

Bila kuzingatia namna wanavyofikia bei ya bidhaa husika, ni wazi IPTL imekuwa ikiipatia INVOICES Tanesco, Ili Tanesco Iilipe IPTL.

Sheria yetu ya kodi ya VAT ya mwaka 1997, imetoa maelekezo yanayowapa wafanyabishara FURSA ya kukusanya kodi ya VAT kutoka kwa wanunuzi wa bidhaa zao, kwa niaba ya TRA.

Kutokana na vigezo vilivyowekwa katika sheria husika, IPTL nao ni wakara wa TRA katika kukusanya kodi ya VAT kutoka Tanesco.

Kutokana na mahusiano ya kibishara kati ya TANESCO NA IPTL, TANESCO Haina mamlaka mpaka leo ya kuchukua maamuzi ya kutoilipa IPTL VAT eti ipeleke VAT hiyo TRA yenyewe.

Hivyo basi, hata katika PESA zilizokuwa kwenye ACCOUNT YA ESCROW, TANESCO walitekeleza wajibu wao wa kisheria na kibiasha kuziweka hela hizo kwenye account hiyo zote za IPTL pamoja na VAT (Ambazo kimsingi zote ni za IPTL), Na wakati malipo yanafanyika kutoka account hiyo, YALIFANYIKA KWA USAHIHI KABISA Kwa PESA zote KULIPWA kwa IPTL. Kwa sababu ni wajibu wa IPTL kukusanya VAT kutoka Tanesco.

TRA walipaswa kuidai IPTL pesa hiyo ndani ya mwezi mmoja baada ya IPTL kuipatia INVOICES Tanesco, bila kujali kama IPTL wanaubishani na Tanesco juu ya usahihi wa INVOICE AMOUNTS au la?.

Huu ndio utaratibu, sio mpya, na wote tunaufahamu, jana nimetoa mfano ambao haukueleweka, ukienda dukani kununua bidhaa, unaambiwa bei ya bidhaa ambayo ndani yake kuna VAT, ukifanya maamuzi ya kununua unamlipa muuzaji pesa zote, NA KUANZIA HAPO ZINAKUWA ZAKE na wewe bidhaa inakuwa yako rasmi.
Swala la wafanyabishara kutopeleka makusanyo ya VAT TRA ni tatizo lingine.

HIVYO BASI
Kama sababu ya msingi ya kudai kwamba zile pesa ni za UMA ni sababu ya VAT COMPONENT KWA ZILE HELA, HUO NI UONGO NI UPOTOSHAJI.

Nawasilisha.
 
Bila kutliza akili yako, na kwa jinsi mjadala unavyokanganya lazima utakuja na haya. Mimi nilivyomuelewa Lusinde na mimi mwenyewe ninavyoamini, fedha za escro zote si za itpl bali ndani ya fedha za escro kunaq sehemu ya fedha za umma, upo hapo sangarar????????????????usipotoshe watu
 
Na mibunge mingi ilivyo mipuuzi itakubaliana na upuuzi huo
 
Bila kutliza akili yako, na kwa jinsi mjadala unavyokanganya lazima utakuja na haya. Mimi nilivyomuelewa Lusinde na mimi mwenyewe ninavyoamini, fedha za escro zote si za itpl bali ndani ya fedha za escro kunaq sehemu ya fedha za umma, upo hapo sangarar????????????????usipotoshe watu

Ukinionyesha upotoshaji wa maelezo yangu, nitaulekebisha.
 
Naomba watanzania tusiwe na jazba.

Tanesco ni mfanyabiashara kama wengine tu

Tanesco ni wafanyabiashara ya kutuuzia umeme. Katika kuuza huo umeme wameweka VAT, ambayo wao wanawajibu wa moja kwa moja kuipeleka TRA. Kama Tanesco hawakupeleka VAT, TRA waibane Tanesco sio IPTL

Ili Tanesco wafanye hiyo biashara ya kutuuzia umeme, lazima wagharamie gharama za uzalishaji ikiwemo kuilipa IPTL (achilia mbali mkinzano wa viwango, ambalo hili ni u-pumbavu wa Tanesco).

