Pagan Amum
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 1,930
- 4,409
Katika watu wanaomkwamisha Magufuli kwenye azma yake ya kuifanya Tanzania iwe ya viwanda, wa kwanza ni BRELA....
chek inbox.nimekutumia textImani iwe kwenu Wakuu!
Baada ya mdau moja kuleta uzi leo kuhusu BRELA, naomba nisaidie kuweka record sahihi. Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Mimi ni mteja wa BRELA wa miaka mingi, ukweli ni kwamba BRELA ile ya enzi zile siyo hii ya sasa. BRELA ya sasa wanajitahidi sana kwenda na wakati hususani siku za karibuni
Kwa sasa huduma ya kusajili jina la biashara hutolewa kwa njia ya mtandao kwa Tsh. 20,000 tu, popote ulipo Tanzania, awali ilikuwa inakulazimu kusafiri kwenda Dar es Salaam kusajili jina la biashara
Pia, kupata taarifa za makampuni hususani, majina ya wanahisa, wakurugenzi, ofisi za kampuni na mtaji wa kampuni huduma hizo sasa inapatikana kwa njia ya mtandao
Vile vile ukitaka kusajili kampuni awali ilikulazimu kuandika barua na kupeleka kwenye ofisi za BRELA (DSM) kuomba jina hilo unalotaka kusajili kuhakikiwa kama hakuna kampuni nyingine iliyosajiliwa kwa jina hilo hilo, sasa hivi huduma hiyo inatolewa kwa njia ya mtandao na ni bure, ila ukiwa unapenda jina hilo litunzwe kwa muda wa siku 60 itakulazimu kulipa nafkiri Tsh. 50,000 tu. Na hii ni kwa mujibu wa sheria za makampuni
Pia, malipo ya huduma zote za usajili sikuhizi hulipwa kwa njia ya mtandao; Mpesa, Tigopesa, Fahari huduma, Simbanking, Mobile banking, matawi yote ya CRDB, matawi yote ya NMB Tanzania nzima.
Mwisho, naomba niwasihi wana Jukwaa hili na wananchi wote, kwa kuepuka upotoshaji kama ulivyoletwa humu JF kwa makusudi yake binafsi, ni vyema tujenge tabia ya kupata taarifa zaidi za usajili wa makampuni kwa kuwatembelea ofisini kwao moja kwa moja ama kwa njia ya mtandao www.brela.go.tz (Hapo utapata kila kitu, na sio ule upotoshwaji uliofanya na member mwenzetu wa JF)..
Asanteni!
BRELA kuna urasimu sana nilitaka kusajili kampuni nikashindwa hasa wa mikoani mpaka uende makao makuu Dar na bado ukifika huko unazungushwa weeee hata online ndio hakuna kitu website yao hata ku update shida habari toka za mwaka juzi ndio hizo hizo wanahitaji kubadilika sana
una tabia ya majungu,chek inbox.nimekutumia text
una tabia ya majungu,
anyway,brela wanajitahidi sana,na hii ni taasisi nyeti kwa usalama wa nchi,hawawezi kukurupuka tu na kukusajiria kampuni yako hata kama.ina malengo ya kigaidi na kuuza madawa ya kulevya.
pia si mbaya mtu kusajili kampuni ndani ya siku mbili tatu au maximum wiki moja,una haraka ya nini?unawahi kutapeli au?
la msingi nafikiri imefika wakati wawe na ofisi za kanda,dar,mwanza,arusha
Mtoa mada kwa heshima naomba nitofautiane na wewe. BRELA bado sana tena sana na inalekea hata Brela wenyewe haelewi ni wapi wana mapungufu. Kwa mfano unasema kuwa siku hizi huduma za usajili zinapatikana kupitia kwenye mtandao wao. Lakini sielewi ni kwanini inachukua zaidi ya saa 12 kufanya usajili kwa kutumia mtandao. Jaribu kufanya usajili Singapore, ndani ya dakika kumi umemaliza mchezo, Brela ni utani mtupu.
Kama Brela wanakubaliana na hoja yako kuwa wanatoa huduma nzuri basi tuna tatizo kubwa zaidi. Tuko kwenye dunia ya ushindani, nchi nyingine wanafanya mageuzi makubwa kwenye taasis kama ya Brela ili kuweka mazingira rafiki ya biashara. Hapa Tanzania inalekea Brela wamejiwekea viwango vya chini mno. Na ukienda kwenye Ofisi zao - tena makao makuu ni zogo tupu utafiki tuko kwenye industrial revolution era. Inatia aibu kweli.
BRELA bado hawajajipanga bado msitetee ujinga tenda mmwambie anaesimamia tovuti yao awe shapu kubadilisha taarifa mara kwa mara kama kazi inawashinda waseme
taarifa ipi ilichelewa kubadilishwa?hii nchi ndio maana muingereza alikataa umoja wa mataifa wakamuomba akae nayo kwa muda mpaka.ipate uhuru,uhuru wenyewe tuliupata kwa maneno,ndio maana kila siku maneno,mpaka miaka hamsini ya uhuru tumejaa manenoBRELA bado hawajajipanga bado msitetee ujinga tenda mmwambie anaesimamia tovuti yao awe shapu kubadilisha taarifa mara kwa mara kama kazi inawashinda waseme
Sidhani kama inachukua masaa 12. Last time ilinichukua masaa 2 Mkuu. Like two weeks ago...
Infact nakubaliana na issue ya IT department yao kuwa inactive
Hayo maelezo ya historia ungewafundisha wanafunzi ingependeza kwenye tovuti yenu mnaona ipo sawa kabisa tunavyo apply kupata hiyo fomu ya kusajili jina la kibiashara/kampuni? Halafu mpompo tu hamna ushawishi wowote kwa wateja hata kujitangaza ni kazitaarifa ipi ilichelewa kubadilishwa?hii nchi ndio maana muingereza alikataa umoja wa mataifa wakamuomba akae nayo kwa muda mpaka.ipate uhuru,uhuru wenyewe tuliupata kwa maneno,ndio maana kila siku maneno,mpaka miaka hamsini ya uhuru tumejaa maneno