Kama ilivyo kwa mlaji yeyote, yeye hulipa gharama ya bidhaa na VAT. Suala la muuzaji kuipeleka hiyo VAT TRA ni la huyo muuzaji sio mnunuzi. IPTL ni muuzaji na Tanesco ni mnunuzi. Hivyo wajibu wa kulipa VAT ya capacity charge TRA ni wa IPTL sio Tanesco.

ESCROW ACCOUNT
Kutokana na mzozo wa rates za capacity charge, ilifunguliwa ili kuhifadhi fedha kwa muda hadi hapo watakapo ridhiana kama Tanesco haibiwi, IPTL wachukue pesa zao, na kama wanaibiwa, basi kiasi walichoibiwa wakipunguze kutoka kwenye hii account na kinachobaki IPTL walipwe.

Suala la kulipa VAT kwa pesa hii lilikuwa na linabaki kuwa la IPTL. Nashangaa kwa nini TRA wameshindwa kuitekeleza sheria ya VAT. Naamini Tanesco walikuwa wanatenga hii pesa baada ya kupokea Tax invoices toka IPTL. IPTL kwa kutoa tax invoice, walitakiwa kulipa VAT (baada ya kujaza VAT return) bila kujali kama wamelipwa na Tanesco au la. Hapa TRA wanatakiwa wajibu, sio kukurupuka na kusema ndani ya fedha za Escrow kuna kodi ya serikali NO.

Kama IPTL hawakulipa VAT hadi leo, TRA wanatakiwa kuwajibika.

KULIPWA PESA HIZO IPTL
Kama Tanesco (mdaiwa wa capacity charge) aliridhika kuwa hakuibiwa ????? basi hakuna tatizo lolote kulipa IPTL pesa yote bila kupunguza kodi yeyote, laba ka TRA waliiagiza Tanesco kuwa wakara wa kuikusanyia kodi zote za IPTL, vinginevyo hakuna kosa.

UTARATIBU WA KUTOA PESA
Kila mkataba una utaratibu wake. Naamini hata wakati wa kufungua hii account, kulikuwa na utaratibu wa namna ya kuja kuifunga. Uangaliwe huo kama ulifuatwa au la. Kama haukufuatwa watu wawajibike kwa hilo na hapa wa kuwajibika ni GAVANA WA BENKI KUU.

MIGAWO
Pamoja na maelezo mazuri mengi ya kujitetea namna pesa ilivokuwa inatoka, hapa kuna tatizo kubwa. Sioni shida mtu kuamua kugawa pesa yake kwa anayemtaka, ila katika hili kuna shida, figure zinarandana???????

1. Inaonesha kuwa muda wa kuamua kulipa IPTL au kurudisha fedha Tanesco ulikuwa bado (na hili ndilo halisia), ila wajanja walitumia mwanya huu kujinufaisha au

2. Mtoaji alikuwa anatakatisha pesa chafu aliyonayo, sio ya IPTL tu bali ni Zaidi hizi. Money Laundering au

3. Wapokeaji ndio vinara wa kusuka mipango ya uchotaji huu, na inaonyesha wako wengi Zaidi ya walitajwa

CAPITAL GAINS

Hili sio suala la pesa hii, TRA, IPTL na wote kwenye mnyororo wa kubadilisha hati fungani (shares) wamechemka na wawajibike.

USHAURI

Tusipoteze uelekeo kwa kung'ang'ania kuwa ni za serikali au la.

a) Tujikite kuhoji , je kutoka kwake kulikuwa sahihi kwa maana ya wakati, maana bado kesi ya capacity haijaisha hivyo haikuwa sahihi kutoa hizo pesa, maana iliwekwa BOT kusubiri suluhu.

b) Gavana wa BOT ajibu kama terms of reference za kufungua hii account na namna zilivyotoka ni sahihi? Vinginevyo awajibike na waliomtuma au kumshinikiza

c) Mwanasheria Mkuu, alikuwa sahihi kusema pesa hii haina kodi ya serikali, lakini, kabla ya kutoa hayo maagizo, akiwa mtetezi wa haki za serikali, alitakiwa kujua je VAT ya hiyo fedha, IPTL walilipa kwa wakati TRA? Kama walilipa, ruksa kutoa (kama muda ulikuwa sahihi) kama walikuwa hawajalipa, hakuatakiwa kuruhusu kutoka wakati akijua fika kuwa IPTL iko ICU. Awajibike kwa kutokuwa makini

d) TRA: TRA wanakimbizana na vidagaa Kariakoo, wanaacha kukusanya mabilioni ya VAT (kama IPTL hawakulipa kila mwezi walipotoa invoice za kuidai Tanesco) toka IPTL. Watendaji (Kamishna wakuu na makamishan wa VAT) waliokuwepo toka Escrow account inafunguliwa hadi leo wajibu na kuchukuliwa hatua

e) Kamati ya Zitto, inatakiwa itende haki sio kutumia jazba na chuki binafsi. Wasituaminishe uongo, hasa kusema kulikuwa na pesa za serikali. Wao wangesema, kwa kuwa Tanesco ni shirika la umma, kama wakishinda kesi, itakuwa kazi sana kupata pesa yao toka IPTL. Waache haya maneno ya "inaweza kuwemo……….."

Nawasilisha
 
It seems you have a point. Conclusion yako imechanganya mambo, umesema fedha za escro si za umma na kwamba kamati ya zitto imepotosha wakati huohuo unasema tena umeeleweka vizuri kwamba anayestahili kulipa vat tra ni muuzaji na umesema iptl alikuwa anamuuzia tanesco umeme na tanesco anamlipa iptl sasa iweje fedha za escro zisiitwe ndani yake kuna fedha za umma????? fafanua kidogo, maana tunapokea maswali mengi kutoka vijijini tunakozaliwa ilituwape maelezo yanayojitoshereza
 
Ukinionyesha upotoshaji wa maelezo yangu, nitaulekebisha.

Upotoshaji wako uko hapa: Muuzaji ndiye anayelipa vat pale tra na wala sio mmununzi. iptl ni wauzaji wa umeme kwa tanesco,na tanesco ni mununuzi tu. Sasa kama vat haikulipwa kwani fedha za vat ni za nani??? ninachofahamu fedha za escro sio zote za umma bali kuna sehemu ya fedha za umma ndani ya fedha za escro, sagarara na wewe nipe zako
 
CAG anachunguza pesa zisizo za Serikali?
 
Upotoshaji wako uko hapa: Muuzaji ndiye anayelipa vat pale tra na wala sio mmununzi

TANESCO kama shirika la UMMA ilitakiwa wakati wanalipa IPTL ilibidi wa WITHOLD TAX husika na kuipeleka TRA.
Hawakutakiwa walipe kiwango chote IPTL kikiwa na VAT.
 
Bila kutliza akili yako, na kwa jinsi mjadala unavyokanganya lazima utakuja na haya. Mimi nilivyomuelewa Lusinde na mimi mwenyewe ninavyoamini, fedha za escro zote si za itpl bali ndani ya fedha za escro kunaq sehemu ya fedha za umma, upo hapo sangarar????????????????usipotoshe watu
CAG mwenyewe hana uhakika kama kuna pesa za umma humo.
kina zito walishupalia hii ishu kwa maslahi fulani ambayo yanaelekea kukwama sasa.
hii ni aibu sana kwa zito na inakwenda kummaliza asipoangalia.
 
Kwa upande wangu majibu ya Waziri Muhongo ni maelezo ambayo mtu yoyote anayetuhumiwa kwa tuhuma kama ya ESCROW angeyasema. Licha ya maelezo ya Serikali ya kung'ang'ania kuwa pesa ya ESCROW si ya umma, ukweli unabaki palepale.

1. Sawa pesa si za Umma, aliyelipwa ilikuwa halali yake. Kwa nini baada ya malipo waliokuwa watumishi wa umma, wabunge na majaji wamepewa mgawo?. Huoni hapo kuna dili imechezwa.

2. Sawa pesa si za Umma. Mbona wahusika hawakulipa kodi ya serikali baada ya kulipwa wakati hakuna msamaha wa kodi uliopitishwa na Serikali. Badala yake Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye anayesema kuwa kodi kwenye ESCROW Account haipo.

3. Kwa maoni yangu USHABIKI wa KISIASA ndio unalitafuna TAIFA letu. Serikali ichukue hatua stahili kwa yeyote aliyetuhumiwa kuhusika na sakata hili na sio kuanza kuteteana hadharani wakati ukweli ni kuwa PESA za ESCROW zimegawiwa kwa Watumishi wa Serikali na Wanasiasa.
 
It seems you have a point. Conclusion yako imechanganya mambo, umesema fedha za escro si za umma na kwamba kamati ya zitto imepotosha wakati huohuo unasema tena umeeleweka vizuri kwamba anayestahili kulipa vat tra ni muuzaji na umesema iptl alikuwa anamuuzia tanesco umeme na tanesco anamlipa iptl sasa iweje fedha za escro zisiitwe ndani yake kuna fedha za umma????? fafanua kidogo, maana tunapokea maswali mengi kutoka vijijini tunakozaliwa ilituwape maelezo yanayojitoshereza

Ndugu yangu Fugwe

Kama kusingekuwa na mzozo wa capacity charge, Tanesco wangekuwa wanamlipa IPTL moja kwa moja. Kwa maana hiyo escrow isingefunguliwa. Je kama wangelipa kila mwezi kama walivyokuwa wanafanya kabla tungesemaje

Kwakua Tanesco waliamini kuwa huenda wakarudishiwa chao, wakashikilia malipo. Suala la VAT halina uhusiano wa kama uliyemuuzia amekulipa au hajakulipa. IPTL walipaswa kulipa VAT kila mwezi walipotoa invoice kwenda Tanesco na TRA walitakiwa kila mwezi kuhakisha wamelipwa bila kujali kama wao, IPTL hawajalipwa na Tanesco (from escrow now)

Pesa ya escrow wakati wa kulipwa either kwa IPTL au kw Tanesco ingekuwa ni sawa ukusanyaji wa madeni kama wafanyabiashara wengine wote wanavyofanya. Huwezi iambia TRA sikulipi kodi ya VAT eti kwa sababu Tanesco hawajanilipa, wameweka pesa kwenye escrow, sio kweli.

Pesa ya umma katika maana ya kodi ya VAT haimo kwenye hii escrow money. Kama TRA hawakukusanya kwa wakati wakatumia nguvu nyingi kukimbizana na EFD, wawajibishwe wao sio wanasiasa.

CAG NAYE AMECHANGIA KUTOBOA TUNDU LA KUDOKOLEA.

Tanesco katika mahesabu yao walikuwa wanaonyesha pesa ya escrow kama ASSET upande mmoja na kama LIABILTY upande mwingine ili kukeep track.
CAG katika Audit ya 2012 aliigaiza Tanesco kutoripoti hivyo na ndipo TUNDU la kudokoa lilipotobolewa.
 
Hili jambo lilikosewa toka mwanzo. Kwa sasa hakuna sababu ya kunyoosheana vidole. Tusonge mbele kujiletea maendeleo
 
Juzi nilienda kununua mifuko ya cement. Kwenye stakabadhi ya malipo niliyopewa, kuna item ya VAT. Muuzaji wa cement hakunitaka niende kulipa hiyo VAT TRA bali yeye kama muuzaji ndiye aliyekuwa na dhamana ya kukusanya VAT kutoka kwangu na kuiwasilisha TRA
 
Kwa maelezo aliyotoa jana muhongo waziri wa nishati na madini kama kunamtu ambaye hakumwelewa muhongo atakuwa na shida kidogo kwenye kuchambua haya masuala kwani muhongo alichambia vizuri sana na kuweka bayana kila kitu lakini kama bado kunamtu ambaye mpaka sasa hajaelewa inabidi uelewa wake utiliwe mashaka.
 
Ndugu watanzania wote (in the voice of profesa Muhongo)

Tuache Jaziba, tuache kulazimisha mapenzi yetu kutimia,tuwe na subra, tujipe nafasi ya kutafakari na kupima mambo haya, tujiweke katika nafasi ya kuwatendea maadui zetu vile ambavyo sisi tungependa kutendewa.

Na zaidi, tufuate ushauri alioutoa Mheshimwa Lusinde jana jioni bungeni, kwamba, "TUSEME KWELI ILI TUFANYE MAAMUZI YA HAKI"

KUHUSU PESA ZA ESCROW KUWA NI ZA UMA ETI KWA SABABU KULIKUWA NA KODI YA VAT NDANI YAKE
Ndugu watanzania wote.

Huu ni upotoshaji, ni uongo na uzushi ambao tunapaswa kuukataa, jambo lolote linalofanywa kwa uovu mwisho wake huwa sio mwema.

Report iliyowasilishwa na PAC katika bunge letu, japo ilitegemewa kuwa msingi wa kulipatia haki Taifa letu, imekuwa ni chanzo cha aibu kwa Taifa zima, hutuwezi kupigania maslahi ya Taifa letu kwa kusema uongo, kuficha ukweli kwa wingi wa meneno yaliyopindishwa pindishwa na kupambwa kwa lugha za ghirba.

UKWELI NI HUU
Kama ambavyo mahusiano ya IPTL na TANESCO yanajurikana, hawa walikuwa na bado wanaendelea kufanya biashara pamoja, IPTL akiwa muuzaji na TANESCO Mnunuzi.

Bila kuzingatia namna wanavyofikia bei ya bidhaa husika, ni wazi IPTL imekuwa ikiipatia INVOICES Tanesco, Ili Tanesco Iilipe IPTL.

Sheria yetu ya kodi ya VAT ya mwaka 1997, imetoa maelekezo yanayowapa wafanyabishara FURSA ya kukusanya kodi ya VAT kutoka kwa wanunuzi wa bidhaa zao, kwa niaba ya TRA.

Kutokana na vigezo vilivyowekwa katika sheria husika, IPTL nao ni wakara wa TRA katika kukusanya kodi ya VAT kutoka Tanesco.

Kutokana na mahusiano ya kibishara kati ya TANESCO NA IPTL, TANESCO Haina mamlaka mpaka leo ya kuchukua maamuzi ya kutoilipa IPTL VAT eti ipeleke VAT hiyo TRA yenyewe.

Hivyo basi, hata katika PESA zilizokuwa kwenye ACCOUNT YA ESCROW, TANESCO walitekeleza wajibu wao wa kisheria na kibiasha kuziweka hela hizo kwenye account hiyo zote za IPTL pamoja na VAT (Ambazo kimsingi zote ni za IPTL), Na wakati malipo yanafanyika kutoka account hiyo, YALIFANYIKA KWA USAHIHI KABISA Kwa PESA zote KULIPWA kwa IPTL. Kwa sababu ni wajibu wa IPTL kukusanya VAT kutoka Tanesco.

TRA walipaswa kuidai IPTL pesa hiyo ndani ya mwezi mmoja baada ya IPTL kuipatia INVOICES Tanesco, bila kujali kama IPTL wanaubishani na Tanesco juu ya usahihi wa INVOICE AMOUNTS au la?.

Huu ndio utaratibu, sio mpya, na wote tunaufahamu, jana nimetoa mfano ambao haukueleweka, ukienda dukani kununua bidhaa, unaambiwa bei ya bidhaa ambayo ndani yake kuna VAT, ukifanya maamuzi ya kununua unamlipa muuzaji pesa zote, NA KUANZIA HAPO ZINAKUWA ZAKE na wewe bidhaa inakuwa yako rasmi.
Swala la wafanyabishara kutopeleka makusanyo ya VAT TRA ni tatizo lingine.

HIVYO BASI
Kama sababu ya msingi ya kudai kwamba zile pesa ni za UMA ni sababu ya VAT COMPONENT KWA ZILE HELA, HUO NI UONGO NI UPOTOSHAJI.

Nawasilisha.
SAGHANKA... HEBU TUAMBIE Tanesco ni kampuni inayomilikiwa na akina nani kama sio shirika la umma? Na hela inayopatikana kutoka na biashara inayofanywa na kampuni ya umma (Mfano Bandari, TTCL, POSTA etc) hizo hela ni za uma au la... hizo kampuni ikiwemo Tanesco inapofanya malipo ya aina yeyote kwa wateja wake akiwemo IPTL inafanya malipo hayo kwa niaba ya nani kama sio Umma? Baada ya hapo kumbuka kwamba hata Lusinde naye alishangaa hivi ni nani aliyempa AG uwezo wa kusamehe kodi... Jambo la tatu ni kwamba tunachopigania humu ni uadilifu wa wale tuliowachagua kutuongoza.. sasa unapoambia Muhongo aliomba Rusha kwa kiambatanish cha barua ya singasinga kwa PAC , sijui wewe unalizungumziaje hilo.... muomba, mtoaji na mpokeaji wa rushwa wote huwa ni wahujumu uchumi na huwa wanaadhibiwa.. sasa ni kwa nini wao akina muhingo wanaona vigumu kuachia ngazi kwa hilo tu la kuomba rushwa ili wawe madarali ? kitu kingine I kwamba ndani ya miaka 9 tu, serikali imeteteleka kwa mambo haya haya ya ufisadi .. sasa mtu wa kujipima sio Pinda, Lowasa wala muhongo, ni yeye mwenyewe kikwete ajondoe na arudishe madaraka kwa wananchi wawake viongozi wengine.. hata yeye mweyenye alisema anataka kuchunga Ngombe na sijui ni nani aliyemwambia kuchunga ngombe ni kazi rahisi.. najua unakumbuka pale Kenyamonta jinsi hiyo kazi ya kuchunga ngombe ilivyokuwa ngumu halafu leo hii anasema amechoka anataka kuchunga ngombe , ni kudhalau kazi za watu.. kama amechoka inabidi astaafu hata kwa manufaa ya umma kuliko kila siku kututeulia watu wanaotuletea ufisadi kila kona...na hili la IPTL ameliteta yeye, kwa nini asiwajibike tangu akiwa waziri wa nishani.. ni msanii tupu... ameweka history kwamba amepinduliwa na wabunge kuliko Rais yeyote Tanzania na sasa aondoke tu kuliko kuwalazimisha wenzake wastaafu au kujiudhuru...
 
Hili jambo limekuzwa na kuchafuliwa na wanasiasa ndipo watu walipoanza kuyumba kwa kufuata mielekeo ya wanasiasa bila kupata mda wa kuchambua haya mambo kwa undani.
 
Juzi nilienda kununua mifuko ya cement. Kwenye stakabadhi ya malipo niliyopewa, kuna item ya VAT. Muuzaji wa cement hakunitaka niende kulipa hiyo VAT TRA bali yeye kama muuzaji ndiye aliyekuwa na dhamana ya kukusanya VAT kutoka kwangu na kuiwasilisha TRA

Muuzaji yuko sahihi kabisa kama ambavyo IPTL alivyotakiwa kulipa VAT miaka yote. Kama hakulipa, mbona mitambo ipo??? TRA si wakamate mitambo???
 
Back
Top Bottom